.gif)
Adeladius Makwega-MBAGALA
Siku hii Mwanakwetu aliamka mapema mno, maana alikiwa na kazi iliyokuwa inaanza asubuhi hiyo hiyo. Mara alipofika katika eneo lenye kazi alikutana na watu wanafunga mabango na huku vijana wawili wanafunga muziki wao.
Hapa akatua begi lake mgongoni na kuwasalimu hawa vijana kando na kuomba kupatichika ekstensheni yake ili aweze kufanya kazi zake za kihabari kwa kudoea umeme.
Vijana hawa walikuwa waungwana sana, gafla huyu kijana akapokea simu kabla ya kuipachika ektesheni ya Mwanakwetu huku akimpa maelekezo mtu mwingine kwa maneno haya:
“Wewe nenda kachukue hiyo mikorofoni kisha uje nayo hapa, sawa?…mimi namalizia kufunga vifaa, sawa …”
Asubuhi hii masikio ya Mwanakwetu kwanza yaikaribishwa na milio ya nyundo kwa wale wanaopachika mabango na maturubai na huku kando yanasikika mawimbi ya Ziwa Victoria.Jamaa akaongea na simu kisha akawa anaendelea na kaiz yake vizuri.
Mara huyu kijana akapiga simu kwa mtu mwingine huku akiyasema maneno haya:
“Hii kompyuta naona inatetemeka mno, sasa sijuhi nichezee simu? Kama ipo Kompyuta nyingine uje nayo…”
Hapa palikuwa kimya huku milio ya mawimbi ya Ziwa Victoria na nyundo ikiendelea.
Mara ukachezwa wimbo wa Michael Jackson ule wa I wanna Start Something ambapo ni miongoni mwa nyimbo kadhaa za Michael Jackson kutoka album ya thriller .
Wakati wimbo huu unaendelea, huyu jamaa akachukua ektesheni ya Mwanakwetu na kuipachika katika umeme na kisha kuendelea na majukumu yake. Hapa nayeye
Mwanakwetu anausikiliza muziki huo vizuri sana na maana anaukumbuka tangu akiwa mdogo, mawazo ya Mwanakwetu yakarudi mbali hadi mwaka 1984/1985 Mbagala Jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.
“Nyumbani kwetu kulikuwa na msiba wa bibi wa Baba anayefahamika kama Binti Mkongeni ambaye alikuwa ni mama wa Bibi mzaa baba Mwanakwetu anaitwa Hedwiki Omari Binti Mkomangi. Msiba ukafanyika vizuri na kisha kuzika, msiba ulipohitimishwa, Mimi, mdongo wangu Modestus na Michael, Mkomangi Mkundi, , Nasilika Nyema na watoto wadog wengi tuliambatana na Shangazi Biligita Makwega tukawa tumetumwa Mbagala Bugudadi jirani na Mbagala Misheni kando na nyumbani kwa mama Mwingizi kwa sasa, huku kulikuwa na nyumba aliyokuwa amepanga mtu mmoja anaitwa Julius Gopali ambaye alikuwa anamiliki Gopali Enterprises(Mbagala Sabasaba) tulikuwa tunakwenda kurudisha ndoo na vifaa vingine vingi vilivyotumika msibani. Tukiwa njiani tukakutana na watoto wadogo rika zetu mapacha (kurwa na doto) wakatuchokoza kwa kuchukua mchanga na kutumwagia huku wakiunguruma kama njiwa, kruuuuuuu kruuuuuu, kruuuuuu, kruuuuu….Jambo hili likanikera sana nikawafuata wale watoto ili nipambane nao, nyuma shangazi yangu Biligita Makwega akaja kuongeza nguvu, wale vijana mapacha wakakimbia. Hawa vijana walikuwa wakiunguruma kama njiwa kwa kuwa mimi nilikuwa nimevaa suruali na jinzi ambayo ilikuwa haikugusa viatu surua za njiwa(don’t touch) na ndiyo maana walinitania hivyo na mimi sikukubalia nilipambana nao.”
Kipindi hiki ndipo zile surualia za don’t touch zilikuwa maarufu mno na nyimbo kama huu I wanna startin’ sometin’ na Olie na Jerry wa there no Stopping Us zilikuwa maarufu mno redioni, katika kumbi za muziki katika sikuu majumbani hata katika filamu.
Kumbuka Mwanakwetu yupo katika kazi hii maalumu na shughuli ile haya haya ya nyimb hizo alikuwa anazikumbuka tu. Sasa hapa alipo kazi ikaanza vizuri na baadaya ya dakika 10 wakubwa wakaingia ziwani maana kulikuwa na tukio katikati ya Ziwa Victoria.
