
Adeladius Makwega-MBAGALA.
Aprili 20, 2026 Mwanakwetu alitembelea ukarasa wa Katibu Mkuu Kiongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo kulikuwa na kurasa moja inaonesha Makatibu Wakuu Viongozi waliyopita. Hapa palikuwa na maelezo haya:
“Balozi Hussein A. Kattanga (2021-2023) Balozi Dkt. Bashiru A. Kakurwa (2021-2021), Balozi John W. Kijazi (2016-2021), Balozi Ombeni Y. Sifue (2012-2016), Philemon Luhanjo (2006-2011), Balozi Martin Lumbanga (1995-2006), Balozi Paul Rupia (1986-1995)Timoth Apiyo (1974-1986), Dickson Nkembo (1967-1974), Joseph Namata (1964-1967) na Dastan Omari (1962-1964).”
Baada ya Mwanakwetu kusoma haya maelezo pia akilini mwake alitaka kujua Watanzania waliyoiongoza Idara ya Usalama wa Taifa, hao ni kina nani tangu uhuru? Majibu yalikuwa haya:
“Seleiman Abubakari Mombo(Julai 11, 2024 mpaka sasa, Balozi Ali Idd Siwa (Agost 2023-Julai 11, 2024 ,Said Hussein Nassoro(Januari 2, 2023-Agost 2023), Afande Diwani Athumani Msuya (Septemba 12, 2019-Januari 3, 2023), Dkt. Modestus Kipilimba(2016-2019), Othman Rashid (2005-2016), Kanali Apson Mwang’onda(1995-2005), Luteni Jenerali Imran Kombe(1983-1995). Dkt Augustino Mahiga(1980-1983), Dkt Hassy Kitine (1978-1980), Dkt. Lawrence Gama(1975-1978) na Emilio Mzena(1961-1975).”
Kwa hakika msomaji wangu hayo ni mabango mawili ya Serikali moja ya Watanzania ju ya waliowahi kuwa Wakurugenzi wa Idara ya Usalama Taifa na bango la pili la Watanzania waliowahi Kuwa Makatibu Wakuu Viongozi wa hiyo hiyo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mwanakwetu siku ya leo anaitembeleza Idara ya Usalama wa Taifa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi tangu mwaka 1961, leo Mwanakwetu mtalii wa mabango, leo Mwanakwetu anazisanifu hizi ofisi mbili za umma wa Watanzania. Ukitazama bango la Idara ya Usalama utabaini kuwa Rais. Julius Nyerere alifanya kazi na Wakurugenzi Watano na huku Dkt. Hassy Kitine(3) na Dkt.Agustino Mahiga(4) ndiyo waliofanya naye kazi kipindi kifupi.
Hiki kilikuwa kipindi cha mwaka 1978-1983 ambacho ni kipindi kigumu cha Tanzania kilichopitia wakati wa Vita vya Kagera, Kesi za uhaini, harakati za kuwasaka wahujumu uchumi, hata kuelekea kung’atuka kwa Mwalimu Julius K. Nyerere, kifo cha Edward Moringe na Tanzania kupata Rais mpya mwaka 1985.
Ebu tujiulize hali ilikuwaje kipindi hiki kwa bango la Makatibu Wakuu Viongozi?
Bango hili linatodokeza kuwa Katibu Mkuu kiongozi alikuwa ni mmoja tu ambaye ni Timoth Apiyo na yeye alikuwa tangu mwaka wa 1974 hadi 1986. Kwa upande wake Ali Hassani Mwinyi yeye amefanya kazi na Mkurugenzi mmoja tu wa Idara ya Usalama wa Taifa ambao ni Luteni Jenerali Imrani Kombe na huku Katibu Mkuu Kiongozi alikuwa ni mmoja tu ambaye ni Balozi Paul Rupia(1986-1996) lakini kidogo alifanya kazi na Timoth Apiyo wakati Ali Hassani Mwinyi anaanza kusimama dede. Kwa upande wake Benjamin Mkapa yeye amefanya kazi na Mkurugenzi mmoja wa Idara ya Usalama wa Taifa ambaye ni Kanali Aspson Mwang’onda huku Katibu Mkuu Kiongozi aliyefanya naye kazi ni Martin Lumbanga peke yake.
Kwa Rais Jakaya Kikwete hapa yeye amefanya kazi na Mkurugenzi mmoja tu wa Idara ya Usalama wa Taifa ambaye ni Othman Rashid na Katibu Mkuu Kiongozi aliyefanya kazi nao ni Lumbanga, Luhanjo na Sifue. Kwa upande wa Rais John Pombe Magufuli na Rais Samia Suluhu Hassan kilichotokea mabango haya mawili yanajieleza vizuri Mwanakwetu haoni haja ya kupoteza muda wake kujadili hili lakini nakuomba msomaji wangu nikukumbushe majukumu ya Katibu Mkuu Kiongozi. Huyu ni mtu muhimu sana kwa kuwa ni kiungo na Idara ya Usalama wa Taifa huku majukumu yake makuu ni haya:
“Katibu wa Baraza la Mawaziri hapa anakazi ya kuandaa ajenda, kuandika kumbukumbu, na kusimamia utekelezaji wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri. Yeye ndiye Mkuu wa Watumishi wa Umma.Kazi yake nyingine ni kusimamia utendaji, nidhamu, na ufanisi wa watumishi wote wa umma. Kazi ya mwisho yeye ndiye Mshauri Mkuu wa Rais: kuhusu masuala ya utawala, sera, na Msimamizi wa Serikali na anahakikisha sera za Serikali zinatekelezwa na wizara na idara zote. Kwa ufupi, Katibu Mkuu Kiongozi ndiye kiunganishi kikuu kati ya Rais, Baraza la Mawaziri, na Utumishi wa Umma.”
