Adeladius Makwega – MBAGALA
Juni 10, 2026
Mwanakwetu alikutana na ndugu zake kadhaa, watunzaji wa kumbukumbu na waandishi waendesha ofisi kutoka taasisi mbalimbali, akawa anawatania:
“Jamani, ile posho yenu ya maziwa tunajiandaa kuiondoa, maana sasa tumeshahama kutoka analojia na kuhamia mfumo wa kidigitali.”
Hawa jamaa wakacheka sana.
Mmoja wao akaongea kwa utani: “Au ndilo yale ya Biblia ya mkulima na talanta moja? Huko tusifike, maana vumbi bado lipo na maziwa bado yanahitajika!”
Ndugu mmoja akasema:
“Utunzaji
wa kumbukumbu na maendeleo ya kidigitali ni mada muhimu inayohusisha jinsi
taarifa zinavyohifadhiwa, kusimamiwa na kutumika kwa kutumia teknolojia ya
kisasa.
Utunzaji wa kumbukumbu ni mchakato wa kukusanya, kuhifadhi na kupanga taarifa
ili ziweze kutumika baadaye. Kumbukumbu zinaweza kuwa nyaraka (karatasi),
takwimu, picha, sauti, video au faili za kidigitali (kwenye kompyuta au simu).”
Akaendelea kusema kuwa kazi hiyo bado ipo, kwani hata kama zamani kumbukumbu zilihifadhiwa kwenye mafaili ya karatasi, sasa zinahifadhiwa kwenye kompyuta. Hivyo, matumizi ya teknolojia hayawezi kuondoa umuhimu wa kazi hiyo—wala posho ya maziwa!
Wenzake wakacheka tena kwa nguvu, huku wakiongeza:
“Umuhimu wa utunzaji wa kumbukumbu ni pamoja na kusaidia kufuatilia maendeleo (mfano mapato na matumizi), kuwa rejea wakati wa kufanya maamuzi, kuongeza uwazi na uwajibikaji, kusaidia kupanga mipango ya baadaye, na kurahisisha mawasiliano pamoja na utoaji wa taarifa.”
Jamaa mwingine, ambaye ni mwandishi mwendesha ofisi, akasema:
“Maendeleo ya kidigitali ni matumizi ya teknolojia kama kompyuta, intaneti na simu kuboresha shughuli mbalimbali kama mawasiliano, elimu, biashara, kilimo, ufugaji, uvuvi na huduma za jamii. Teknolojia imefanya kazi kuwa rahisi, haraka na yenye ufanisi zaidi.”
Mwisho Bi Ester Musa Mwangaza, ambaye pia ni mwandishi mwendesha ofisi, akaema:
“Maendeleo ya kidigitali yamebadilisha sana namna kumbukumbu zinavyotunzwa. Sasa kumbukumbu zinahifadhiwa kwenye kompyuta au ‘cloud’ badala ya karatasi. Ni rahisi kutafuta na kupata taarifa haraka, hupunguza hatari ya kupotea au kuharibika kwa kumbukumbu, na huruhusu upatikanaji wa taarifa popote na wakati wowote.”
Baadaye, Mwanakwetu aliagana na ndugu hawa kisha akaenda kuyaandika makala haya.
Mwanakwetu anasema nini leo?
Faida za kutumia mfumo wa kidigitali katika utunzaji wa kumbukumbu ni pamoja na kuokoa muda na gharama, kuongeza usalama wa taarifa, kurahisisha uchambuzi wa data, na kuboresha maamuzi pamoja na mipango.
Kwa ujumla, utunzaji wa kumbukumbu ni msingi wa maendeleo yoyote. Maendeleo ya kidigitali yameboresha sana namna kumbukumbu zinavyohifadhiwa na kutumika. Kwa pamoja, vinasaidia kuongeza ufanisi, uwazi na maendeleo katika jamii na taasisi.
Mwanakwetu anawaambia rafiki zake watunzaji wa kumbukumbu na waandishi wa waendesha ofisi kuwa sasa ametambua kuwa kumbe ile posho ya maziwa haiwezi kuondolewa na sasa Mwanakwetu amekacha ule mpango wake wa kumwambia Katibu Mkuu Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ndugu yake Juma Seleiman Mkomi juu ya kuiondoa posho hii maana kazi bado zipo nyingi.
Mwanakwetu upo? Kumbuka:
“Tutawapokonya posho ya maziwa.”
Nakutakia siku njema.
Mawasiliano:
Barua pepe: makwadeladius@gmail.com
Simu: 0717 649 257
.gif)
.gif)
.gif)
.gif)
Post a Comment