Adeladius Makwega-MBAGALA
Jumapili moja Mwanakwetu alisali Kanisa Katoliki la Malya ambapo siku hii ilikuwa na uchangamfu mno , watu wengi kila kona mlio ya pikipiki na baiskeli siku nzima watu wakienda katika gulio kununua na kuuza kidhaa mbalimbali.
“Eneo la Malya lililopo Wilayani Kwimba Mkoani Mwanza ni maarufu sana kwa kilimo na ufugaji, huku likipitiwa na reli ya mwendokasi na reli ile ya mkoloni huku milio ya treni mara nyingi ikisisikika.”
Mwanakwetu anatoka kusali dominika hii mandarin mbele yake waamini wawili wanawake wanaongea:
“Huyu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ametusaidia kutujengea Kituo cha Polisi, kwa hapa Malya uhalifu siyo mwingi na kituo cha awali polisi cha awali kilitosha, yeye angesaidia kujenga hata zahanati nyingine ili tuweze kutibiwa au angeboresha hata kituo cha Afya cha Kata ya Malya…”
Msomaji wangu eneo hili wakati huo lilikuwa nyumbani kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan Dkt.Eliezer Feleshi ambaye alikalia nafasi hii tangu mwaka 2021 hadi 2024 na wakati huo Rais Samia alikuwa anamalizia kipindi kile cha Rais Magufuli mara baada ya kufariki.
Kumbuka Mwanakwetu anatoka zake kanisa na mbele yake akina mama wawili wanaongea:
“Wasomi mawazo yao yote ni ulinzi na usalama ndiyo maana amekumbuka kujenga kituo cha polisi lakini uwepo wa kituo cha polisi ni usalama wa uwekezaji wake hapa kijiji…”
Hivi ulishawahi kusikia Kanisa Katoliki linajenga kituo cha polisi? Kanisa mar azote linajenga Hospitali, shule na taasisi zinazogusa ustawi wa binadamu. Hawa akina mama wanaongea mama mmoja aliyekuwa kimya akawa anasema hata usalama ni jambo la msingi lakini kikubwa hapa kituo cha polisi kipo cha awali na kilitosha sana au kama maboreshi kingefanyiwa ukarabati tu na hapo palipojengwa kituo kipya ingekuwa hata zahanati hili nakubaliana nalo. Mara hawa kina mama wakawa wanasalimiana na watu kando na eneo hili nayeye Mwanakwetu kuwapita kuelekea huku alipokuwa anakwenda.
Kwani Mwanakwetu amelikumbuka tukio hili?
Hivi karibuni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Charles Kichere amesema :
“Mradi wa ujenzi wa Uwanja wa michezo wa Arusha uliokadiliwa kujengwa kwa shilingi bilioni 187 mktaba wake ulisainiwa kwa shilingi za Kitanzania Bilioni 338.54 likiwa ongezeko la asilimia 81.”
Mara baada ya taarifa hiyo kusomwa hadharani majibu ya Katibu Mkuu wa Wizara iliyojengewa hoja hii na CAG alisema kwamba gharama hizo zimekuwa kubwa kukidhi vigezo vya CAF. Hapa hoja ilivyojengwa na majibu yaliyotolewa hadharani yamempa mashaka Mwanakwetu kisha na kuwa na tafakari kubwa huku akilikumbuka tukio la akina mama hawa na ujenzi wa kituo cha Polisi kipya kijijini mwao.
“Kwa kawaida ili CAG awe na hoja inawezekana hoja hii ikajengwa na Mkaguzi wa Ndani wa Wizara husika na ikajibiwa na pengine hakuridhishwa na majibu, kisha CAG akaja akaikuta hoja akapewa majibu hakuridhika na majibu hayo au inawezekana CAG mwenyewe hoja hii aliibaini akaomba majibu akapewa na hakuridhika nayo na ndiyo maana hoja hii ikabaki hadi katika vitabu vya hoja na kusomwa hadharani.”
Haya ni mawazo ya Mwanakwetu.
