NDEGE WANNE WA ASKOFU MWAMAKULA

 



Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula

Mzizima –Dar es Salaam

Akiwa amezungukwa na maaskofu wengi, saa 5 usiku wa Juni 2 , 2025 , Askofu Gwajima akiutangazia ulimwengu kuwa Kanisa lake limezingirwa na Polisi wakiwa 2na difenda 3. Wakati akitangaza hayo, Askofu Gwajima, maaskofu, wachungaji na waumini walikuwa ndani ya Kanisa hilo pale Ubungo.

 

“Muda mfupi kabla, nilikuwa nimetuma ujumbe kwa mamlaka kuuliza kama barua mbili ambazo zilisambaa mitandaoni juu ya kufutiwa usajili wa Kanisa la Ufufuo na Uzima zilitoka kwao? Lakini sikupata majibu. Lakini nitaandika zaidi juu suala hili la barua baadaye.

 

Nilijipumzisha mapema na kulala kama 'maiti' kutokana na uchovu uliojilimbika, kwa sababu hiyo sikujua kilichojiri hadi asubuhi hii wakati nilipotafutwa na watu kadhaa kuhusu suala hili la Askofu Gwajima.”

 

Kwa hakika msomaji wangu hali ilikuwa hivyo,

 

“Nilijitia purukushani kutaka kujua kilichompata Askofu Gwajima, namba zake hazikupatikana na hata za wasaidizi wake muhimu. Niliingiwa na wasiwasi nikidhani watakuwa wametoweka naye au 'wamemtokomeza'! Lakini nilishauriwa na hisia kuwa huenda hajachukuliwa kwa hiyo niliwatuma njiwa tetere, ndege mnana na ntiiti wakatafute kujua ukweli zaidi pale Ubungo.

 

Njiwa tetere walikuja na majibu ya kuwa Polisi hawakufanikiwa kumkamata Askofu Gwajima! Walieleza zaidi kuwa alipita katikati yao baada ya kuvalishwa dela akaonekana kama mama mwenye mapepo aliyekwenda kuombewa!”

Kwa hakika mimi Baba Askofu Mwamakula naendelea kusimulia kisa hiki nikisema,

 

“Ndege mnana walikuja na majibu kuwa Polisi hawakufanikiwa kumkamata Askofu Gwajima! Wao walisema kuwa 'upepo wa kisulisuli' ndio uliomtwaa kwa hiyo hawajui alikwenda wapi!

 

Ntiiti nao walikuja na majibu ya kuwa Polisi pia hawakumuona Askofu Gwajima kwani alivalia kama wale maaskofu lakini alijibadilisha sura na hivyo walimpita bila kumtambua, akasepa!

 

Lakini sikuridhika na majibu yao, nilituma tena ndege aina ya jwegele. Huyu akaja na maelezo ya ziada kuwa alimuona mama mmoja kwenye chumba kimoja cha maombi akikemea pepo kimya kimya akiwa katikati ya vijana pamoja na wanawake wengi. Alipochunguza zaidi alihisi alikuwa ni yule mtu wa 'kuliamsha dude'. Hivyo, Polisi hawakuweza kumtambua na baada ya muda kidogo alitoka kupitia mlango wa mbele.”

 

Kwamba Askofu Gwajima hayupo mikononi mwa Jeshi la Polisi, hadi sasa ni jambo ambalo limethibitishwa na ndege wote wanne. Lakini kuna taarifa ya kunguru inasema kuwa Askofu Gwajima aliendelea kubaki Kanisani kwa muda mrefu bila Polisi kumtambua! Kwamba alitoka nje katika mazingira ya kutatanisha, ni moja ya mambo yanayowafikirisha 'Wanyanyembe'!

 


Pengine swali hapa ni kuwa, Askofu Gwajima ataendelea kuwa adimu hadi lini?

 

“Kwa vyovyote vile, Askofu Gwajima atajisamilisha mbele ya mamlaka yeye mwenyewe akiwa ameongozana na maaskofu, wachungaji, wazee na maelfu ya waumini! Na hii itakuwa ni salama zaidi kwake kuliko ile ya kuchukuliwa usiku kama kinda la bata maji!

 

Haitakuwa kosa na wala pia haitakuwa dhambi kwa waumini kufuatana naye au kumsindikiza Askofu Gwajima katika Kituo cha Polisi kama watapata taarifa juu siku, tarehe, muda na jina la kituo! Ila swali linabaki kuwa ni kwa namna gani Askofu Gwajima alifanikiwa kuukwepa ule mkono wa wakamataji pale Kanisani usiku? Je, alitwaliwa na gari la farasi na wapanda farasi wake kama ilivyokuwa kwa Nabii Eliya? ”

 

Je, Askofu Gwajima ni jasusi lililofuzu mafunzo ya kikomandoo ya Kabila la Benyamini? Je, hao Polisi walifanikiwa kumtwaa Askofu Gwajima na sasa wanamshikilia katika Kituo cha Polisi kimojawapo? Je, hao ndege waliotumwa katika kusaka taarifa za Gwajima walipata taarifa hizo kutoka kwa watu wa mfumo hivyo wamezileta hizi taarifa kwa Askofu Mwamakula ili kusudi aamini kuwa Askofu Gwajima hayuko katika mikono ya Polisi lakini lengo likiwa kupumbaza fikra ili nguvu za kupiga kelele zipungue?

Lakini kwa nini mamlaka au serikali inatumia nguvu kubwa sana kupambana na Askofu Gwajima? Je, Askofu Gwajima pia atapewa kesi ya uhaini kama alivyopewa Tundu Lissu?Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!


 

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

 Mwanakwetu amejawa na maswali mengi juu ya haya ,Je harakati hizi ndizo zitakuwa tamati ya Kanisa la Ufufuo na Uzima? Msomaji wa Mwanakwetu nakukumbusha kuwa sababu mojawapo ya Ukristo kuenea ulimwenguni ni matukio ya kutisha kama vile mauwaji yaliyofanywa na mfalme Nero mwaka 64 baada mwaka 303 yaliyofanya na mfalme Dioctratian Wakristo waliuwawa sana waliogoma kuikana imani yao. Hta Utaratibu wa Wakristo kusali ulikuwa watu wanaitana kwa siri lakini baadaye wakaruhusiwa kutumia ishara mbalimbali hadi baadae zitatumika kengele hizi zinazotumika hadi sasa, changamoto hizo na nyingine tele zilisaidia mno Wakriso kueneza imani yao ulimwenguni.


 

Mwanakwetu upo?

 Kumbuka tu

“Ndege Wanne wa Baba Askofu Mwamakula.”

 

Nakutakia siku njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257



 








 

0/Post a Comment/Comments