Tuwe Makini Tunapotangaza Hali ya Hatari

 

 

Adeladius Makwega-MBAGALA

 

Kulingana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na marekebisho yake Ibara ya 32 inampa Rais mamlaka ya kutangaza hali ya hatari nchi nzima au sehemu yoyote iwapo kuna vita, hatari ya kuvamiwa, au kuvurugika kwa amani na usalama. Tamko hili lazima liwasilishwe bungeni ndani ya siku 14 na linaweza kusitisha baadhi ya haki za kimsingi. 

 

 

Mambo Muhimu kuhusu Hali ya Hatari ni haya:

Ibara ya 32 inafafanua kuwa Rais anaweza kutangaza hali ya hatari ikiwa kuna tishio la vita, kuvamiwa, au kuvurugika kwa amani na usalama wa jamii huku Ibara ya 31 inaruhusu ukiukaji wa baadhi ya haki na uhuru wakati wa hali ya hatari, isipokuwa haki ya kuishi.

Rais anatakiwa kuwasilisha tamko hilo kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ataitisha kikao ndani ya siku 14 kulijadili. Bunge linaweza kuongeza muda wa tamko la hali ya hatari kwa vipindi vya miezi 6. Narudia haya maneno(Bunge linaweza kuongeza muda wa tamko la hali ya hatari kwa vipindi vya miezi 6.)

Hali hii inatumika kuhakikisha usalama wa nchi na kuokoa maisha au mali wakati wa majanga makubwa au matishio dhidi ya Jamhuri ya Muungano Tanzania.”

 

Swali la msingi ni moja tu je haki hizo za binadamu za msingi ni zipi?

Haki za binadamu za msingi nchini Tanzania zimeainishwa katika Sura ya Kwanza, Sehemu ya Tatu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na marekebisho yake (ibara ya 12 hadi 29), ikijumuisha haki ya kuishi, usawa mbele ya sheria, utu, faragha, uhuru wa kujieleza, kusafiri, na kumiliki mali.

 

 

Haki Kuu za Msingi Kulingana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni tangu Ibara 12 hadi 29 kama nilivyodekeza awali:

“Haki ya Kuishi (Ibara 14): Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata hifadhi ya maisha yake kutoka kwa jamii. Usawa mbele ya Sheria (Ibara 13): Watu wote ni sawa mbele ya sheria na wanastahili ulinzi sawa bila ubaguzi wowote. Haki ya Utu na Heshima (Ibara 12): Watu wote huzaliwa huru na ni sawa, na utu wao unapaswa kuheshimiwa. Haki ya Uhuru wa Mtu Binafsi (Ibara 16): Haki ya faragha ya maisha yake, familia, nyumba, na mawasiliano. Uhuru wa Kujieleza na Habari (Ibara 18): Haki ya kutoa maoni, kutafuta, kupokea, na kutoa habari. Uhuru wa Imani na Dini (Ibara 19): Kila mtu anao uhuru wa kuamini, kuabudu, na kueneza dini yake. Haki ya Kumiliki Mali (Ibara 24): Haki ya kumiliki mali halali na kupata fidia ikiwa itatwaliwa na serikali. Haki ya Kufanya Kazi (Ibara 22): Kila raia anayo haki ya kufanya kazi na kupata ujira sawa.Uhuru wa Kujumuika (Ibara 20): Haki ya kushirikiana na wengine, ikiwa ni pamoja na vyama vya siasa.”

Haki hizi hauwezi kuzipoka utakavyo bali unamjulisha Spika kusudio lako, spika anaitisha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kikao halali kinafanyika, wabunge wanajadili ikikubaliwa ndipo unatangaza hali ya hatari.Hoja ni moja kama jambo linatokea gafla inakuwaje? Hoja ni zile zile Tanzania ina vyombo vya uchunguzi wa mwenendo wa taifa , hatari yoyote lazima ijulikane na ndipo hali ya hatari inatangazwa kwa utaratibu uliyowekwa.

 

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Nakuomba msomaji wangu tutazame mambo matatu hauwezi kutangaza hali ya hatari kama bunge halijajulishwa na kujadili hoja hii.

“Rais anatakiwa kuwasilisha tamko hilo kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye ataitisha kikao ndani ya siku 14 kulijadili.”

Nakuomba msomaji wangu utambue kuwa hali ya hatari ikitangazwa haki kadhaa zinapokwa hapa hauwezi kufanya mikutano ya siasa, hauwezi kuzunguka mitaani kufanya mikutano, mijadala matangazo ya kisiasa.

 

Tatu na mwisho katika hili la Haki ya Uhuru wa Mtu Binafsi (Ibara 16): Haki ya faragha ya maisha yake, familia, nyumba, na mawasiliano.

“Pale tu unapotangaza hali ya hatari wapo askari na wanajeshi wanakuwa tayari kupambana na adui huyu aliyesababisha hali ya utulivu kutoweka . Hawa askari/wanajeshi wanabaki makambini kungoja amri ya kuagizwa cha kufanya kupambana na adui. Hawa askari/wanajeshi wakiwa makambini maana yake mambo ya nyumbani iwe ndoa zao, ndugu zao hata kama kumetokea msiba familia husika inajua kuwa mume wake, mke wake yupo kambini kutokana na kutangazwa hali ya hatari.

Mke hawezi kumlalamikia mumewe mwanajeshi yupo katika nyumba ndogo kama anajua hali ya hatari imetangazwa. Mathalani Mwanajeshi Z0000H ana wake wanne hawezi kuhisi mumewe kaongeza siku kwa mke mkubwa au mke mdogo kwa sababu anaifahamu kazi ya mumewe na hali ya hatari imetangazwa.”

Sasa changamoto ni moja kama utaratibu wa kutangaza hali ya hatari unapokiukwa na vyombo vya ulinzi vikatekeleza kwa kutumia hoja hali ya hatari vinaweza kuwajibishwa na si vyombo vya ulinzi na usalama tu hata mtoa hoja batili anawajibishwa kwa sababu amekiuka Katiba:

“Hapa lazima Rais Hoja yake aipeleke Bungeni , Spika aitishe Bunge, hoja ijadiliwe, wananchi wajulishwe maana Bunge linaweza kutoa ushairi wa kina namna ya kutekeleza hiyo hali ya hatari n ahata kuiongozea muda.”

Watanzania wengi hawafahamu kuwa hata Rais anashitakiwa vizuri sana kwa kukiuka Katiba mathalani ulitangaza hali ya hatari bila kufuata utaratibu ambapo ulikiuka Katiba uliyokula kiapo kuilinda na isitoshe maamuzi yako haya yalisababisha madhara kadhaa ikiwamo upotevu wa mali,vilema na vifo vya raia na askari.

 

Kwa hiyo katika hali kama hii kama Mahakama za Ndani zinakuwa dhaifu hapo ndipo mahakama za Kimatiafa zinaingilia kati mathalani ICC.

Mwanakwetu upo?Kumbuka:

“Tuwe Makini Tunapotangaza Hali ya Hatari.”

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257

 



















 

0/Post a Comment/Comments