Adeladius Makwega-MWANZA
Asubuhi ya Februari 9, 2024 Mwanakwetu alikutana na video
fupi kwenye anuani hii,
https:www:facebook.com/share/r/pAnSuwGyFzxfcgf/?mbextid=oFDknk,
ikiwaonesha vijana wawili wakiwa wamevalia sare za CCM, mashati
ya kijani, mmoja la mikono mirefu na mmoja la mikono mifupi, huyu wa mikono
mifupi amevaa kofia na miwani juu yake, wote wamevaa suruali nyeusi.
Kunogesha uroda wao wa kupanda boda boda hiyo aliyepakizwa akishika
na bendera ya CCM mkono wa shoti. Akilini kwa Mwanakwetu ilimjia taswira kuwa
ni yaleyale yanayolalamikiwa katika ziara za ndugu Paul Makonda-Katibu Muenezi
CCM Taifa.
Mwanakwetu akasema moyoni,
“Vijana wanafanya mikogo katika vyombo vya moto! Jamani
pikipiki siyo baiskeli, eti ukaweka miguu migoko breki , hapo hakuna bampa,
hapo bampa ni mwili wako.”
Mwanakwetu akasema tena moyoni.
“Hawa jamaa wanakiharibia sana Chama Cha Mapinduzi, bila ya wao
kuliona hilo lakini pia wanalipa Jeshi la Polisi Tanzania wakati mgumu sana
katika kusimamia Sheria na Kanuni za Usalama Barabarani, labda askari hodari wa
usalama barabarani bado wapo likizo za mwaka mpya ?”
Mwanakwetu aliangalia na kunukuu namba
ya pikipiki hiyo kuwa ni MC 841 DVX na mara akayasikia maneno kutoka kwa abiria
aliyepakizwa akisema
“...eeee bwana eee , siyo
lazima upande hiyooo...”
Mwanakwetu alipotazama jina la
ukurasa huo ulikuwa ukiitwa Dodoma Zone
na ukifuatiliwa na watu 243 K , huku video hiyo ikitazamwa na watu 1.2 K na waliotoa
maoni yao ni watu 1.4K hadi Februari 9, 2024.
Mwanakwetu alipowatazama vizuri wahusika
hao alibaini kuwa sura hizo zinafanana wanasiasa wa Tanzania ambao ni wabunge
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Antony Mavunde ambaye ndiye
Waziri wa Madini wa Tanzania na Deo Ndyejembi ambaye ni Naibu Waziri wa TAMISEMI
ambazo zote ni Wizara za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mwanakwetu akastajabu sana moyoni mwake
kumbe Mawaziri/Mawaziri Wadogo Wanapenda Uroda wa Bodaboda!
Hawa ni mawazri ambao kwa nafasi yao
ya Ubunge na Uwaziri wanayo magari yanayoendeshwa na madereva na wasaidizi wao
labda wapo likizo.
Kwa nia yao, wao wenyewe waliamua
kupanda pikipiki hiyo na kurekodiwa, huku mmoja kuwa dereva wa pikipiki hiyo, maswali
ni je huyo dereva anayo leseni ya kuendesha pikipiki? Tuamini anayo, swali la pili,
je kwa nini hawakuvaa kofia za kujikinga na ajali?
Hawakumbuki Mwanakwetu anasema,
“Vijana wanafanya mikogo katika vyombo vya moto, jamani
pikipiki siyo baiskeli eti ukaweka breki migoko, hapo hakuna bampa, hapo bampa ni
mwili wako.”
Kwa mwaka 2023 yupo mbunge mmoja aliyefariki
kwa ajali ya bodaboda na hilo kusababisha kufanyika kwa uchaguzi wa jimbo na
jimbo hilo likapata mbunge mpya , kufanyika uchaguzi wa kuziba pengo ni gharama
kwa taifa letu, hilo litokee kwa bahati mbaya sawa na siyo kwa kujitakia, pesa
hizo ziende hata kujenga zahanati vijijini.
