WAZIRI MKUU MWIGULU NCHEMBA KUFANYA ZIARA YA KWANZA MKOANI MARA

 

Adeladius Makwega – Mara

Wananchi wa Mkoa wa Mara wanaigoja kwa hamu ziara rasmi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba (Mb), itakayofanyika kuanzia Julai 1 hadi 5, 2026.

 

Wananchi kutoka Serengeti, Bunda, Tarime na Butiama wameeleza kufurahishwa na ujio huo, wakisema ni fursa muhimu ya kumuona Waziri Mkuu na kuwasilisha maoni yao kwa serikali.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Alfred Mtambi, ziara hiyo itahusisha ukaguzi, uzinduzi na uwekaji wa mawe ya msingi kwa miradi saba ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 52.9.

Ratiba ya ziara hiyo inajumuisha wilaya za Serengeti, Tarime, Rorya, Butiama, Musoma na Bunda, ambapo pia Waziri Mkuu atafanya mikutano kadhaa ya hadhara.

 

Hii ni ziara yake ya kwanza mkoani Mara tangu kuteuliwa kwake baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2026, na hivyo kuwa Waziri Mkuu wa pili kutembelea mkoa huo tangu mwaka 2024, akitanguliwa na mtangulizi wake, Mheshimiwa Kassim Majaliwa.

makwadeladius@gmail,com

0717649257










0/Post a Comment/Comments