
Adeladius Makwega-MBAGALA.
“Machi 25, 2026 aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI, Reuben Kwagilwa, alitoa maelekezo ya kumvua majukumu Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu yake. Hii ni kufuatia kutoonekana kwa nyaraka muhimu za Ujenzi wa Jengo la Idara ya Afya, ambalo lilijengwa takribani miaka 12 iliyopita, huku ujenzi huo ukiwa haujakamilika. ”
Aprili 8, 2026 mamlaka ya uteuzi ya Mawaziri nchini Tanzania ilimuhamishia ndugu Kagwila Wizara ya Muungano na Mazingira. Jambo hili lilimshangaza mno Mwanakwetu, akijiuliza hivi mamlaka ya uteuzi ilikuwa inatambua mchango wa ndugu Kagwila hapo TAMISEMI?Au unapokuwa kiongozi nchini Tanzania wewe pokea mshahara na mengine yaache yaende kama yalivyo? Je tunajua matumizi sahihi ya rasilimala watu tulizo nazo?
“Unaweza kuwa na jembe, panga, fyekeo, leki na shoka hizo zote ni zana za kilimo ili kuweza kufanikisha shughuli ya kilimo lazima mkulima mwenyewe ajue kutumia zana sahihi, pahala sahihi wakati sahihi na siyo vinginevyo.”
Kama Halmashauri ya jiji la Mwanza haina nyaraka zake za miaka 12 yaani mwaka wa 2014 ni jambo la kuchekesha na haya ni matusi wa wananchi wa Mwanza maana historia inadokeza kuwa eno hili lilianzishwa rasmi mwaka 1892 kama kituo cha biashara, miaka 134 iliyopita, Mwanza ilikuwa Manisipaa mwaka wa 1978 miaka 48 iliyopita na kuwa jiji mwaka wa 2000 miaka 26 iliyopita , sasa kupotea kwa hati ya mwaka wa 2014 ni hatari maana yake lolote linaweza kutokea katika ofisi hii ya umma maana jukumu mojawapo la taasisi kutunza nyaraka za umma.
Kwa hiyo ndugu Reuben Kagwila akiwa kiongozi TAMISEMI ameonesha umahiri hapa lazima tungemuacha huyu ndugu afanye kazi hapo au kumpandisha ngazi hapo hapo TAMISEMI. Unapomuhamishia Mazingira na Muungano ni kuinyima jamii ya Watanzania kufikiwa na kutatuliwa kero zao.Hili linaibua maswali mengi ambayo hayana majibu ikiwamo kushindwa kutambua kuwa zana hii ya kilimo inatumika pahala ambalo si sahihi.
Kwa hakika kosa hili hilo ndilo lililofanywa na mamlaka yetu ya uteuzi kwa Dkt. Seleiman Serera kumtoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na kumpeleka wizara nyingine huku madhalimu wanashangilia.
Dkt Serera ni mwanasheria angeweza kuokoa jahazi na huku baadaye Mkataba wa Uwanja wa Arusha unasainiwa kwa gharama mara mbili kutoka Bilioni 187 hadi kuwa Bilioni 338.54.
Matumizi sahihi ya rasilimali watu ni jambo muhimu wanaofanya maamuzi wasidhani kuwa wao wanaona zaidi kuliko jamii, watambue kuwa jamii inawafahamu vijana wao na hata hao wanaofanya maamuzi mnafahamika vizuri sana, hivyo umakini ni muhimu na maslahi ya wengi ni lazima.
Makosa haya ndiyo mara nyingi wizara zetu zinafanya, viongozi wa Wizara wanatazama maslahi binafsi wakidhani wizara hizo zipo kwa ajili yao leo hii, zipo kwa ajili ya Waziri na Katibu Mkuu tu. Watambue kuwa Wizara hizo zilikuwepo tangu enzi na kama maslahi yako ni miaka mitano au kumi tu vipi maslahi ya milele ya Watanzania ziadi ya milioni 72?
Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo ilifanya kosa moja baya miaka minee nyuma kwa rasimali watu kwa kuwaondoa kwa kuwapa uhamisho ndugu kadhaa kwanza Mkurugenzi wa Miundo Mbinu ndugu Alex Mkenyenge(Msabato). Huyu jamaa alihamishiwa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kuwa Mkufunzi kisha Idara ya Miundombinu kukabidhiwa mtu mwingine ambaye hakuwa na uzoefu baadaye idara hii ikarejeshwe tena kwa ndugu Alex Mkenyenge. Swali ni moja tu ilikuwaje ulimuondoa mtumsihi A na kumlipa gharama za uhamsho za serikali kisha unamrudisha tena katika nafasi hiyo. Jamii ikihoji je ulifanya hizo ili kututoa katika Bilioni 187 na kisha kutupeleka kuwa Bilioni 338.54 itakuwa siyo sahihi?
Tuseme wewe ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu unatoka kwenu unafanya uhamisho utakavyo tu kwa gharama za Watanzania? Haiko hivyo maana pesa za uhamisho haulipi wewe, hailipi familia yako bali Watanzania wanalipa kutokana na kodi zao, hapo uhamisho huo lazima uwe na tija kwa manufaa ya jamii ya Watanzania siyo vinginevyo, hata ukiitwa leo hii utoe ushahidi wa manufaa ya uhamisho huo unaweza kujibu?
Jina la pili ni la aliyekuwa Mkurugenzi wa Mipango ndugu Haji Janabi (hamsa salawati) huyu ndugu alipewa barua na kutoka hapo kwa cheo cha chini, kunaweza kutolewa majibu? Hoja ni ile ile kuitoa Wizara hiyo kutoka Bilioni 187 hadi Bilioni 338.54.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Msomaji wangu kumbuka jambo moja tu pale unapomuadhibu paka shume lazima umuoneshe njia ya kutoka. Sasa ndugu zangu katika hili lazima mtambue jamii ya Watanzania kwa sasa ipo makini mno, inawafahamu mno vijana na ndugu zao wanaonesha uhodari, wapo wanaona na kukaa kimya, wapo wanaona na kuhifadhi kumbukumbu na wapo wanaona na kuandika hawa ni akina Mwanakwetu na ndiyo maana leo ametajwa Alex Mkenyenge, ametajwa Ndugu Haji Janabi na hata mheshimwa Reuben Kagwila kwa uhodari wao hakuna mwenye ugomvi na mtu bali mambo ya umma yafanywe vizuri. Kufanyika vizuri kwa mambo ya umma hiyo ndiyo njia pekee ya kupenya kwa paka shume.
Kwa hakika Mwanakwetu bado anaendelea kumpongeza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali nchni Tanzania Dkt Charles Kicher kwa kazi nzuri katika ripoti yake yam waka wa fedha 2024/ 2025.
Mwanakwetu upo?Kumbuka:
“Unapomuadhibu Paka Shume Muonesha Pa Kutokea.”
Nakutakia siku njema
0717649257


.png)
.png)
.gif)
.gif)
.png)
.png)
Post a Comment