BBT Uvuvi Kurwa na BBT Mifugo Doto

 



Adeladius Makwega-LakeSide Musoma.

Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evansi Alfred Mtambi Mei 28, 2026 amewataka vijana wanaopokea mikopo mbalimbali kukumbuka kurejesha mikopo hiyo wanayopokea ili kutoa nafasi kwa wengine kuweza kunufaika na mikopo hii.

Haya yamezungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mara wakati akizindua mradi wa vijana karibu 40 ambapo unaosimamiwa na BBT Uvuvi chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizngumza katika hotuba yake Mkuu wa Mkoa wa Mara pia ameiomba Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuukukmbuka mkoa wa Mara katika mradi wa BBT Mifugo.

“Natambua hii ni miradi pacha, Hii ni miradi Kurwa na Doto Mkoa wetu una mifugo bora sana huku nyuma ya mkoa wa Mara ni bora sana, mkoa wa Mara ni rafiki kwa mifugo maana mifugo mkoa wa Mara ipo nyumbani kwao.Hapa ndipo nyumbani kwa wanyama wote tangu enzi lazima tuwe na nyama bora. Kama mmemleta Kurwa (BBT-Uvuvi) basi mumlete na Doto wake(BBT-MIfugo).”

Akizungumzia usalama wa vizimba na ufugaji wa samaki Kanali Mtambi aliagiza Wilaya ya Musoma kuhakikisha kunakuwa na usalama na kupambana vilivyo na wavuvi haramu na huku akiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mara kuongeza ulinzi ndani ya Ziwa Victoria.

 

Awali wakati Kanali  Mtambi akipiga bisimilai ya hotuba yake alitoa kizimba kimoja cha samaki ambacho tayari kipo ziwani kwa vijana wa hamasa kutoka Mkoa wa Mara ,na baadaye Vijana hao walipewa  vizimba vingine vine vya samaki ziwani  ambapo walilala masikini na kuamka matajiri.

Kwa upande wake Afisa Biashara wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo TADB Bi Glacial Maruguja alisema kuwa benki yao inatoa mikopo katika mradi huu ambapo imetoa mikopo kwa vizimba 99 na huku ikiwanufaisha wanawake na vijana karibu ya 500 huku akiomba mikopo irejeshwe kwa wakati.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, mwakilishi wa wizara hii ndugu Samweli Mdachi alisema kuwa ameagizwa na wizara yao kuleta kazi, tabasamu la utu, huku akishukuru kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara kuutendea haki mradi wa BBT –Uvuvi.

 

Ndugu Mdachi aliongeza na haya:

 

“Programu ya BBT-Uvuvi ni mojawapo ya programu kubwa mbili za wizara yetu, huku tukiwa pia na programu ya BBT Mifugo, shabaha yetu ni kuongeza fursa ya kipato, ajira na chakula wa jamii ya Watanzania.”

Akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Mara Mkuu wa Wilaya ya Musoma mhe. Juma Chikoka alisema kuwa Ziwa Victoria limekuwa chanzo kikubwa cha matajiri wote wa mkoa wa Mara, hivyo Wilaya ya Musoma inalipa heshima kubwa Ziwa Victoria,

“Hili halikuanza leo, ni la muda mrefu, ninashukuru sana Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kuja na programu ya BBT Uvuvi kwa vijana. Nawaomba kwanza ifahamike kuwa wale wanaovua kwa ndoano ni Watanzania wenzetu na ni haki yao, huu uvuvi wa ndoani ni uvuvi asilia lazima tuwaheshimu lakini na wao wavue umbali wa mita mia kutoka kilipo kizimba, kila mvuvi wa samaki awe salama na hili litasaidia kila mmoja kunufaika na uchumi wa bluu kwa Ziwa Victoria.”

 

Awali Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Mtambi alipata maelezo ya mradi wa BBT Uvuvi kwa vijana Mkoa wa Mara, kisha alikwenda kukagua mradi huo katika vizimba kadhaa ndani ya Ziwa Victoria, ambapo alipata fursa ya kupiga kipenga cha mradi huo kwa kuwarushia chakula samaki ndani ya vizimba vyao.

Mwanakwetu akiwa katika ziara hiyo alishuhudia samaki hao ndani ya vizimba na wale walio nje vizimba wakimsogelea kwa karibu Kanali Mtambi, huku wakimpigia saluti ya ukaribisho wakati akirusha chakula hicho katikati ya Ziwa Victoria.

Akishuhudia tukio hili la kuwapa samaki hao chakula katika ya Ziwa Victori huku ziwa likiwa limechafuka, kukiwa na mawimbi makala Mtakwimu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara Issa Rajabu Mbombwe alisema,

“Kumbe Mwanakwetu hiki chakula kinachotolewa kwa samani ndani ya vizimba kinawanufaisha hata samaki wengine ambao hawapo ndani ya vizimba, kumbe ufugaji wa kisasa una manufaa kwa ziwa nzima.”

Akizungumza kwa njia ya simu Mbunge wa Musoma Mjini Mhe. Mgore Miraji Kigera alisema kuwa yeye kama mbunge wa jimbo hili anashukuru sana kwa wananchi wake kupata mikopo ya BBT-Uvuvi, huku akiongeza kuwa:

 

“Programu ya BBT-Uvuvi ni vifupisho vikimaanisha Building a Better Tomorrow na ni mradi wa Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi wenye lengo la kuwajengea uwezo vijana na wanawake ili kujihusisha na uchumi wa bluu, ufugaji wa samaki ni uvuvi wa kisasa na una shabaha ya Uwezeshaji Kifedha ambapo unatoa mitaji na ruzuku za serikali ili kuwawezesha vijana kuanzisha miradi ya uvuvi, Ufugaji wa Samaki (Aquaculture): unahimiza matumizi ya teknolojia za kisasa kama vizimba (cages) na mabwawa, kuboresha uzalishaji na shabaha ya mwisho ni Fursa za Kanda ya Ziwa hii ni fursa muhimu kwani inajumuisha miradi inayofadhiliwa na serikali na washirika kadhaa.”

Msomaji wangu haya yote ni katika hafla hii ya uzinduzi wa mradi wa BBT Uvuvi mkoani Mara ambapo ni mradi Kurwa na wakati haya yakiendelea hapa Musoma hali ya hewani nyuzi joto 21, unyevunyevu ni wa asilimia sufuri , ujirani na mvua ni wa asilimia 62 na upepo ukivuma kwa KM 14 kwa saa.

Mwanakwetu upo?Kumbuka

“BBT Uvuvi Kurwa na BBT Mifugo Doto.”

Nakutakia siku Njema

makwadeladius@gmail.com

0717649257

 





















 

 

0/Post a Comment/Comments