Eh ehhh… (Eeh ehhh…)
Doria barabarani… (Sawa sawa!)
Redio yaita kituoni… (Copy that!)
Kiungo kikivunjika je? (Bini vuu!)
Control! Control! — tunaanza doria!
Nimepigiwa simu — redio yalia kituoni (kituoni!),
“Control to unit — ajali imetokea njiani!” (njiani!),
Maafande doria — wakakimbiza mwendo kasi (mwendo kasi!),
Wakidhani maandamano — leo yangewaka wazi (wazi!).
Siren zikalira — wee woo! wee woo!
barabarani (barabarani!),
Lakini walikuta kimya — hakuna tukio mitaani (mitaani!),
Ghafla Defender layumba — katikati ya njia (ya njia!),
Tie rod end yakatika — ikakata mawasiliano ya njia!
Unit! Unit! — ripoti kwa control!
Kiungo kimekatika — tumepoteza control!
Tie rod end — oooh imekatika!
(Heeey!)
(Bini vuu! Bini vuu!)
Usukani mkononi — lakini haushikiki! (Weeh!)
(Bini vuu! Bini vuu!)
Control hatuna — gari layumba-yumba,
Ukikosa kiungo — safari yote inaanguka!
Walikuwa standby — wakisubiri amri kutoka juu (kutoka juu!),
Dispatch ikasema — “hakikisha mnafika mapema huko!”
Wakaongeza mwendo — doria ikawa kali (kali!),
Lakini wakakuta ukimya — hakuna maandamano wala hali.
Kushoto kulia — gari lavutwa bila
ridhaa (ridhaa!),
Afande dereva — akapoteza control ghafla (ghafla!),
Backup haijafika — tukio latokea njiani (njiani!),
Ajali ikatokea — kabla ya kufika kituoni (kituoni!).
Hata bila maandamano — maafande
wakaumia (wakaumia!),
Hatari haipangiwi — huja bila taarifa!
Control! Control! — hali si shwari!
Kiungo kimekatika — hatuwezi kuongoza gari!
Tie rod end — oooh imekatika!
(Bini vuu! Bini vuu!)
Usukani mkononi — lakini haishikiki!
(Bini vuu! Bini vuu!)
Njia inapotea — gari layumba-yumba,
Ukikosa kiungo — safari yote inaanguka!
Eeeh… (Copy that…)
Jamii nayo ina kiungo chake (kiungo chake…),
Sauti za watu — ndizo njia yake (njia yake…),
Ukizizima… ukizifunga… ukizizuia (zuia!),
Ripoti itasema — mwelekeo umepotea dunia!
Kama doria bila control — haifiki salama,
Jamii bila sauti — hupoteza mwanga na dhamira,
Maandamano ya amani — si tukio la vurugu,
Ni taarifa ya wananchi — kwa njia iliyo tulivu.
Ukizuia mara kwa mara — bila sababu
ya msingi,
Ni kama gari la doria — linaenda bila kiungo msingi,
Tahadhari yatolewa — kama ripoti ya mwisho,
Tusivunje vinavyotuunganisha — tusipoteze mwelekeo.
Tie rod end — oooh imekatika! (Wote sasa!)
(Bini vuu! Bini vuu!)
Usukani mkononi — lakini haishikiki!
(Bini vuu! Bini vuu!)
Control imepotea — gari layumba-yumba,
Ukikosa kiungo — safari yote inaanguka!
Chini ya mwembe Dodo — wakisubiri
backup (backup!),
Wakitoa ripoti — kwa sauti ya pole na makeup,
(Bini vuu… bini vuu…)
Control… Control… safari imekatika…
(Bini vuu… bini vuu…)




Post a Comment