Mnyonge Mnyongeni Haki yake Mpeni

 


Adeladius Makwega-Musoma-MARA.

Aprili 13, 2026 Mwanakwetu alitembelea Ofisi ya Mbunge wa Musoma Mjini, mheshimiwa Mgore Miraj Kigera kwanza kumsalimia mheshmiwa huyu na kisha kupata majibu ya maswali machache juu ya Jimbo lake la Musoma Mjini ambalo lipo katika Manispaa ya Musoma mkoani Mara nchni Tanzania.

Hapa Mwanakwetu alikaribishwa na mabinti wawili warembo na wakarimu sana. Mwanakwetu alikuwa na maswali kadhaa katika ofisi hii ya Mbunge, miongoni mwao ni changamoto ya wakazi wa Malima Mkomaji Kata ya Kwangwa juu ya changamoto ya kuwekewa kalavati ambalo litaweza kuunganisha mitaa miwili jirani. 

 

Ofisi ya Mbunge wa Musoma Mjini Mhe. Mgore Miraj Kigera ikajibu:

“Changamoto hii tunaifahamu na ofisi ya mbunge imeshafika katika eneo hili na kuzungumza na wakazi wa mitaa yote jirani na hoja hii imefikishwa TARURA kwa ajili ya utekelezaji.”

Mwanakwetu aliuliza swali la pili juu ya baadhi ya wateja wa maji safi na salama kwa baadhi ya maeneo ya Musoma Mjini kuwa kumekuwa na madai za ankara zao za maji kama zinaandikwa tu bila ya kusomwa na mamlaka hayo, hapa Ofisi ya Mbunge wa Musoma Mjini ilisema.

“Malalamiko haya tumeyapokea na kwa hakika katika kupitia vyombo vya habari tunaomba mamlaka husika zijitahidi kusoma mita za maji vizuri na kwa wakati na hili tutalisisitiza katika vikao vya Baraza la Madiwani na hata vikao vya Bunge lakini Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, najua mamlaka ya Maji, Safi Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) inafanya kazi vizuri na ni nadra sana kusikia maji yanakatikakatika mji huu, ninawapongeza sana MUWASA kwa kazi nzuri wanayoifanya.”

Baada ya majibu ya maswali haya mawili Mwanakwetu alitoka zake na kurudi alipotoka.

 

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Haya ni maswali mawili kwa Mbunge wa Musoma Mjini kutoka kwa wakazi wake ambayo yalikusanywa na Mwanakwetu na kujibiwa vizuri . Siku nyingine akienda huku akiwa na swali na kupatiwa majibu atawasilimulia.

Mwanakwetu anamshukuru sana Mbunge wa Musoma Mjini mhe Mgore Miraj Kigera kwa majibu haya

Mwanakwetu upo? Kumbuka:

“Mnyonge Mnyongeni Haki Yake Mpeni.”

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257















 

0/Post a Comment/Comments