Hapa waliobaki pale pale jamaa mmoja siyo yule DJs akapokea simu huku pakiwa na utulivu na yakawa yanasikika maneno haya:
“Nimekwambia hakuna kwenda JKT, wewe si umesikia waziri kasema kazi ya askari kuuwa ni kawaida sasa unataka kwenda huku ukaue watu? Kama unataka kwenda huko usitumie jina langu na ukatuletea jina baya. Nimesema hakuna kwenda na mama yako nimeshamwambia…hata kama ni kazi utafanya kazi zingine, kwani lazima ufanye kazi huko?”
Jamaa huyu alikata simu hapa hapa Mwanakwetu akamuuliza huyu ndugu mbona unagombana katika simu? Jamaa akasema anakijana wake amemaliza kidato cha sita anatakiwa kwenda JKT kwa mujibu wa sheria nay eye amekataa akihofia hali mbaya ya sasa kumekosekana maelewana ndani ya jamii kwanini nimuigize mwanangu kwene matatizo asiyoyajua chanzo?
“Hao hao walioanzisha ugomvi wapambane na ugomvi wao wasiniingizie mwanangu, staki kabisa…”
Mwanakwetu akamuuliza huyu jamaa kwani Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa amesema nini? Jamaa huyu akajibu siyo Waziri wa Ulinzi bali Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Tanzania anaitwa Mahmodu Thabiti Kombo. Jamaa huyu akatoa simu yake janja na kisha kuicheza video hii.
“Kila mmoja anatekeleza majukumu yake, kila mmoja anakwenda kazini, jamani ya nini chokochoko, kwa nini mnarejesha choko choko jamani ! Tumeshalitibu taifa, tumeshaliponya taifa, hadi kwenye taasisi za dini, tumeshaponya. Wewe jaribu hapa ukitoka nje ukitoka nje ukimrembea(kumtishia) jiwe polisi, fanya hivyo uone! fanya hivyo uone! General Oder yao inaruhusu, General Oder inamwambia attack first, hakuna wa kumlaumu, mwenyezi amelijalia taifa letu zuri na kutujalia taifa letu zuri la Tanzania, jamani Katiba imeshafanya kazi yake na sisi tutawahusisha wengine mahusiano mema , tutawahusisha kwa Diplomasia…”
Baada ya Mwanakwetu kuutazama video hii gafla viongozi walirudi kutoka ziwani na shughuli hii kuendelea huku shughuli hii ilikuwa imehudhuriwa na vijana wengi kutoka vyombo vya ulinzi na usalama.
Wakati shughuli hii inaendelea umbali wa mita kama 10 alikuwepo askari wa kike ambaye alikuwa hapo tangu mapema, kisha huyu binti askari akaja binti mwingine na wa awali akaondoka zake, huku yule wa awali na huyu aliyekuja mara pili rika lilikuwa moja wakiwa vijana wenye nguvu.
Baadaye shughuli hii iliisha na kisha Mwanakwetu kwenda katika kazi ya pili ya siku hii huku masikioni mwake alipachika kiongeza sauti akiusikilzia wimbo wa Olie na Jerry wa there no Stopping Us miongoni mwa nyimbo za miaka ya 1980 na baada ya siku kadhaa mbele yake akaamua kuyatayarisha makala haya.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Tanzania amenukuliwa akiyasema maneno haya…
“…wewe jaribu hapa ukitoka nje ukitoka nje ukimrembea(kumtishia) jiwe polisi, fanya hivyo uone! fanya hivyo uone! General Oder yao inaruhusu, General Oder inamwambia attack first, hakuna wa kumlaumu,..”
Mwanakwetu anaamini maneno haya hayakuwa sahihi kuzungumzwa na Waziri Kombo kwanza yeye hausika na Wizara ya Mambo ya Ndani na wala siyo Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Angalia haya maneno yanawakatisha tamaa wazazi na kukataa kuwaruhusu watoto wao katika mambo ya msingi. je tunaweza kwenda namna gani katika hali kama hii? Sisi kama taifa? Maneno kama haya yanawapa mazingira magumu polisi wetu ambao kwa hakika hawana ugomvi bali ugomvi upo kwa wanaota maagizo kwa polisi. Haiwezekana polisi atishiwe kurushiwa jiwe na raia kama hakuna maagizo mabaya ? Mtoa maagizo lazima awe makini , awe na utu na kujalia usalama wa Polisi na Raia na kama yupo mtu kama Mahamoud Thabiti Kombo hii ni shida na ndiyo chanzo cha matatizo yte yasiyokwisha.
Mwanakwetu Upo? Kumbuka
“Shida ni Mtoa Maagizo.”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257









.gif)
.gif)
.gif)
Post a Comment