Njia Yake Haitatupeleka Katika Dhambi

Adeladius Makwega-MBAGALA

“Leo tuko katika Jumapili ya nne ya Pasaka. Katika Injili ya dominika hii Yesu anajitambulisha kama mchungaji wa kondoo na lango la kondoo. Kama mchungaji, anawaita kondoo wake kwa majina yao na kuwaongoza.

Kondoo wake wanamfuata kwa sababu wanajua na kutambua sauti yake. Kama lango, yeye ndiye njia ya wokovu na malisho ili kondoo wapate uzima, na waongezeke.

Yesu anatuhadharisha kuhusu wezi na wanyang’anyi wanaojifanya wachungaji, tuwe nao makini.

Ikiwa njia inayowasilishwa kwetu haileti wokovu, tusimame kidogo na kuchunguza mioyo yetu ili kusikia sauti ya mchungaji mwema. Njia yake haitatupeleka katika dhambi na maangamizi. Tumtafute yeye kama anavyotutafuta.”

Haya ni mahubiri ya Kadinali Luis Antonie Tagle Mkuu wa Propaganda Fide ya Kanisa Katoli Ulimwenguni juu ya Dominika ya nne baada ya Pasaka ya Aprili 26, 2026.

 

Katika hili kuna wakati Papa Fransisko akiwa hai alihimiza sana mapadre kuwa ‘wachungaji wanaonuka harufu ya kondoo.’ taswira inayosisitiza kwamba wachungaji wanapaswa kuwa karibu na waamini wao, wakishiriki maisha yao, furaha zao, na mateso yao.

Kauli hii ilitajwa kwa mara ya kwanza mwaka 2013, na inahimiza huduma ya vitendo na ya kujihusisha moja kwa moja, ikiwasukuma viongozi wa dini kutoka katika mazingira ya starehe na yaliyofungwa ili kwenda kuhudumia watu walioko husani pembezoni mwa jamii ambako wanaishi na kuteseka.

Mwanakwetu katika hili anaona kuwa siyo wachungaji tu hata siye wazazi, walezi na viongozi hakika wajibu wa kila mmoja katika jamii ni kunuka harufu ya walio chini yake haiwezekani kiongozi anukie manukato jamii inuke harufu ya kondoo.

Mwanakwetu Upo?Kumbuka:

“Njia Yake Haitatupeleka Katika Dhambi na Maangamizi.”

Nakutakia Jumapili Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257













 

0/Post a Comment/Comments