MGOGORO WA AZANIA NA TAMBAZA XX

 

 





Adeladius Makwega-Arusha

 

Katika matini iliyotangulia nililitazama kapu langu la maswali na maoni kwa hakika sikuweza kuyamaliza maswali na maoni yote leo ninaendelea kuyaleta kwako msomaji wangu kidogo kidogo.

 Katika matini hii naomba kwa hisani yako msomaji walau nianze na zawadi yangu ya pili kwa wale waliofunga Ramadhani kwa ubeti wa huu wa shairi maalumu la Ramadhani.

 

Jitolee kwa futari, Peleka Msikitini , Apate kula fakiri, Pamoja na Masikini, Au katoka safari, mlishe huyo mgeni, Ramadhani imefika, Mola Tusamehe Dhambi.

 

 

Kumbuka makala haya wakati yanatoka kwa mara ya kwanza ilikuwa ni mfungo wa Ramadhani kwa wale Waisilamu.

 

Katika matini nambar XVIII (18) nilimtaja Dkt wa Binadamu Edmund Eliezer Ndalama, mara baada ya matini hiyo kutoka nilipokea ujumbe kutoka kwa ndugu Philemon Ferix akiniambia kuwa Dkt .Ndalama ni dakitari bingwa wa mifupa hapo MOI wako viranja wawili wanaojihusisha na Sign Nail mmojawapo ni yeye (Dkt Ndalama).

 

Hawa ni vijana wa zamani wa Tambaza madaktari bingwa hapo Muhimbili. Kwa hiyo msomaji wangu vijana wa Tambaza walikuwa wakipenda kusoma sana na ndiyo maana hawa madakatari bingwa wanatajwa leo hii na haya majina unakutana nayo katika matini hizi ni majina ya mabingwa wa kila fani ninazokutajia waliosoma shule hii kongwe.

 

Antony Kombo nayeye alikuwa mwanafunzi wa Tambaza mwenye kipaji cha kufanya vizuri kitaaluma kama alivyokuwa Abdil Rashidi. Wakati huo shule ya Tambaza ilikuwa chini ya Mkuu wa Shule aliyefahamika kama mwalimu Kalumuna.

 

Kwa kuwa ndugu Kombo alikuwa akifanya vizuri tangu kidato cha kwanza pale Tambaza siku ya mahafali yake Mkuu wa Wilaya ya Ilala wakati hio ndugu David Mlangwa alimpongeza ndugu huyu na kumkabidhi zawadi ya taaluma.

 

Picha ya tukio hilo ilitoka katika gazeti la Daily News wakati huo ni Daily News ilikuwa kweli kweli DAILY NEWS na picha hii inaambatana na makala haya.

 

Antony Kombo, alikuwa anaishi Block 41 jirani na Dawasa nyuma ya UWT hostel ambayo ilikuja kuwa Gogo Hotel baadaye na sasa ni pale ilipo Airtel. Kwa sasa naambiwa ndugu Antony Kombo yupo Marekani anaendesha maisha yake huko Ughaibuni.

 

 

Tambaza ilikuwa na vinara wengine kitaaluma kama vile Benedict Ndomba ambaye sasa ni Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao Tanzania, habari zake nyingi akiwa mwanafunzi wa Tambaza nitakusimulia katika matini zijazo.

 

Je kipi kitaendelea subiri matini ijayo.

Kumbuka hii ni sehemu ya XX ya Mgogoro wa Azania na Tambaza

 

Nakutakia siku njema.

makwadeladius@gmail.com
0717649257 



 

 

0/Post a Comment/Comments