MGOGORO WA AZANIA NA TAMBAZA XXVII

 



Adeladius Makwega-DODOMA

Kikao cha bodi ya shule hii kilifanyika na kilihudhuriwa na wajumbe wote wa Bodi Isipokuwa Mzee Agrey Mwambene ambaye alikuwa mtumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi. Kwa hakika akidi ilitimia na kikao hicho kilifanyika. Haikufahamika sababu ya mjumbe Mwambene kutokushiriki kikao hicho.

Pengine majibu yake alikuwa nayo mwenyekiti wa bodi na katibu wake Mwalimu Mtera.

 

Kufahamu kuwa Mwambene hakushiriki kikao hicho, Mwanakwetu hakumuona kikaoni tangu mwanzo hadi mwisho. Swali la kujiuliza mjumbe huyu halali kwanini alikacha kikao hicho ? Swakli hili nitalijibu hapo mbeleni.

 

Bodi ya shule hi ikiwa chini ya mwenyekiti wake na katibu wake Mwalimu Mtera iliwasikilizia wanafunzi wote 15 mmoja baada ya mwingine kila mmoja akatoa maelezo yake juu ya kushiriki kwake au kutokushiriki katika fujo za shule hiyo ambazo zilidaiwa kuipa Tambaza sifa mbaya.

Kwa maelezo ya wajumbe wa bodi walisema bayana kuwa walimfuata mwanafunzi Fausta Jangwani na alitoa maelezo bayana juu ya tukio hilo na kuwataja wanafunzi wote 15.na kuwatambua wahusika kwa kutumia picha zao za mafaili zilizochukuliwa wakiwa kidato cha kwanza.

 

Kwa maelezo ya Fausta mwenyewe anasema bayana kuwa hakuonana na bodi hiyo ya shule na wala hawakufika Jangwani sekondari baada ya tukio hilo kama Fausta alivyozungumza Mwanakwetu Aprili 19, 2022.(miaka 30 baada tukio hilo kutokea)

Maelezo ya Said Masoudi ambaye alikuwa kijana wa mchanganyiko wa Mwarabu na Mhindi yeye alidai kuwa ndani ya Kikao cha bodi ya Tambaza mapema ya Novemba 1993 alisema bayana kuwa hausiki fujo za siku hiyo alikuwa nyuma darasani akijisomea.

 

Ndugu huyu ambaye sasa dakitari wa binadamu huko Marekani alisema kuwa alimuona binti Mrembo Fausta kupitia dirishani akiongozana na Atanas Luis.



Maelezo marefu sana aliyatoa Edga Wiliam Chibura ambao kwa hakika alikuwa na ufahamu wa tukio hilo na alikuwa mkubwa kwa umri zaidi ya wanafunzi wote wa 3R1 ambapo baadaye alikuwa ni Afisa wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT huku akiwa kaka wa hekima darasani akipenda sana kucheza mchezo wa soka japokuwa hakuweza kuucheza vizuri mchezo huo, Edgar William  Chibura alikuwa anapiga fwogo mara nyingi.

 

Pia naye Atanas Luis kwa usalama wake na ili kupona kufukuzwa shule ilikuwa ni kutoa ushirikiano kwa bodi hiyo na hakika majina mengi yalitajwa kwa wale wote walithubutu kumgusa Fausta lakini sasa mbona nayeye anaigizwa katika sekeseke hilo?

Atanasi Luis kada maarufu wa Chama cha Mapinduzi hizi sasa alitoa maelezo yenye ushirikiano mno kikaoni.

 

Maelezo ya Alone Sifuni ambaye alifariki mwaka 1994 yeye alisema bayana kuwa hata siku tukio hilo linatokea  hakuwepo shuleni, bodi ilitaka kujua alikuwa wapi wakati yeye kama mwanafunzi alipaswa kuwepo shuleni? Ilikuwa ni kujitetea lakini ndiyo alikuwa anajiingiza katika mdomo wa mamba , Arone alikuwa nje ya darasa na kwa ukweli wa Mungu Arone Sifuni AKA  KATISI hakuwepo darasani.


