Adeladius Makwega-MBAGALA
Mapema ya Mei 14, 2026 Mwanakwetu alitembelea Idara ya Elimu Mkoa wa Mara kutaka kujua hali ya Kielimu Mkoa huu ikoje ?
Hapa alipokelewa na maafisa kadhaa wa ofisi hii ya umma iliyopo kando ya Ziwa Victoria, huku mkoa huu ukiongozwa na Kanali Evans Alfred Mtambi na Katibu Tawala wake ni ndugu Gerald Musabila Kusaya.
Akizungumzia hali ya Elimu kwa Mkoa huu Afisa Elimu Mkoa Dkt. Elpidius Baganda alisema kuwa hali ya taaluma kwa sasa ipo vizuri huku watahiniwa wa mitihani kadhaa ya kitaifa wakiendelea kufanya mitihani hiyo katika maeneo mbalimbali.
Dkt. Baganda aliongeza kuwa:
“Tangu Mei 4 hadi 22, 2026 ni ratiba za mitihani hiyo ikiwamo ya kidato cha sita na ile ya vyuo vya ualimu, Mkoa wetu una shule 33 zenye kidato cha sita na wanaoketi kufanya mitihani ni wanafunzi 4767 ndani ya mikondo 152 na vyuo vya ualimu vitatu vikiwa na mikondo 22 watahiniwa 723.”
Akizichambua takwimu hizo Afisa Taaluma Mkoa wa Mara ndugu Ayubu Mbilinyi amesema kuwa takwimu za wanafunzi wanaojiunga na kidato cha tano na kuhitimu kidato cha sita kwa mkoa wa Mara zimekuwa zikiongeza kila mwaka:
“Mwaka wa 2023 tulikuwa na watahiniwa 3076, 2024 -3035 na mwaka wa 2025-3317.”
Ndugu Mbilinyi alisema kuwa kwa hakika shule za kidato cha tano na sita za umma nchini Tanzania zinapokea wanafunzi kutoka nchi nzima bila kujali mkoa anapotoka mwanafunzi husika lakini :
“Kwa mkoa wa Mara asilimia 70 ya wanaosoma kidato cha tano na sita kwa shule za umma ni wanafunzi kutoka kanda ya ziwa na asilimia 30 ni kutoka mikoa mingine ya Tanzania.”
Mara baada ya Mwanakwetu kufahamu haya ndiyo alipoamua kuyaandika makala haya.
Wakati haya yakifanyika katika ofisi hii ya Mkoa wa Mara, hali ya kutoa huduma katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara iliendelea vizuri wananchi waliendela kupata huduma huku watumishi wa taasisi hii walikutwa wakichapa kazi. Kwa upande wa hali ya hewa ya mji wa Musoma ni nyuzi joto 27, unyevunyevu ni wa asilimia 30, ujirani na mvua ni wa asilimia 63 na upepo ukivuma kwa KM 6 kwa saa.
Mwanakwetu upo? Kumbuka:
“Asilimia 70 Kidato cha Sita Mkoa wa Mara Wanatoka Kanda ya ziwa.”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257
.gif)










.gif)
Post a Comment