Mwanakwetu Nimesimama, Nafikiri kwa Makini
Mbungi na Mganda Pia, Zanivutia Moyoni
Kila Moja Ina Sifa, Zenye Mvuto wa Ndani
Najiuliza kwa haraka, Nichague Ipi Mapema?
Mbungi Ngoma ya Shangwe, Midundo Yake ya Nguvu
Huwavutia Wengi Sana, Kwa Suati na Miendo
Ni ya Furaha na Vigelegele, Hupamba Sherehe Nyingi
Huenda Nikichagua Hii, Nitawafurahisha Wengi
Mganda Nayo Tulivu, Lakini ina Maana
Hufundisha Mila Njema, Na Historia ya Kwetu
Si ya Makelele Sana, Bali Hubeba Busara
Huifanya Jamii Yote, Ijuvunie Asili
Moyoni Nafanya Shauri, Nichague Ipi Kwa Haki
Furaha ya Mbungi Kubwa, Lakini Yapaa Haraka
Mganda Ina Uzito, Wa Mila na Heshima
Naona Njia Iliyo Bora, Si Ya Pupa Wala Tamaa.
Basi Jibu Nimepata, Bila Kusita Wala Woga
Mganda Ndio Chaguo, Kwa Faida na Kudumu
Nitaianza Mapema, Kwa Bidii na Maarifa
Mwanakwetu Nashukuru, Nimeamua Kwa Hekima
Utenzi huu umetungwa na Adeladius Makwega wa Mbagala Mei 10, 2026.
0717649257
.gif)


.gif)
Post a Comment