Maelezo ya Mohamed Said AKA MZUKIZI ambaye nayeye alifarki miaka hiyo ya kati 1994-1995 alisema bayana kuwa yeye anasoma 3M1 na hasomi 3R1 kwa hiyo kumuiginza katika matukio ya R1 ni kumuonea bure. Lakini pia japokuwa hakusoma R1 ilidaiwa kuwa alionekana katika korido jirani na tukio hilo wakati Fausta anafika Tambaza. Ndugu huyu ambaye alikuwa hasikii vizuri na huku akisema kwa kigugumizi alimaliza utetezi wake katika bodi hii.

Kwa upande wake Mwanamkwetu(Adeladius Francis Makwega) alisema bayana kuwa siku ya tukio hilo alikuwa darasani akichora miale ya mwanga katika mada ya somo la Fizikia inayofahamika kama Mwanga. Mara alisikia kelele na kuamka katika dawati lake na kutoka mlangoni aliona msichana aliyevalia sare za Jangwani akishuka ngazi akilia, huku akiongozwa na wanafunzi wengine.

Mwanakwetu alirudi darasani kuendelea na kazi yake ya kuchora michoro hiyo ya mwanga.

Mbele ya bodi hiii mjumbe mmojawapo aliuza swali kwa Mwanakwetu ehe mbona matokeo yako yanapanda na kushuka mno ? Mara 9 mara 15 mara wa tatu? Swali hilo halikupata majibu kutoka kwa Makwega kijana kutoka Mbagala.

 

Mwenyekiti wabodi ya shule hii alimuuliza Mwanakwetu swali juu ya mwanafunzi mmoja wa Zanaki Sekondari aliyekuwa akisoma tuition anayefahamika kama Kemikembe Mulokozi ambaye alikuwa akifika sana Tambaza sekondari kusoma, vipi Mwanakwetu anafahamu ?

 

Mwanakwetu alijibu kumfahamu vizuri  Kemilembi Mlulokozi kwa kuwa kaka yake aliyekuwa akifahamika kama Muchunguzi Mulokozi Kamugusha alikuwa akisoma pamoja naye.

 

Mjumbe mwingine wa bodi alimuuliza Mwanakwetu ehe mbona mnamuone gere mwalimu kumfundisha Kemikembe Mulokozi? Mnataka nyinyi msomeshe Kemikembe Mulokozi?

(Wajumbe wengine wa bodi wakicheka)

Mwanakwetu alijibu kuwa hapana, Kemikembi ni sawa dada yetu maana kaka yake tunasoma naye. Hatumuonei gere mwalimu

Mwenyekiti wa bodi aliuliza na kusema kuwa Mwanakwetu unaonekana unampenda sana Kemikembi Mulokozi unaonaje tukuamishie shule ya mchanganyiko ukasome na wasichana (swali hilo halikujibiwa). Mwanakwetu alikaa kimya.

Mwenyekiti wa bodi alimalizia kwa swali lengine kwa Mwanakwetu, inaonekana wewe unafahamika sana hapa shuleni, unaonaje tukupe kazi ya kila wenzako wanapokwenda kufanya fujo wewe uwe unashiriki lakini uwe unakuja kutupatia majina ya wote wanaoshiriki kwa siri?

Mwanakwetu alikaa kimya kwa muda, alafu akajibu kuwa siwezi kufanya kazi hiyo.

Mwenyekiti wa bodi aliuliza kwanini? Mwanakwetu alijibu kuwa sikuja kufanya kazi hiyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya sekondari Tambaza aliuliza Unamfahamu Fausta …? Mwanakwetu alijibu kuwa simfahamu, Mwneyekiti wa bodi alisema mbona yeye anasema kuwa unamfahamu vizuri sana na alipokuja wewe ulimfanyia fujo?

Mwanakwetu alijibu siyo kweli.

Mwanakwetu alitolewa nje ya chumba cha kikao na baada ya dakika kama tano aliitwa tena akaulizwa swali lile lile la kuwa aawe anawataja wale watakaoshiriki fujo za Tambaza huku yeye akiwa anashiriki.

Mwanakwetu alijibu kwa mara ya pili kuwa nimetoka nyumbani kuja kusoma, sikuja kufanya kazi hiyo.

 

Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Tambaza alimruhusu Mwanakwetu kurudi darsani kusubiri maamuzi ya bodi.

Kweli Mwanakwetu alirudi darasani.

Je bodi itafanya maamuzi gani?

Subiri matini ijayo.

Kumbuka haya ni makala ya Mgogoro wa Azania na Tambaza XXVII.

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com
0717649257

 

 

0/Post a Comment/Comments