
Tanzania yetu inachekesha sana, pale tunapoyazungumzia masuala makubwa ya taifa letu wako wapumbavu, wako wajinga na wako bumbumbu mzungu wa reli wachache wanaotumia dhana ya dini kuficha udhalimu wao.
Hatuwezi kumsema mtu yoyote kwa sababu ya Uisilamu wake, hatuwezi kumsema mtu yoyote kwa Ukristo wake na hatuwezi kumnanga mtu kwa Upagani wake na hatuwezi kumsema mtu yoyote kwa sababu ya Ubudha wake. Tunamsema mtu huyu kwa namna yeye mwenyewe alivyoshindwa kutenda iliyo sahihi kwa manufaa ya Watanzania wote. Katika hili msomaji wangu binafsi nikwambie hili, nilikula kiapo miaka kadhaa nyuma kuwa kama nitakutana Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Philip Mpango siwezi kumpa shikamoo yangu, kwa hoja moja tu akiwa amekalia kiti hicho alishindwa kuonesha umahiri wake kama msomi, umahiri wake kama kiongozi na umahiri wake kama Mtanganyika Wakati Bandari ya Dar es Salaam Inapelekwa Sokoni.
Msomaji wangu lazima ufahamu kuwa Dkt. Philipo Mpango ni Mkristo lakini hili haliwezi kubadilisha msimamo wa Mwanakwetu maana kinachoaminiwa na Mwanakwetu ni kuwa Dkt. Mpango hakuitendea haki nafasi hiyo na ndiyo maana inawekwa hadharani kuwa Dkt. Emmanuel Asiwe Kama Dkt .Philip Mpango.
Nakuomba msomaji wangu ufahamu hivi:
“Kumronga(kushugulika) Dkt. Philip Mpango ilikuwa kazi ngumu maana Dkt. Mpango siasa zake kaanzia ukubwani lakini kumroga Dkt. Emmanuel Nchimbi ni kazi nyepesi sana maana siasa zake kaanza udogo, tunamjua uimara na udhaifu wake tangu enzi. Hivyo kushughulika naye kama akikengeuka ni jambo jepesi wewe unaamua kwa kuchagua pa kuanzia kama ni unyayoni, kiunoni au kichwani na kazi imamalizika haraka.
Kwa hiyo Dkt .Nchimbi awe makini kwa maslahi ya Tanganyika hili linasemwa bayana na hukuna haja ya kumficha.”
Kwa hakika siyo kweli kwamba mtu yoyote anayesemwa nchini Tanzania kwa sasa ni kwa kuwa ni Muisilamu bali tunasema kwa kuwa ameshindwa kuonesha uhodari katika masuala ya Taifa hili.
“Kwani Dkt .Philip Mpango anasali Msikiti wa Manyema?Au Dkt Philip Mpango alipokuwa Makamu wa Rais alibadilisha dini na kuwa Muisilamu?”
Labda msomaji wangu nikukumbushe wakati wa hoja ya hati rasmi ya makubaliano kati ya pande mbili juu ya Bandari ya Dar es Salaam Mwanakwetu alichunguza mengi na mojawapo ni hivi ni kina nani hao wanaokwenda huko Arabuni na kurudi katika biashara hiyo? Hasa zoezi hili katika wizara husika?Majibu yalikuwa haya?
“Wizara husika anakwenda Waziri Profesa Makame Mbawala, Naibu Katibu Mkuu Dkt. Ally Possi na timu ya watu kadhaa.”
Wizara hiyo ilikuwa na Katibu Mkuu ambaye alikuwa hashiriki na wala kibali chake cha kusafiri kilionesha hakuwa na safari za nenda rudi nenda rudi huko Arabuni. Huyu Ally Possi ambaye ni mwanasheria awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na baadaye Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kisha akapelekwa huku kwenye Bandari.
Ukimtazama Dkt. Ally Possi ndiyo alikuwa anaanza maisha na hata ndoa yake ilikuwa bado changa akiwa na watoto wadogo na hata harakati za kujenga ndiyo zilikuwa zinafanyika. Haya ni kwa utafiti wa Mwanakwetu juu ya MOU ya Bandari ya Dar es Salaam wakati huo.
Kwanini Katibu Mkuu hawamshirikishi? Aliyeulizwa swali hili alisema kuwa yaani wanamvuka mzee wa watu nayeye hataki ugomvi na mtu ili astaafu salama. Baadaye Wizara hii ilitenganishwa na kuwa wizara mbili na yule Katibu Mkuu aliyekuwa mtulivu aliondolewa kabisa na huyu Dkt. Ally Possi akaenda kuwa Wakili Mkuu wa Serikali.
Kwa wale wanaokumbuka kipindi hiki ndiyo Diwani Athuman Msuya anaondolewa Ukurugenzi wa Idara yetu ile na hata Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Katanga anaondolewa nafasi yake na kurudi kuwa Balozi .
Swali la Mwanakwetu lilikuwa ni kwanini Balozi Hussein Katanga akae katika nafasi hii kwa kipindi kifupi? Wakati wapo Makatibu Wakuu Viongozi kadhaa waliweza kuifanyia kazi ofisi hiyo hadi marais wawili? Shida ni nini? Mwanakwetu alikuwa na mawazo mengi na mojawapo alilodhani ni hili la Bandari ya Dar es Salaam. Je Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Kattanga alikuwa na msimamo gani katika hili? Swali la kujiuliza Balozi Moses Kusiluka aliyekuja baadaye Kuwa Katibu Mkuu Kiongozi yeye alipoingia ofisini alikuwa na msimamo gani? Je Profesa Moses Kusiluka msimamo wake ndiyo unaosababisha akae hapo kipindi kirefu chote hiki? Yeye amekubali Bandari yetu ipelekwa sokoni?
“Ukiyaangalia majina haya mawili Diwani Athuman Msuya na Balozi Hussein Kattanga hawa jamaa wanasali Azania Front au wanasali Saint Joseph Cathedral na Je huyu Profesa Moses Kusiluka anasali Masjib Abubakari Zuberi pale Chamwino Ikulu?”
Nina hakika inafahamika Balozi Hussein Katanga ni Muisilamu nayeye Balozi Moses Kusiluka ni Mkristo. Hayani mawazo ya Mwanakwetu siku ya leo.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Kwa hakika ukitazama hali ya Tanzania ilivyo inaonesha wapo Waisilamu wengi katika Utumishi wa Umma wanaonesha uhodari mkubwa wa kulinda rasimali za umma wa Watanzania kwa nafasi zao walizokalia na hakuna haja ya mtu kubaki katika nafasi kisha mwingine afanye atakavyo. Hapa simulizi nyingi zikisimuliwa juu ya Balozi Hussein Kattanga na wengine wengi. Hapa kinachoelezwa ni mchango wa kila mmoja kulinda Tanzania na siyo hoja ya dini ya mhusika.
Mwanakwetu upo?Kumbuka:
“Kwani Balozi Hussein Kattanga Anasali Kanisa la Azania Front?”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257








.gif)
.gif)
Post a Comment