
Adeladius Makwega-MBAGALA.
“Hivi unajua kwanini Rais wa Jamhuri ya Muungano akitoka Tanganyika na Makamu wa Rais anatoka Zanzibar na Rais akitoka Zanzibar makamu wa Rais anatoka Tanganyika? Je Kwanini kipengele hiki kiliwekwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?”
Haya ni maswali mawili ambayo majibu yake ni haya:
“Kulingana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 (kama ilivyorekebishwa), Ibara ya 47(3) inaweka wazi kuwa ikiwa mgombea urais (Rais) anatoka sehemu moja ya Muungano (Zanzibar), basi mgombea mwenza (Makamu wa Rais) lazima atoke sehemu ya pili ya Muungano (Tanganyika). Kulingana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na taratibu za uchaguzi zinataka mgombea urais na mgombea mwenza wasitoke upande mmoja. Kanuni hii inahakikisha usawa wa uwakilishi wa pande zote mbili za Muungano katika nafasi za juu za uongozi. Haya ni kwa mujibu wa mabadiliko yam waka 1992/1995: Kabla ya mabadiliko haya, Rais wa Zanzibar alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Muungano moja kwa moja lakini mfumo wa sasa unamtaka mgombea urais kuchagua mgombea mwenza kutoka upande tofauti na sio lazima awe Rais wa Zanzibar. Kwa kifupi, katiba inakataza Rais na Makamu wa Rais kutoka upande mmoja wa Muungano.”
Katika hili japokuwa Mgombea Urais na Mgombea Mwenza wanapigiwa kura katika kapu moja lakini wanapokula kiapo kila mmoja hula kiapo chake na kila mmoja ukalia kiti chake kwa majukumu yake.
Hata kama Mgombea Urais wa chama chochote kile anapomchangua mgombea mwenza, mara baada ya uchaguzi mkishashinda haimaanishi kuwa Makamu wa Rais awe mnyonge, Makamu wa Rais awe mtumwa wa Rais au Makamu wa Rais awe chawa wa Rais, bali Makamu wa Rais kwa mujibu wa sheria na Kanuni za Uchaguzi analo jukumu moja kubwa:
“Haya ni mabadiliko ya mwaka 1992/1995, Kanuni hii inahakikisha usawa wa uwakilishi wa pande zote mbili za Muungano katika nafasi za juu za uongozi.”
Sasa unapokuwa Rais au Makamu wa Rais lazima ujiulize je unauwakilisha vipi upande wa mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ule unapotoka wewe?
Kumbuka:
“Haya ni mabadiliko ya 1992/1995, Kanuni hii inahakikisha usawa na uwakilishi wa pande zote mbili za Muungano katika nafasi za juu za uongozi.”
Je unapokuwa mwakilishi wa upande mmoja wa Janhuri ya Muungano wa Tanzania katika nafasi hizo wewe unakwenda kukalia kiti na kufumbata mikono na kupokea mshahara tu?
Nakuomba msomaji wangu nikusimulie kisha hiki:
Mwaka wa 2022 iliyokuwa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ilimpokea Waziri mpya mhe. Mohammed Mchengerwa huku kiongozi huyu alifika hapo akiwa na timu ya wafanyakazi kadhaa akiwamo Mwandishi Mwendesha Ofisi na Msaidizi wa Waziri. Ujio huu uliwapa unyonge baadhi ya watumishi ambao walikuwa wanafanya kazi hizo katika ofisi hii ya umma na huku baadhi yao wakipangiwa majukumu mengine. Baadaye ilibainika kuwa huyu Mwandishi Mwendesha Ofisi aliyefika hapo alikuwa na udugu wa damu na Msaidizi wa Waziri kwa maana majina yao mawili ya mwisho yalikuwa yakifanana. wengine wakisema kaka na dada na wengine wakisema mama na mwana.
“Waziri Mchengerwa mbona amehamia na familia nzima hapa? Hili siyo haki.”
Watumishi wanaongea. Miongoni mwa watumishi walilobaini hilo ni Mwanakwetu na baadaye Mwanakwetu kuuliza kwa jamaa mmoja wa wale wanaoshughulika na rasilimali watu, jamaa alijibu kuwa wamelibaini hilo na linafanyiwa kazi.
