.gif)
Adeladius Makwega-DODOMA
Msomaji wangu unaweza ukajiuliza je kwanini Mwanakwetu anamzungumzia wakili
Phidelis Mwidunda? Kwa hakika hii nyaraka yangu iliyokwenda katika Bodi ya
Rufaa ilitayarishwa na Ndugu Peter Pinda, mheshimiwa sana, katika hatua za
kukusanya ushahidi, hilo nina hakika nalo kwa asilimia 100 lakini hata kuandika
katika hatua za awali hadi mwisho.
Nina hisi kuwa kumshirikisha huko kulikuwa kwa mawasiliano ya simu tu. Kama mheshimiwa sana asingaliniambia kuipelekea nakala hiyo nisingali fahamu kuwa ndugu huyu alishiriki kuitayarisha nyaraka hiyo.
Ndiyo kusema kwa ukweli wa Mungu, Wakili Mwidunda hakunihoji chochote na wala hakukutana na akina Ibrahimu Liguo, Atanas Luis na Hamisi Ramadhani (Rashidi Kazyoba)Edgar Chibula wille John,Emmanuel Yesaya na wengine ambao hadi leo hii wapo hai.
Kwa kuwa msomaji wangu katika matini iliyotangulia nimezungumzia kwa kiasi kidogo
Wakili huyu wa serikali naomba kwa kiasi nikuume sikio juu ya wakili huyu.
Ndugu huyu alizaliwa katika Kijiji cha Kiwele Kitongoji kinachofahamika kama
Mapinduzi Wilaya ya Iringa Vijijini, mkoa wa Iringa kama nilivyofika huko mwaka
2006 nikikusanya taarifa za ndugu huyu.
Ukifika Iringa Mjini ukiwa unaelekea Chuo Kikuu cha Mkwawa kuna njia inaelekea
bondeni hiyo njia ndiyo inakwenda huko Mapinduzi-Kiwele na nadhani kisiasa lile
ni jimbo Kalenga na siyo Jimbo la Isimani.

Kijiji hiki nilibaini ni cha watu masikini sana huku wakilima kunde, mahindi,
tumbaku na hata Mpunga kwa bondeni. Kwa wakati huo walikuwa na shule ya msingi
ambayo ndiyo aliyosoma wakili huyu na shule moja mpya ya sekondari, pia wakiwa
na zahanati.
Kijiji hiki kikaliwa na
Wahehe na Wabena wengi.
Umbali kutoka shule ya
msingi, sekondari na zahanati ilikuwa kama dakika 20 za mguu kutoka kwenye makazi
ya baba wa Wakili Mwidunda.
Ndugu huyu kwa utafiti wangu nilibaini kuwa kidato cha nne na cha sita alifanya vizuri sana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alisoma sheria pia alifanywa vizuri sana, hata Chuo Kikuu cha Malta-Italia ambapo alifanya shahada ya uzamili katika sheria za bahari pia hakukiuka mwiko wake, alifanya vizuri mno.
.
Mahakama ina sifa moja kubwa ya kuhifadhi kumbukumbu ya mashauri makubwa
makubwa, miongoni mwa kesi kubwa ambazo ndugu huyu aliiwakilisha serikali
vizuri mahakamani ni ile ya rufaa ya mke wa Marehemu Imrani Kombe, ambapo mama
huyo aliomba alipwe kiasi fulani cha fedha ambacho kilikuwa kikubwa mno, upande
wa serikali uliomba alipwe nadhani milioni 200 kama fidia baada ya mauwaji ya
mumewe ili aweze kutunza familia naye mama huyu akiomba milioni 500.
Nadhani ombi hilo la serikali lilikubaliwa na mahakama, wanasheria kama mnasoma
matini hii mtanisaidia pale nilipokwenda kombo.
Kwa hiyo rufaa yangu iliandaliwa na wabobezi wa sheria kweli kweli hata ndugu Peter
Pinda ni hatari sana kwenye sheria, japokuwa yeye huwa na desturi ya kama
kuigiza kuwa yeye si mbonezi (huwa ni mtu wa kujishusha).
Unaweza kusema kesi hii ya Tambaza ilikuwa ni ndogo, mbona Mwanakwetu alitumia
nguvu kubwa kuielezea?
Mwanakwetu tambua kuwa kesi
ni kesi tu maana maamuzi ya kesi ni mawili kushinda au kushindwa yana athari kubwa
katika maisha ya binadamu.
Phidelis Mwidunda kama asingalishiriki katika kutayarisha nyaraka hizi leo hii
nisingalimkumbuka kabisa.
Nitoe ushauri kwa rafiki zangu wanasheria wote msidharau kesi yoyote,
unayoletewa na mteja wako, ifanyie kazi kwa moyo wote na uwezo wako wote,
tambua dunia ina kesho, mambo ya kesho Mungu anajua.
Lakini pia kesi ndogo ya
mteja inaweza kukupa mteja mwenye kesi kubwa.
Angaweza kumwambia ndugu Peter kuwa achana nao, hao wanafunzi wa Tambaza ni
wahuni tu, wavuta bangi, lakini hawakufanya hivyo.
Kwa bahati mbaya Phidelis
Mwidunda leo hii macho yake, masikio na kiwiwili chake kimelala katika makaburi
ya huku kwao Mapinduzi-Kiwele mkoani Iringa, maana alifariki mwaka 2003,
natambua matini hii inaweza kusomwa na watoto wake, nduguze na Wanyaulukolo wa
Iringa Vijijini. Mungu awakabiriki sana.
Kwa leo naiweka chini kalamu yangu hapo.
Mungu ailazee roho ya marehemu Phidelis Mwidunda pahala pema peponi amina.
makwadeladius@gmail.com
0717649257

.gif)
Post a Comment