.gif)
Adeladius Makwega-MBAGALA
Mapema ya mwezi Mei, 2026 Tanzania imempokea Rais wa Kenya mhe. William Samoe Ruto na katika heka heka za ugeni huu nchini Tanzania, Mwanakwetu hakujaliwa kusikiliza hotuba zote juu ya ziara hii hapa Tanzania.
Huku Mei 6, 2026 Mwanakwetu alimsikiliza Nabii Dkt. Tito Lemo ambapo yeye aliyazungumzia mambo kadhaa hasa juu ya ziara hii.
Kwa kuwa Mwanakwetu ni mfuatiliaji mkubwa wa mitandao ya kijamii na kila kinachoeleza na Nabii huyu kutoka Kenya anakisikiliza Mwanakwetu alikumbuka kuwa kuna wakati Nabii Dkt. Tito Lemo, ndugu aliwaambia waamini wake kuwa:
“Nyumba isiyo na ndama tambueni nyumba hiyo haina ng’ombe.”
Hii ikiwa dhana ya mazingira ya ufugaji ambapo ndama akinyeshwa maziwa vizuri, akilindwa vizuri, mwisho wa siku anakuwa ng’ombe bora.
Kwa uhakika hili unaweza kuliona hata katika mazingira ya wafugaji wakubwa barani Afrika, wenye ng;ombe wengi huwa wanakuwa makini na ndama wao n ahata huwa kuna mtu maalumu anayefanya kazi ya uchungaji wa ndama tu maana ndama ni ng’ombe wajao.
Msomaji wangu kikubwa hata Nabii Dkt Tito Lemo alikuwa anasisitiza umuhimu wa kuwathamini vijana katika jamii zetu maana kama hakuna vijana taifa halipo, wazee wako jirani kuondoka.
Nabii za Dkt Tito Lemo ni nyingi na nabii mojawapo aliyowahi kusema ni hii:
“Hali ya Tanzania itakapokuwa ni tete kwa yale niliyoyatabiri natawauma sikio na kuwa punde yakiwa karibu kutokea nitakuwa nimevaa suti nyeupe…”
Hii ikiwa ishara ya kiongozi huyu wa kiroho nchini Kenya.
Mwanakwetu hana hakika kama mambo haya yametokea au bado na kama yametoa ndiyo basi tena lakini kama bado leo hii Mwanakwetu anamwambia nabii kuwa anamfuatilia mno hatua kwa hatua na hata pale anapotoa unabii juu ya Uganda , Kenya na hata mataifa mengine moyoni mwake huwa na simanzi na kuchukia mno akisema kwanini nabii hasemi kitu juu ya Tanzania? Nabii Mwanakwetu anauliza:
“Kama haya mambo bado na haujavaa suti ile nyeupe, je Nabii lini utavaa suti yako nyeupe? Vipi ile Suti yako nyeupe utavaa na viatu vyeupe? Je suti yako hii itakuwa mpya au ya zamani? Kama ni ya zamani umeshaipelekea kufuliwa kwa dobi au anafua mama nabii?”
Mwanakwetu kwa makala haya anamuomba Nabii Dkt.Tito lemo haya :
“Siku ikijongea anza kuvaa kimoja kimoja kwanza vaa soksi nyeupe na viatu vyeupe, kisha siku inayofuata unavaaa suruali nyeupe soksi nyeupe na viatu vyeupe, siku nyengine unaongeza na shati jeupe, siku inayofuata unavaa na tai nyeupe na kisha siku ya mwisho unamalizia na koti jeupe na usisahau kupachika na beji ya bendera ya Tanzania.”
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo? Mwanakwetu ametayarisha makala haya kwanza kwa kuvutiwa na kisa kile cha ndama katika zizi na pia makala haya ni ya salaam kwa Nabii Dkt. Tito Lemo huko nchini Kenya.
“Salaam hizi zikufikie wewe Nabii, familia yako na waamini wako wote.”
Mwanakwetu ametoa ushauri huo kwa Nabii kama ukiwa unafaa basi nabii anaweza kuutumia, kikubwa ni kujua kusoma majira na alama za nyakati kwa wale Mungu aliyowajalia.
Mwanakwetu upo? Kumbuka:
“Nabii Anza Kuvaa Kimoja kimoja.”
Nakutakia Siku Njema.
0727649257







.gif)

Post a Comment