Mwanakwetu akasema hili jambo ni baya linaleta mgawanyiko mkubwa kazini huku lazima kiongozi mwenyewe awe soni(aibu)na awe na uwezo wa kufanya kazi na mtu yoyote anayekutana naye na kama hilo haliwezekani na kiongozi hajajaliwa tabia hii basi lazima Utumishi wa Umma wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umlazimishe kiongozi huyo kuwa na tabia hiyo.
“Haya mambo yana madhara makubwa kwa jamii na yanaleta miganyiko mikubwa na chuki kwa serikali yao.”
Mwanakwetu alipobaini hili aliandika makala akishauri Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati huo mhe. Dkt. Philip Mpango akae ni mawaziri hawa angalau kuongea nao juu ya mambo kadhaa likiwamo na kujitahidi kufanya kazi na timu wanazokutana nazo katika wizara na taasisi hizo za umma tangu Madereva, Waandishi Waendesha Ofisi, Wasaidizi na Hata wahudmu wa Ofisi maana hawa ni watumishi wa Serikali na hizi tabia za mawaziri za kuhama na timu ni mbaya zinaweza kuwa na madhara katika maamuzi makubwa ya kitaifa.
Mwanakwetu hakuwa na hakika kama Mhe.Dkt.Philip Mpango alikaa na hao mawaziri au la.
Baadaye waziri husika alihama na timu hiyo kama ilivyo na kwenda nayo Wizara ya Maliasili na Utalii.
Jambo la kusikitisha baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2025 Mhe Mohammed Mchengerwa akawa Waziri wa Afya na huku Mkewe mhe.Wanu Amiri akateuliwa kuwa Waziri Mdogo wa Elimu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kibaya wakiwa ni ujamaa na rais wa wakati huu.
Maamuzi haya yalimkumbusha Mwanakwetu kisa kile cha mwaka wa 2022 pale wizarani kaka na dada/mama na mtoto kufanya kazi pamoja.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Kwa hakika tangu mwaka wa 2021 yapo matukio mengi yenye maswali ambayo hayana majibu. Mwanakwetu hana hakika kama Dkt. Philip Mpango kama aliwajibika ipasavyo katika nafasi hiyo ikiwamo hoja kadhaa hata ile ya kuuzwa kwa Bandari ya Dar es Salaam.
Kwa makala haya Mwanakwetu anamkumbusha nduguye Makamu wa Rais wa sasa Dkt. Emmanuel Nchimbi japokuwa wameingia madarakani katika hali inayolalamikiwa sana lakini anawajibu mkubwa wa kufanya kazi kwa bidii na kuyasimamia maslahi ya Tanganyika kufa na kupona maana baadhi ya viongozi hawana aibu lazima watu wa namna hii tuwaeleze ukweli wa maana sahihi ya utumishi wa umma na siyo sahihi kuyaacha mambo yaende kama yalivyo mathalani hili la Mke kuwa Naibu Waziri nayeye Mume kuwa Waziri wakati ni sehemu ya familia ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dkt. Nchimbi katika hili umelikalia kimya na lazima nikulamu na mzigo huo wa lawama ni wako, kuwa makini maana hili limefanyika wewe ni Makamu wa Rais, usije kuwa kama Dkt. Philip Mpango maana kama yeye angezungumza na mhe Mchengerwa n ahata mawaziri mengine juu ya hoja ile ya mwaka wa 2022 pengine haya ya mwaka wa 2025/2026 ya Wanu na Mchengerwa yasingalitokea. Kama Dkt. Nchimbi asipokuwa makini atazalisha akina Mchengerwa na Wanu wengi. Tukumbuke Tanzania ni nchi kubwa yenye watu zaidi ya milioni 72 tusizunguke katika koo zile zile, koo moja ikiwa na nafasi nyingi inakosa ubunifu na huku chuki kwa mkubwa wao zinahamishiwa kwa wale wadogo na utumishi wa umma unayumba.
Mwanakwetu upo?Kumbuka:
“Dkt. Nchimbi Asiwe kama Dkt. Mpango.”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257
.gif)




.gif)


Post a Comment