Kwa hakika video hiyo ya Mavunde na
Ndyejembi imemkwaza sana Mwanakwetu siku ya leo.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Kwa mwaka 2023 yupo mbunge mmoja aliyefariki
kwa ajali ya bodaboda na hilo kusababisha kufanyika kwa uchaguzi wa jimbo na
jimbo hilo likapata mbunge mpya , kufanyika uchaguzi wa kuziba pengo ni gharama
kwa taifa letu, hilo litokee kwa bahati mbaya sawa na siyo kwa kujitakia, hapo
heri pesa hizo ziende hata kujenga zahanati vijijini.
Je Antony Mavunde na Deo Ndejembi
hawaoni kwa kufanya hivyo nia yao ni kuisababishia Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania hasara ?
Je wao kama mawaziri hawaoni kuwa
kufanya hivyo wamevunja Sheria na Kanuni za Usalama Barabarani na wanapaswa
kuadhibiwa mara moja?
Kwa hakika video hiyo inaonesha wazi
na fika kuwa papo mahali pana shida, lazima pafanyiwe maarifa mapema sana,
maana kitendo hicho hakitoi picha na fundisho bora kwa watoto na vijana wadogo
wa Kitanzania.
Kwa hivi sasa ukienda trafiki na
mahakamani, utakutana na waendesha mashtaka, polisi na mahakimu wakipata tabu
na mashauri mengi ya kukiukwa kwa Sheria na Kanuni za Usalama Barabarani.
Je Antony Mavunde na Deo Ndyejembe
kwa kufanya kitendo hicho hawaoni kuwa ni kuwakatisha tamaa Kikosi cha Usalama
Barabarani, Waendesha Mashitaka na Mahakimu/ Majaji wa Tanzania?
Mwanakwetu anawaambia ndugu hao wawili
watambue kuwa Ubunge waliona na hata huo Uwaziri siyo mali yao, bali ni mali ya
Watanzania, ili wao wabaki salama katika nafasi hizo wanawajibika kuheshimu
Sheria zetu zote ikiwamo hii ya Usalama Barabarani na Kanuni zake.
Mwanakwetu kwa heshima zote anawaomba
Jeshi la Polisi Tanzania hasa Kikosi cha usalama Barabarani, Waendesha Mashtaka
na Mahakimu/ Majaji msikate tamaa nyie fanyeni kazi na anzeni na hilo la Mavunde
na Ndyejembi.
Kama Waziri anashindwa kuheshimu
Sheria na Kanuni za Usalama Barabarani hadharani ambayo inamlinda hata yeye kwa
uhai wake, je ataweza kweli kulinda Sheria na Kanuni za madini ambayo ni mawe
tu hata likichukuliwa yeye hapati madhara yoyote mwilini? Au anaweza kweli kuheshimu
na kulinda sheria ndogo ndogo za halmashauri
zetu anazozipitisha ?
Mwanakwetu upo?
Kumbe Mawaziri Wanapenda Uroda wa
Bodaboda EeeH
Nakutakia siku Njema
0717649257
Usiwe na shaka, hiyo inaitwa joyride, na sio trip!. Joyride ni pale mtu yoyote anapoendesha chombo chochote cha moto kwa umbali mfupi just for enjoyment.
ReplyDeleteKwa viongozi ni for Publicity stunts for display only ili wapiga kura wao wawaone ni wenzao, hivyo hawahitaji kuvaa kofia wala kuwa na leseni, hata Rais Samia alipovuta ile mashine kubwa 4x4 hardtop kwenye filamu ya Royal Tour, alipaswa kuwa na leseni ya class C, but that was just
a joyride, karibu hotel za kitalii zenye water sports watu wanaendesha speed boats, na scabs scuba bila leseni.
Na kwa taarifa yako hata kuendesha baiskeli wanapaswa kuwa na kofia na mavazi maalumu yenye reflectors lakini sisi Bongo hatuna hizo
Nimekuja blog yako kufuatia changamoto uliyokutana nayo kwa makala ya UDOM.
Pole kwa maswahibu hayo tuko na wewe@.
Pasco
Post a Comment