Wafanyakazi Wavutiwa na Dua la Sheikh wa Mkoa wa Mara

 





Adeladius Makwega-BUNDA/MUSOMA

Ni majira ya asubuhi ya Mei Mosi , 2026 Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi anafika katika maadhimsho ya Sikukuu ya Wafanyakazi kimkoa katika Viwanja vya Muembeni Wilayani Bunda.

Eneo hili lilikuwa na manyunyu huku hayakuweza kuikwamisha shughuli hii ya umma, wananchi wa Bunda na viunga vyake wakichoma nyama nayeye Kanali Mtambi akiwaambia wafanyakazi kuwa Serikali mpaka sasa imelipa marimbikizo yao kwa karibu Shilingi Bilioni 3 yakiwamo yale ya mshahara na yale madeni mengine.

“Isitoshe wafanyakazi karibu 1708 wamepandisha madaraja yao. Nawaomba kwa sasa mchape kazi .”

Sherehe hii ilipambwa na uwepo wa Katibu Tawala Mkoa wa Mara Ndugu Gerald Musabila Kusaya na wakuu kadhaa wa taasisi za umma na binafsi. Wafanyakazi waliingia katika viwanja hivi huku wakiwa na mabango, zana za kazi na katika hali ya kuipamba sherehe hii TANESCO Tanzania walikuwa na gari moja kubwa huku wakionesha namna milingoti ya umeme inavyopachikwa nyaya za umeme na kuunganishwa.

 

Kama ilivyo mila na desturi ya sherehe za wafanyakazi kuimba wimbo wao wa Mshikamano Daima kulifanyika hivyo lakini wimbo huu uliimbwa kwa kiitikio peke yake.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Mara akiwa amevalia suti nyeusi alikagua mabanda kadhaa yaliyozunguka pembe za kiwanja hiki ambapo kila banda lilikuwa na kile walichokielezea huku Chuo Kikuu cha Kilimo na Tekinolojia kilicho Butiama kilieleza kuwa kina kinatoa kozi kadhaa tangu stashahada na shahada na kikiwa na kampasi mbili ile ya Osward Nang’ombe na Kampasi Kuu.

Mambo kadhaa yaliwavutia wengi mojawapo ni wakati Sheikh wa Mkoa wa Mara Ustadh Musabaawakati akiombea ufunguzi wa sherehe hii aliweka ndani ya dua yake maombi ya kumuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Samia Suluhu Hassan na akimsihi mhe Rais aongeze mishahara ya wafanyakazi, hapa nao wafanyakazi wakisema amina kwa sauti ya juu na dua hili likishangiliwa mno.

 

Shughuli hii ilihitimishwa majira ya saa 11 jioni kwa burudani zilizotanguliwa kwa kutoa zawadi kwa wafanyakazi hodari.

Wakati haya yakiendelea hali ya hewa ya Mji wa Bunda ni nyuzi 21, unyevunyevu ni wa asilimia 20, ujirani na mvua ni wa asilimia 87 huku mvua kubwa ilinyesha na upepo ukivuma kwa KM 2 kwa saa.

Mwanakwetu Upo?Kumbuka?

“Wafanyakazi Wavutiwa na Dua la Sheikh wa Mkoa wa Mara.”

Nakutakia Siku Njema

 

makwadeladius@gmail.com

0717649257

 

 

0/Post a Comment/Comments