Mbunge Musoma Apokea Pongezi za Serikali na Hoja za Wananchi

Adeladius Makwega-Nyamihongo-MUSOMA

“Kabla ya ukoloni eneo la Musoma lilikuwa ni ardhi ya Wakabwa, kundi la Wajaluo waliokuwa wa kwanza walifika hapa na kuhamia, huku Wajerumani wa kwanza walifika mnamo mwaka 1910 wamisionari wawili ambao ni Dominik na Paulo, walijenga makazi na shule karibu na makao ya Mtemi hapo Nyabange kisha wakafuatwa na afisa wa kwanza Mjerumani aliyebatizwa jina na wenyeji ‘Bwana Sirusi’ Akiwa Afisa wa Forodha na inaaminika alihamia Musoma kwa kazi hii huku kina cha maji cha Mji wa Musoma kilifaa kwa meli kutia Nanga.

Ndugu Sirusi alihamia Musoma ya leo kwa sababu hapa kina cha maji ufukoni kilifaa zaidi kwa meli kufika na kutia nanga ndipo baadaye ikawa wilaya hii ya sasa.”

Haya ni historia ya Mji huu mkongwe ambao ndiyo Makao Makuu ya Mkoa wa Mara uliopo Kaskazini Mashariki mwa Tanzania.

 

Haya ni kale je kwa sasa kuna nini?

Mapema ya Aprili 24, 2026 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipokea majibu ya maswali kadhaa ya Serikali kwa Mbunge wa Musoma Mjini Bi Mghore Miraj Kighera juu shabaha ya kufufua Viwanda vya Mkoa wa Mara .

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilisema kuwa inampongeza Mbunge wa Musoma Mjini Mhe.Mgore Miraji Kighera kwa kuwa mfuatiliaji wa maendeleo ya Viwanda na Biashara kwa Mkoa wa Mara maana shabaha ya Serikali mkoa huu kuwa na viwanda vipya kadhaa na kufufua viwanda vya zamani viwili ambavyo vilikuwa havifanyi kazi.

 

Haya yamesemwa Bungeni Aprili 24, 2026 wakati Wizara ya Viwanda na Biashara ikijibu swali la msingi namba 185 na maswali kadhaa ya nyongeza kutoka kwa Mbunge Kighera Miraji.

“Kipaombele cha kufufua viwanda kimeanza ambapo Kiwanda cha Nguo Cha Musoma na Kiwanda cha Maziwa cha Musoma vinafufuliwa maana taratibu zinakamilika. Mbunge wa Musoma aondoe shaka zoezi hili linafanyiwa kazi kwa ueledi.”

 

Wakati haya yakiendelea Bungeni Dodoma, Mbunge wa Musoma Mjini amepokea malalamiko kadhaa ya wakazi wa Makoko wakiomba kufungwa haraka kwa Mtambo wa X Rays ambao upo Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere upachikwe ili uweze kufanya kazi katika Hospitali hii ya Rufaa ambapo kwa sasa huduma hii inatolewa Hospitali ya Manispaa ya Musoma.

Wakazi hao wa Makoko waliomba pia kukamilika haraka kwa chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali hii.

 

Akitoa Majibu ya hoja hii kwa wananchi Nyamiongo Makoko Mhe Kighera Miraj amesema kuwa anatambua kuwa hivi karibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya alitembelea Hospitali hii huku akitoa maagizo kadhaa lakini yeye anazibeba hizo hoja kama zilivyo na atazifikisha Wizara ya Afya ili ziweze kufanyiwa kazi haraka.

Kwa upande wa Wananachi wa Kiara B wao wamemuomba Mbunge wa Musoma kutatua changamoto ya mabomba ya maji ili yaweze kufika katika mtaa huo. Akilijibu swali hili Mhe. Mgore amesema kuwa hoja hii anaibeba na ataifikisha Mamlaka ya Maji Musoma MUWASA na litafanyiwa kazi.

 

Kwa upande wao wananchi wa Mtaa wa Mshikamano wakiongozwa na Ndugu Joseph Sese Warioba alisema kuwa wananchi wa eneo lao wanachangamoto ya barabara za mitaa kupitika tu hili lifanyiwe kazi. Mh Mghore Kighera Miraji alisema kuwa hili analibeba na litafanyiwa kazi.

Wakati haya yaliendelea hali ya hewa ya Mji wa Musoma ni nyuzi joto 27, unyevunyevu ni wa asilimia 10 ujirani na mvua ni wa asilimia 56 na upepo ukivuma kwa KM 8 kwa saa.

Mwanakwetu upo? Kumbuka:

“Mbunge wa Musoma Apokea Pongezi za Serikali na Hoja za Wananchi.”

Nakutakia Siku njema.

makwaadeladius@gmail.com

0717649257

 















 

 

 

 

 

0/Post a Comment/Comments