Adeladius Makwega-MBAGALA
Vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vinaendelea katikati ya Jiji la Idodomia(Dodoma) nchini Tanzania, nayeye Mwanakwetu akiwa madongo poromoka amekuwa akifuatilia kwa karibu kila kinachowasilisha na kujadiliwa hatua kwa hatua, huku akipima namna wabunge wetu wanavyochangia, wanavyotoa maoni yao na hata kuuliza maswali ndani ya Bunge hili la Tanzania , taifa la Afrika ya Mashariki.
Mwanakwetu anafahamu fika kuwa Changamoto kubwa ya mataifa ya Afrika ni kuwa na Bajeti Tegemezi ambayo inategemea sana wafadhili kutoka nje na huku kukiwa na kidonda ndugu cha matumizi ya fedha katika mambo ya kawaida mambo yasiyo ya msingi.
Katika kulichanganua hili Aprili 19, 2026 Mwanakwetu alifanya mazungumzo na msomi mmojawapo wa ngazi ya Shahada ya Uzamili nchini Tanzania juu ya hali ya Bajeti ya Taifa hili kwa mwaka wa fedha 2026/2027 kulingana na mawasilisho yao Bungeni.
Ndugu huyu kwanza aliyasema haya:
“Chanzo ni mapato ya ndani kutoka Mamlaka ya Mapato na Kwa Bajeti inayoendelea uwezo ni wa Trioni 40 na huku mapato mengine kama faini, halmashauri ni kama Trioni 6 jumla kuu inakuwa Trioni 46.”
Msomaji wangu tambua kuwa Mwanakwetu anajua kuwa unaweza kukusanya vizuri lakini changamoto ni pale unapopanga matumizi ya haya makusanyo, hapa ndipo mapishi yanaweza kuharibika na ukapikwa ugali mbichi na kushindwa kulika, Watanzania tunavaa viatu ya kushoto kulia na kulia kushoto:
“Ukiangalia Ofisi ya Rais, Ofisi ya Makamu wa Rais na Waziri Mkuu. Kwa Ofisi ya Makamu wa Rais haina mambo mengi, hakuna miradi pale yeye ana Muungano na Mazingira tu. Changamoto ipo kwa Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Rais fedha za matumizi ya kawaida ni Trioni 9.5 hizi ni fedha nyingi. Makamu wa Rais ni kama bilioni 150-200 tu huwa haiwezi kuzidi hapo.
Kwa upande wizara ambazo mara nyingi zinapata pesa nyingi ni elimu mathalani miaka ya nyuma walipata trioni 7, afya walipata trioni 5, Nishati trioni 4 na ujenzi Trioni 4. Niseme tu kwa hapa tunataka kuona sura ya bajeti yetu inakuwaje?”
Kwa hakika madhaifu yapo mengi huku Mwanakwetu akifuatilia mawasilisho ya wizara kadhaa huku marajio ya Mwanakwetu ni kwa wabunge wetu wawe na macho ya kuyaona haya ili fedha ziweze kwenda katika mambo ya msingi mambo ya lazima.
Ebu msomaji wangu twende hatua kwa hatua kwanza tuyatazame majukumu ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora:
“Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (OR-MUUUB) ina jukumu la kuimarisha utawala bora, kusimamia rasilimaliwatu, sera, sheria na taratibu za utumishi wa umma, pamoja na kukuza maadili na serikali mtandao ili kutoa huduma bora kwa wananchi.
Huku Majukumu Makuu ni pamoja na kuandaa na kusimamia sera, sheria, na taratibu za utendaji katika Utumishi wa Umma, Kusimamia ajira, mishahara, mafunzo, na maendeleo ya watumishi wa umma, Kukuza uadilifu, uwajibikaji, na uwazi katika utumishi wa umma, Kusimamia mifumo ya TEHAMA na utendaji kazi wa kisasa serikalini, Kusimamia mifumo ya nyaraka za Taifa na Kuboresha miundombinu na utoaji wa huduma kwa wananchi.”
