Sikilizeni enyi watu,
Nawaletea hoja nzito,
Kuhusu siri ilivyo,
Ya mtu au ya jamii yote.
Baada ya uhuru wetu,
Serikali ikazaliwa,
Ya watu wote kwa dhati,
Si ya mmoja kujimilikia.
Makabila yalitengana,
Kila moja na mipaka,
Lakini umoja ukaja,
Ukafuta ile tofauti.
Watawala wa zamani,
Walitumia siri nyingi,
Siri yao wakajisitiri,
Wananchi hawakujua.
SIRI, SECRET, na SIR-I,
GEHEIMNIS kwa Wajerumani,
Yote yalikuwa ya watawala,
Si ya watu wa kawaida.
Lakini leo tumehuru,
Serikali ni yetu sote,
Kwa nini basi siri ibaki,
Kwa wachache tu milele?
Zipo siri za taifa,
Zilindwazo kwa manufaa,
Kama ramani za vita,
Zikivuja ni hatari.
Na pia mitihani yetu,
Ikivuja hupotosha,
Wasiofaa hupita,
Taifa hupata hasara.
Hizi ni siri za umma,
Kila mmoja alinde,
Maana madhara yake,
Hugusa jamii nzima.
Lakini ipo hadithi,
Ya waziri mwenye tabia,
Aendaye kwa siri usiku,
Bila kujulikana wazi.
Dereva wake mwaminifu,
Hukaa nje akimngojea,
Asijue kinachoendelea,
Ndani ya chumba cha VIP.
Kumbe nyuma ya pazia,
Waziri hutoka kisiri,
Kupanda boda boda,
Kufuata mambo ya siri.
Baadaye yakafahamika,
Kwa macho ya dereva,
Akatambua ukweli,
Wa maisha ya kiongozi.
Je hii ni siri ipi?
Ya serikali au binafsi?
Jibu lake lafikiriwa,
Kwa mizani ya hekima.
Maana akipatwa ajali,
Taifa lote huumia,
Hasara si yake peke,
Bali ya jamii nzima.
Hapo ndipo swali huja,
Mipaka iko wapi?
Ya siri ya mtu binafsi,
Na ile ya umma wote.
Ni vyema kwanza kunena,
Kwa hekima na heshima,
Ili kuepusha madhara,
Bila kuaibisha mtu.
Lakini akikataa kusikia,
Na hatari ikaendelea,
Jamii nayo hujitokeza,
Kulinda maslahi ya wote.
Hitimisho nalisema,
Kwa sauti ya wazi,
Zipo siri za kulindwa,
Na zipo za kuwekwa wazi.
Tambua mipaka yake,
Kwa akili na busara,
Ili kulinda haki zote,
Za mtu na za taifa.
Mtunzi ni Adeladius Makwega wa Mbagala
0717649257


Post a Comment