Kwa hakika Hoja ya Ukaguzi inapotolewa haijibiwi kwa vyombo vya habari, bali unatoa majibu yako ukiwa na ushahidi wa nyaraka zote kama vile hivyo vigezo vya CAF mbele ya meza ya mkaguzi wa hesabu.
“Ilikuwaje awali gharama ilikuwa chini na sasa inakuwa karibu mara mbili?”
Hapa ya msingi kama ingejibiwa vizuri Dkt. Charles Kichere kwa hakika lazima angeelewa tu na kwa bahati nzuri Dkt. Kicheere ni miongoni mwa vijana wa zamani waliokuwa wanafunzi bora kitaaluma pale Tambaza Sekondari wakati anahitimu kidato cha nne. Katika hili wale vijana wa zamani waliosoma Tambaza Mkoani Dar es Salaam mnakumbuka. Hoja ya gharama kupanda kwa kiwanja cha Arusha inalingana na wale akina mama Wakatoliki wa Malya kuwa hapa kituo polisi kipo iweje huyu mtoto wetu amezaliwa hapa, kwanini asitujengee hospitali? Yeye anatujengea kituo cha polisi? Hizi ni hoja za watu na kama unazisikia unazijibu. Hoja hizi ni haki kwa watu kusema hata kama pesa unatoa wewe au anatoa mtu mwingine au pesa za umma. Hoja ni kwanini gharama ipande karibu mara mbili?
Hisia ni nyingi,
“Labda kiwanja cha Arusha kinajengwa huku kuna eneo lingine la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinajengwa kiwanja kama hicho kwa gharama za kiwanja cha Arusha kwa hiyo zile bilioni za awali zinajenga Arusha na zingine zinazoongezeka zinajengwa huko.”
Kwa mtazamo mwingine jamii inatambua wazi kuwa Wizara ya Habari , Utamaduni Sanaa na Michezo hii ni Wizara ya iliyokuwa Tanganyika haipo katika mambo yale ya Muungano: Hapa kuna mawazo mengi mojawapo ni hili:
“Unajua kabla jambo kufanyika kunakuwa na hatua za awali, watu wanaona ramani hivyo hisia inakuja inawezeka yupo mtu mwenye dhamana alivutia na ramani akasema ngoja mjenge na kule kwa ramani hiyo hiyo nyinyi angalieni cha kufanya.”
Haya ni mawazo ya kihisia tu kwa kulitazama jambo hili kwa picha nyingine.
Jambo la mwisho ambalo ni Mwanakwetu analiona na muhimu kuzingatia ni hili Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo ambayo sasa ni Wizara ya Habari , utamaduni, Sanaa na Michezo imewahi kuongozwa na mawaziri kadhaa akiwamo Mheshimwa Mohammed Mchengerwa tangu Januari 10, 2022 hadi Februari 14, 2023 maana yake alikaa na wizara hii kwa miezi 13, kisha kwenda Wizara ya Maliasili na Utali. Katika kipindi hiki wizara husika ilikuwa na miradi yoyote ya kimkakati Kama ujenzi wa Kiwanja cha Arusha? Je hali ilikuwaje? Katika hili msomaji wangu tilia maanani pawepo na ujenzi au ukarabati hali ilikuwaje?
Kama ilifanyika hiyo miradi ilikamilika kwa wakati? Gharama zilikuwaje? Wale waliokuwa wanahudumu kando au jirani na miradi hii hali ilikuwaje? Maana hawa waliokuwa kand na miradi hii ni sawa na wale wanawake kando ya Ujenzi wa Kituo cha Polisi Malya.
Kwa leo msomaji wangu inatosha sana.
Mwanakwetu anasema hata kama hizo pesa anatoa nani lakini ni heri tungeenda kujenga Hospitali za kisasa ili Watanzania watibiwe bure kulikuwa kuwa na miradi ambayo gharama zake zinapanda maradufu.
Mwanakwetu Upo?Kumbuka:
“Angetujengea Zahanati ya Kisasa na Tungetibiwa Bure.”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257






Post a Comment