Msomaji wangu haya ni majukumu ya OR-MUUUB inayoongozwa na Waziri Mhe. Ridhiwani Kikwete(Mb) ambaye aliteuliwa mara baada ya uchaguzi wa Oktoba 29, 2025 na huku Katibu Mkuu ni ndugu Juma Seleiman Mkomi, huku kumbukumbu zinadokeza kuwa ameanza kukalia kiti hiki tangu Februari 27, 2023 akiwa ni Katibu Mkuu ambaye ahamishwi hamishiwi.
Sasa msomaji wangu twende Bungeni tuitazame Bajeti ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambayo ndugu Seleiman Mkomi na wataalamu wake ndiye wao wameandaa:
“Utumishi wa Umma na Utawala Bora wamepanga trioni 1.4 kwa matumizi ya kawaida(OC). Hizi ni fedha nyingi sana na kwa kufanya ulinganifu lile Daraja la Kigongo Busisi limejengwa kwa bilioni 700 hapa unajenga madaraja mawili, kwa Daraja la Tanzanite pale Dar es Salaam unajenga sita kama yale maana lile lilijengwa kwa bilioni 200 na ushehe. Hivi kweli unapeleka trioni 1.4 katika matumizi ya kawaida kama vile posho?
Kama hii haitoshi ikumbukwe kuwa Rais alikopa trioni 1.3 pesa za uviko zilipelekwa kuboresha shule, madarasa na vituo vya afya ambayo awali ileta maneno hadi Spika wa Bunege la wakati huo mhe Job Ndugai akajiuzulu. Hizi trioni 1.3 na kweli fedha hizi zilikuwa na mchango mkubwa sana katika uchumi wetu kule zilipopelekwa sasa kweli wewe unapanga kutumia trioni 1.4 kwa matumizi ya kawaida?”
Msomaji wangu unayaona haya? Vipi wabunge wetu wanatayaona haya?
Msomaji wangu hii ni safari ya uchambuzi wa bajeti kwa jicho la daktari huyo wa falsafa na Mwanakwetu na kisa cha mfano ni Ofisi wa Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora nchini Tanzania kwa mwaka wa fedha 2026/2027 lakini pengine wabunge wanaweza kuyaweka mambo sawa.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Kwa wizara hii Ridhiwani Kikwete tumuweke kando maana ni mgeni na ninaweza kusema kakuta watu wameanda bajeti, hili halina ubishi lakini mtu wa kuhangaika naye ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ndugu Seleiman Mkomi.
“Haiwezekani trioni 1.4 zipangiwe matumizi ya kawaida maana bado Watanzania wana changamoto tele katika sekta kadhaa na fedha zipelekwe kwenye sekta ya Afya. Kilimo na Elimu.”
Kwa kifupi Mwanakwetu anashauri ndugu yetu Seleiman Mkomi amekaa muda mrefu katika wizara hii tangu mwaka wa 2023 nashauri mamlaka ya uteuzi ipeleke Katibu Mkuu mwingine na ndugu Mkomi ahamishiwe taasisi zingine.
“Hili litasaidia kutoa fursa ya mawazo mapya, mitazamo mipya na kutoa fursa kwa Watanzania wengine kuonesha vipaji vyao katika hapa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Umma na Utawala Bora, maana utumishi wa umma wa Tanzania ni rasimali mojawapo ambayo watanzania wameirithi kutoka kwa mkoloni”
Kupeleka trioni 1.4 katika matumizi ya kawaida ni sawa na kugeuza viatu yaani Kiatu cha Kushoto Kulia na Kulia Kushoto. Hapa hauwezi kutembea vizuri , kiongozi wetu atapotea njia na kuelekea vichakani na huko atagongwa na nyoka , huyu ni ndugu yetu lazima tumuwahi mapema.
Mwanakwetu Upo?Kumbuka:
“Katibu Mkuu Menejimenti Utumishi wa Umma Hodari wa Kugeuza Viatu.”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257

.gif)





.gif)


Post a Comment