KANALI MTAMBI AWATAKIA HERI YA PASAKA WANA MARA

 



Adeladius Makwega-MBAGALA

“Nawatakia heri ya Pasaka wana Mara wote, nawasihi kila mmoja wetu asherehekee sikukuu hii kwa amani na utulivu, baada ya sikukuu hii kila mmoja wetu aweze kurejea salama katika mraba na duara lake pale anapojiingizia kipato maana wana tunasema MINGANYARO KWANZA…”

Haya ni maelezo ya Mkuu wa Mkoa wa Mara mheshimiwa Kanali Evans Alfred Mtambi akizungumza kwa njia ya simu akiwatakia heri wananchi wa Mkoa wa Mara nchini Tanzania.

Mraba ni pahala panapofanyika kazi yoyote ile hasa ya kilimo, duara ni sehemu inapochimbwa madini ambapo kila mchimbaji hupewa eneo lake lenye madini ili achimbe na huku Miganyaro ni mgao wa fedha kwa haki kwa kila mfanyakazi ambaye ni mchimbaji madini katika duara lake baada ya kufanya kazi ya kuchimba madini.Hii ikiwa misamiati maarufu sana mkoani Mara. Huu ukiwa mkoa wenye utajiri mkubwa wa madini ya dhahabu.

Awali akizungumza na wafanyakazi wa Halmashauri ya Butiama katika Shule ya Amali, Katibu Tawala Mkoa wa Mara Ndugu Gerald Musabila Kusaya nayeye aliwatakia heri ya Pasaka Wafanyakazi wote wa Mkoa wa Mara.

“Wafanyakazi wangu najua siyo wageni wa sherehe. Natambua ugeni una mambo katika sherehe, mimi nawatakia Pasaka Njema.”

Pasaka ni sherehe ya Wakristo ulimwenguni ambayo husherekewa Jumapili baada ya Ijumaa Kuu ambapo ni sikukuu ya baada ya Yesu kusubiwa msalabani, kufa na kufufuka  katika wafu siku ya tatu

makwadeladius@gmail.com

0717649257







 

 

0/Post a Comment/Comments