Wageni wa Katibu Tawala Mkoa wa Mara wanajua Kusoma na Kuandika

 



Adeladius Makwega-Musoma MARA.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara Aprili 15, 2026 imeendelea kutoa huduma kwa wananchi wa eneo hili lililopo Kaskazini Mashariki mwa Tanzania ambalo lipo jirani na Ziwa Victoria, huku likikadiliwa kuwa na watu zaidi ya milioni mbili wanaojishughulisha na biashara, kilimo, uvuvi, uchimbaji madini na ufugaji.

Mwanakwetu ameshuhudia wananchi kadhaa wakiingia katika ofisi hii ya umma iliyopo kando ya Mlima Mukendo ambapo mwaka mzima mlima huu hupambwa na kijani ya Chanikiwiti.

 

Hadi saa 5.00 ya Aprili 15, wananchi kadhaa waliingia kupata huduma na miongoni mwao ni Said Hassan ambaye alijitambulisha kuwa anatokea Kinondoni Dar es Salaam ambapo aliingia kumuona Katibu Tawala Mkoa wa Mara saa 2. 49 ya asubuhi ,alimuona Katibu Tawala Mkoa wa Mara Ndugu Gerald Musabila Kusaya na kuhudumiwa vizuri kisha kuondoka zake.

Wanawake na wao hawakubaki nyuma kuitembelea taasisi hii ya umma ambapo Bi Maryciana Sonda kutoka Musoma Vijijini alifika na kumuona Katibu Tawala Mkoa Mara, Bi Sonda alipatiwa huduma na kisha kuondoka zake.

Wageni hao wote waliomuona Katibu Tawala Mkoa wa Mara ndugu Kusaya huku awali walipokelewa vizuri na Richard Magoiga ambaye Msaidizi wa Ofisi Mwandamizi na Bi Misambo Gambuna ambaye ni Mwendeshaji Ofisi Mwandamizi katika Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Mara. 

 

Wakati makala haya yanatayarisha tayari kurasa mbili za kitabu cha wageni katika geti kuu la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara zilikuwa zimejazwa majina ya wageni hao kwa miandiko yao na hii ikitoa ishara kuwa wageni wote walioingia katika taasisi hii siku hii wanajua kusoma na kuandika.

Wakati haya yakiendelea hali ya hewa ya mji wa Musoma ni nyuzi joto 26, unyenyevu ni wa asilimia 10, ujirani na mvua ni wa asilimia 56 na upepo ukivuma kwa KM 13 kwa saa.

Mwanakwetu upo?Kumbuka:

“Wageni wa Katibu Tawala Mkoa wa Mara Wanajua Kusoma na Kuandika.”

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257

 









 

0/Post a Comment/Comments