Adeladius Makwega-MBAGALA
Mei 15, 2026 Mwanakwetu alitembelea Idara ya Afya ya Ofisi ya Mkoa wa Mara ili kujua kinachoendelea katika idara hii ya umma inayoshughulika na siha za Wananchi wa Mkoa wa Mara, hapa alipokelewa na wafanyakazi wa idara hii wakiwamo wahudumu, wauguzi, makatibu wa Afya, wafamasia na matabibu kadhaa wakiwa chini ya usimamizi wa Dkt Zablon Elias Masatu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara.
“Karibu sana Mwanakwetu, hapa sisi kama Idara ya Afya ndiyo tumetoka kukamilisha zoezi la Mop Up ya Chanjo ya Ugonjwa wa Polio awamu ya pili ambayo tulihimitisha Mei 11, 2026. Kwa hakika zoezi hili tumelifanya vizuri huku tumefikia malengo yetu na kwa hakika tunawashukuru wananchi wa Mkoa wa Mara kwa namna walivyojitokeza, pia shukurani ziende kwa wahisani wote walivyowezesha zoezi hili tangu Red Cross Tanzania , WHO , UNICEF na hata Wizara yetu ya Afya.”
Akizungumza ofisini kwake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt. Masatu aliongeza na haya:
“Unajua ili kufanikisha zoezi la njanjo kwanza lazima uwe na mahitaji yote ya kufanikisha zoezi kama vile chanjo yenyewe, vifaa vya kubebea chanjo, watumishi, magari na uwezo wa kuifikia jamii pale ilipo na kisha ni je muitikio wa wananchi unakuwaje? Kwa hakika wananchi wamejitokeza vizuri kuwaleta watoto wote waliolengwa katika hili ili tunatoa pongezi kubwa wa wananchi wa mkoa wa Mara kufanikisha zoezi na viongozi wao ngazi zote.”
Dkt. Masatu aliongeza kuwa ugonjwa wa polio ulishatokomezwa karibu mikaa 20 iliyopita ndipo mara ya mwisho vimelea vyake vilionekana lakini hivi karibuni kulifanyika utafiti ikaonekana kuwa Kanda ya Ziwa kulioneka vimelea vya Polio katika maji taka ili likasababisha kufanyika zoezi ili kufanyika kwa watoto wa chini ya miaka 9 na miezi kumi na moja kupatiwa chanjo hii.
Akizungumizia hali ya takwimu zilivyokuwa Bi Grace Mgongorwa ambaye ni ni Mratibu wa Takwimu za Utoaji wa Chanjo ya Polio Awamu ya Pili alisema kuwa siku ya Mop Up walichanja watoto 6,417 huku wakivuka lengo lao la mkoa ambapo kuchanjwa watoto 1,05,429 na kuwafikia watoto 1,048,727 ikiwa ni asilimia 100.31.
Akizichambua taarifa hizo Bi Mgongora alisema:
“Mei 10 , 2026 walichanja watoto 106,722, Mei 9, 2026 walichanja watoto 203,201 , Mei 8, 2026 walichanja watoto 283,629 na Mei 7, 2026 walichanja watoto 448,758.”
Dkt. Masatu akizichambua takwimu hizo alisema kuwa kati ya watoto wote 1,048,727 asilimia 51 ni wasichana na huku asilimia 49 ni wavulana.
Baada ya Mwanakwetu kuyakusanya yote haya ndipo alipoamua kuyatayarisha makala haya.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Ugonjwa Polio ni ugonjwa hatari unaoshambulia mfumo wa neva na kusabbaisha kupooza kwa misuli hasa kwa watoto chini ya mikaa mitano. Chanjo ya polio kwa sehemu kubwa imesaidia mno kupamb ana na ugonjwa huu hatari tangu mwaka 1950 huku sasa vimesalia virusi vya Polio vya mwitu (WPV1) ambapo vipo nchini Afghanistan na Pakistan.
Mwanakwetu Upo ? Kumbuka:
“Muitiko wa Wananchi ni Muhimu Wakati wa Kutoa Chanjo.”
Nakutakia siku Njema.
0717649257
.gif)
.gif)








Post a Comment