Nakuomba msomaji wangu kumbuka maneno haya:
“Msimamizi wa Serikali na anahakikisha sera za Serikali zinatekelezwa na wizara na Idara zote …”
Kwa maelezo haya inaonekana kuwa hata Idara ya Usalama wa Taifa inafanya kazi chini ya Katibu Mkuu Kiongozi ili aweze kumshauri vizuri rais, yeye ni Kiranja Mkuu Msaidizi na yeye ndiye mshauri wa karibu wa Rais. Hapa msomaji wangu rejea majukumu ya Idara ya Usalama wa Taifa ambayo ni
“Kukusanya, kuchambua, na kutoa taarifa za intelijensia kulinda usalama, amani, na ustawi wa nchi. Kazi zake ni pamoja na kuzuia ujasusi wa kigeni, hujuma za kiuchumi, ugaidi, na uzandiki wa ndani.”
Siku ya leo msomaji wangu Mwanakwetu alikuwa mtalii wa Mabango mawili ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Naomba msomaji wangu nikupe dhana ya mchezo wa mpira wa miguu pengine sote tutaelewana.
Huyu Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa katika Mpira wa Miguu Mwanakwetu anaweza kumlinganisha na mchezaji namba sita wa mchezo huu ambaye anajulikana kama kiungo mkabaji (Defensive Midfielder).
“Huyu ni mchezaji muhimu anayefanya kazi kati ya safu ya ulinzi (mabeki) na safu ya kiungo cha ushambuliaji. Kazi zake kuu uwanjani ni:Kuzuia mashambulizi: Hufanya kazi ya kukaba na kuvunja mashambulizi ya timu pinzani kabla hayajafika kwa mabeki wa kati. Kulinda safu ya ulinzi:Yeye Hujenga ukuta wa ulinzi mbele ya mabeki wa kati, akizuia timu kupigwa pasi za katikati. Kuanzisha mashambulizi:Hapa huchukua mpira kutoka kwa mabeki na kuusambaza kwenda kwa viungo wa juu au washambuliaji.Kuunganisha mchezo: Yeye ni kiunganishi kati ya mabeki na viungo wengine, mara nyingi anashuka chini kusaidia kupokea mpira wakati wa kuanzisha shambulizi. Kupunguza presha: Kupitia uwezo wake wa kumiliki mpira na kupiga pasi, anasaidia timu kutulia na kupunguza presha ya mpinzani mchezoni. Huyu ni moyo wa ulinzi wa katikati wa uwanja.”
Msomaji wangu hii ndiyo Idara ya Usalama wa Taifa.
Ukija kwa Katibu Mkuu Kiongozi kwa muktadha uleule wa mchezo wa Mpira wa Miguu yeye ni sawa na namba nane uwanjani:
“Huyu ni Mchezaji anayevaa jezi namba 8 katika mpira wa miguu hujulikana kama kiungo wa kati au mara nyingi huitwa ‘box-to-box midfielder’. Kiungo Mshambuliaji. Majukumu yake makuu uwanjani ni pamoja na: Kuunganisha Ulinzi na Mashambulizi: Anafanya kazi ya kuchukua mpira kutoka kwa mabeki au kiungo mkabaji (namba 6) na kuupeleka kwa washambuliaji (namba 9 na 10).Kutengeneza Nafasi za Magoli: Namba 8 hutumia uwezo wake wa kupiga pasi za uhakika, krosi, na kuona ‘gap (nafasi) ili kutengeneza nafasi za hatari kwa timu yake.Kushambulia na Kufunga: Tofauti na namba 6 anayebaki zaidi nyuma, namba 8 ana uhuru wa kupanda mbele, kuingia kwenye boksi la mpinzani, na hata kupiga mashuti ya mbali. Kukaba (Ulinzi): Kwa sababu ni mchezaji wa ‘box-to-box,’ anapaswa kurudi nyuma kusaidia ulinzi timu inapopoteza mpira ili kuziba nafasi katikati ya uwanja. Kudhibiti Mdundo wa Mchezo: Namba 8 mara nyingi ndiye ‘injini’ ya timu, akizunguka uwanja mzima ili kuhakikisha timu inamiliki mpira na mchezo unakuwa na uhai.”
Kwa hakika Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa taifa na hata Katibu Mkuu Kiongozi si sawa na kuwaondoa uwanjani namba 6 na namba 8 hilo ni kosa kubwa sana maana yake tusilinde goli na tusi shambulie.
Hapa maana yeke mwamuzi kawapiga kadi nyekundu kiungo Mkabaji na Kiungo mshambuliaji. Hapa Mashabika tunalalamikia uamuzi huu maana timu hii haiwezi kushinda mwamuzi amekosea?Maana akina Elias Hamis wa Bandari hawezi kufanya chochote kuelekea goli la timu pinzani. Hiki ndicho kilichofanyika wakati wa kuondolea kwa Afande Diwani Athumani Msuya na Balozi Hussein Kattanga ati kupangiwa majukumu mengine.
Kwa leo msomaji wangu inatosha sana .
Mwanakwetu Upo? Kumbuka:
“Mwaamuzi Kauwa Timu.”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257








.gif)


.gif)
Post a Comment