Jengeni Kwa ubora Nyumba Zenu Za Ibada

 

 

Adeladius Makwega-MBAGALA.

 

“Bwana wa Majeshi asema hivi, ya kwamba, watu hawa husema. Huu sio wakati utupasao kuja, huu sio wakati wa kujenga nyumba ya Bwana. Ndipo Neno la Bwana lilikuja kwa kinywa cha Nabii Hagai, kusema. Je huu ndiyo wakati wa ninyi kukaa nyumba zenye mapambo ya mbao, iwapo nyumba hii inakaa na kuharibika? Bwana Sasa, Bwana Wa Majeshi asema zitafakarini njia zenu.”

Haya ni maneno ya Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa nchini Tanzania Mhe. Rhimo Nyahsaho, Aprli 11, 2026 akiyanukuu kutoka kitabu cha Hagai sura ya kwanza 1-5 , hapa akihimiza Wakristo nchini Tanzania kuendelea kujenga nyumba zao Ibada maana si jambo jema kama Mkristo anakaa katika nyumba nzuri huku kanisa lake lipo hoe hae.

Mhe. Nyahsaho ameyasemema haya wakati akiongoza uchangiaji wa Harambee ya ujenzi wa Ofisi za Jimbo la North Mara za Kanisa ya Waadiventista Wasabato hapa Tarime Mkoani Mara.

Akizungumza katika uchangiaji huyo Mhe. Nyahsaho alisema:

“Mimi nimekuja hapa kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe.Mwigulu Nchemba ambae mlimualika na hata kama yeye angekuja mimi lazima ningeshiriki nanyi maana mimi ni Msabato pia natokea Mkoa huu wa Mara.”

Akiendelea kusoma hotuba yake Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa alisema:

“Ninashukuru Kanisa hili limefanikisha kuwapa elimu Watanzania kadhaa akiwemo Profesa Philemone Sarungi, Profesa Samweli Wangwe na wengine wengi tangu lilipoanza huduma zake za elimu mwaka 1913 katika eneo la Tarime na huku matunda haya ya Profesa Wangwe na Profesa Sarungi yamewanufaisha Watanzania wengi.”

Awali Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi akizungumza wakati akimkaribisha Waziri wa ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa alimshukuru sana Waziri huyu kwa kuwa jirani na wana Mara huku akishrikiana nao kwa karibu japokuwa sasa amekuwa na majukumu ya kitaifa.

“Karibu sana Mara, Mkoa wetu sasa mambo yetu ni mazuri hatupo namba moja katika mambo mabaya sasa mkoa wetu una utulivu mkubwa.Tunaonda ulitazame vizuri suala la barabara hii ya Tarime.”

Katika harambee hiyo Waziri Mkuu mhe Mwigulu Nchemba, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mkuu wa Mkoa wa Mara walichangia milioni themanini na mbili huku waamini wa Kanisa la Waadeventista Wasabato wenyewe walichangia milioni 500 na ushehe huku changizo hili likakusanya karibu shilingi milioni 600 za Kitanzania.

 

Shughuli hii iilihudhuliwa na viongozi mbalimbali kutoka Wilaya na Halmashahri zote za Mkoa wa Mara wakiongozwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara ndugu Humphrey Frolence Kong’oke.

“Nipo pamoja na viongozi hao wote na pamoja na Wakuu Idara, vitengo na sehemu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara. Kikubwa tumetumia magari machache kutii agizo la serikali la kutumia magari machache, tumelitekeleza ili kubana matumizi ya mafuta”

Ndugu Kong’oke alisema.

Katika harambee hii kulikuwa na mambo mengi ya kuvutia, Mwanakwetu anakutajia mawili: Mosi namna waamini wa Kanisa la Waadeventista Wasabato walivyoweza kukusanya karibu shilingi milioni 500 na ushehe ambayo ni inakaribia dola 200,000 za Kimarekani ambayo ni pesa nyingi.

Pili: Wakati Mkuu wa Mkoa wa Mara anaongea na hadhara hii ili kumkaribisha Waziri wa Ulinzi aliomba umati uliokusanyika wa Kanisa hili kuimba wimbo wa Jina la Yesu Salaam:

“Jina la Yesu Salaam Lisujudieni, Lisujudieni, Ninyi Mbinguni, hukumu.

Na enzi na enzi na Enzi na Enzi Mpeni…”

Wimbo huu uliwachangamsha watu wote walioshiriki harambee hii bila kujali kama walikuwa wa dhehebu gani.

Mwanakwetu upo? Kumbuka:

“Jengeni Kwa Ubora Nyumba Zenu za Ibada.”

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257




















 








 

 

 

0/Post a Comment/Comments