NYARAKA YA ZAMANI YA TBC.

 

Adeladius Makwega – Ofisi ya Rais, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Dodoma

 

Asubuhi ya Oktoba 22, 2026, Mwanakwetu alitembelea Idara ya Usimamizi wa Kumbukumbu katika Ofisi ya Rais, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, jijini Dodoma.

 

Akiwa katika pitapita hiyo, Mwanakwetu alipokelewa kwa mikono miwili na Bi. Adolphina Mapala, Afisa Kumbukumbu katika Idara hiyo. Bi. Mapala ni mwenye asili ya kabila la Wafipa, kutoka Kata ya Katumba, Sumbawanga, mkoani Rukwa.

 

Katika mazungumzo haya, Bi. Mapala alimwonesha Mwanakwetu nyaraka ya kihistoria yenye umri unaokaribiana na kipindi cha kuelekea Uhuru wa Tanganyika.

 

Nyaraka hiyo ilikuwa ni hati ya maandalizi (script) ya makala iliyotayarishwa na Shirika la Utangazaji Tanganyika (TBC) na kurushwa hewani Septemba 10, 1961. Makala hiyo ilihusu historia ya eneo la Mvumi, ambalo kwa sasa linapatikana katika Mkoa wa Dodoma.

 

Ugunduzi na uhifadhi wa nyaraka za aina hii una umuhimu mkubwa katika kuendeleza uelewa wa historia ya maeneo mbalimbali nchini. Kupitia nyaraka za zamani, vizazi vya sasa na vijavyo vinaweza kujifunza kuhusu maisha, mazingira na matukio yaliyounda historia ya jamii zetu.

 

Kwa hakika, nyaraka za zamani ni hazina ya maarifa; zinapotunzwa vizuri, huwa daraja linalounganisha kizazi cha jana, cha leo na cha kesho.

Mwanakwetu upo?Kumbuka.

“Nyaraka ya Zamani ya TBC.”


 

Nakutakia siku njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257


 



 









 




0/Post a Comment/Comments