Mchungaji na Steven Jacob wa Kanisa la Huduma ya Kristo, liliopo Mtaa wa Fanya Fujo Uone(FFU) Murieti Jijini Arusha nchini Tanzania, ambaye ni miongoni mwa viongozi wa dini nchini Tanzania aliyewahi kutekwa na kutupa vichakani, huku akiumizwa vibaya mwaka wa 2025, Machi 10, 2026 amewaomba wahumini wa Kanisa Katoliki Ulimwenguni kumlinda kiongozi wao maana Injili ya Ulimwengu ina gharama kubwa, huku akirejea maisha ya mitume wa Yesu Kristo kama Vile Bathromayo kule India na hata Paulo Mtume ambayo gharama yake ilikuwa ni kupoteza uhai.
Akiendelea kuongea katika katika kanisa lake Mchungaji Jacob alisema:
“Wanadamu walimuuwa Yesu Kristo ambaye hakuwa na baya alilolifanya bali ni kile kile cha kuitangaza injili yake kwa Mataifa. Watu wengi huwa wanaomba Mungu awape Baraka ya kufanya Injili ya Kitaifa na Kimataifa hizi ni Injili hatari sana ni heri mtu abaki na Injili yake ya ngazi ya chini.”
Mchungaji Jacob aliomba kwa kama kuna Mkatoliki yoyote anayeusikia ujumbe huu basi ni vizuri kwa uungwana aubebe na kumkishia Padri wake, Askofu wake na hata Kadinali wake ili umfikie Baba Mtakatifi mwenyewe maana anaona kama kitu kibaya kinakuja kumfika huyu kiongozi wa Wakatoliki Ulimwenguni.
Akizungumza kwa upole sana hatua kwa hatua Mchungaji Jacob alisema maneno haya:
“Leo Machi 10, 2026 sihubiri wana kufundisha, bali nitaongea unabii tu tunaombea ulinzi wa familia , ulinzi wa jamii na ulinzi wa shughuli tunazofanya. Naomba nilizungumzie jambo hili kwa kina wale mnaosali Kanisa Katoliki, naomba kwa hisani yenu muuchukue huu ujumbe, mimi ninaongea kwa Kiswahili na nyinyi mumfikishie yule mhusika, kwa namna inayofaa , nyinyi mnaweza kumfikishia tu, nyinyi pia mkapeana habari. Mungu anaweza kukuonesha mambo yajayo ili mmoja wetu aweze kujiepusha na aweze kujilinda-Bwana Yesu Asifiwe sana.
Ulimwengu huu kuna wanaouendesha, wote hawa marais wetu na wakuu wa dini upo mwamvuli chini yao.
Usiku wa kuamkia Machi 10 nimeonesha kuna kikao cha waendesha ulimwengu kimekaa, sikujaliwa kuona nyuso zao lakini nimeona kikao cha waendesha ulimwengu wakakaa, wakawa wanasema wanataka kuanzisha mfumo mpya wa ulimwengu, kuanzisha maisha fulani mapya hapa duniani, aina mpya ya maisha katika ulimwengu huu lakini kuna watu kana kwamba wanalizuia hilo jambo kufanikiwa, ni kama wanazuia huu mfumo mpya kufanya kazi.
Kile kikao kimekaliwa wakatoa amri itembee mataifa yote na falme zote na itekelezwe mara moja na amri ya kwanza ambayo imetolewa ni ya kushughulika na Baba Makatifu Leo wa XIV. Mimi siyo Mkatoliki wala sisali huko, sijui kwa nini Mungu kanifunilia hili lakini najua Bwana Yesu akikusemesha usema tambua kuwa kuna kusudio.
Agizo la kwanza walilolitoa katika kikao chao linasema washughulike na Baba Mtakatifu Leo wa XIV, Baba Mtakatifu wa sasa.
Haya ni mambo mazito lakini tuongee kwa wepesi tu kikaa chao kimekaa washughulike na Baba Mtakatifu Leo wa XIV ambaye kwa asili ni Mmarekani lakini yupo Vatikani. Ulimwengu unaposema unashughulika na wewe siyo kukuweka jela, kwa lugha rahisi tambua kuwa wanataka kumuondoa. Wakatoliki tambueni kuwa mimi ni nabii kama mnaweza kumlinda mchungaji wenu mumlinde na kama mnaweza kumshauri aepuke siasa la ulimwengu basi mfanye hivyo, afanye hivyo mapema. Huu ujumbe unatolewa kwa Kiswahili, najua yupo mtu ambaye anaweza kutafuta mbinu na kumfikishia basi na afanye hivyo.
Kama huu ujumbe usipomfikia basi mtasikia taarifa ambayo siyo nzuri. Jamii hiyo imeshakaa katika kikao kibaya maana jamii hiyo inaona kuwa Baba Mtakatifu Leo wa XIV amekuwa kikwazo kwao na amekuwa akitoa maagizo kuzuia udhalimu ajenda yao kwa maaskofu wake wa mataifa mbalimbali.
Hili pia limeagizwa kwa kuwafanyia hu uovu hata kwa Maaskofu mbalimbali wenye msimamo wa Baba Mtakatifu Leo wa XIV.
Najua katika baadhi ya majimbo ya Kanisa Katoliki, naomba mtambue kuwa katika baadhi ya majimbo ya Kanisa Katoliki na hata vigango yana uhamsho na baadhi ya majimbo hayana, hili lipo Katika Kanisa Katoliki yapo baadhi ya mambo Maaskofu fulani wanayachukua kwa msimamo wa Baba Mtakatifu ndivyo ilivyo katika hili ninalolisema.
Baadhi ya Maaskofu kama wanataka kulinda nafsi zao hapa dunia waache siasa za ulimwengu, haya ni mambo ya dunia nzima.
Agizo hilo limeagiza pia lishughulike hata na wasemaji mbalimbali ambao wana msimamo wa Baba Mtakatifu Leo wa XIV.
Najua hapa Tanzania yupo msemaji mmoja anayeishi huko Marekani huwa anavaa wigi la aina moja na hata yeye ameingizwa katika orodha hiyo.
Mimi binafsi sifahamu Baba Mtakatifu Leo wa XIV ametoa agizo gani huku najua viongozi wa Kanisa Katoliki watalielewa hili jambo vizuri.
Unajua siasa za kitaifa zina nafuu sana hapa ukigombana na watu wanakufungulia kesi miaka minne mitano unahangaika nayo wee kisha wanakufunga lakini siasa za ulimwengu hawana muda huo.
Injili kwa Mataifa ina gharama kubwa, wewe kama unajaliwa kufanya Injili yako ya mitaani baki nayo huko huko lakini Injili ya Kitaifa na ya Ulimwengu ina gharama kubwa.”
Mchungaji Steven Jacob ni miongoni mwa Viongozi wa Kiroho nchini Tanzania ambao wanatumia vizuri mitando ya Kijami kutoa mahubiri yao na tabiri kadhaa za kisiasa ambazo mara zinafuatiliwa na Watanzania kadhaa.
Mwanakwetu upo? Kumbuka:
“Wakatoliki Mumlinde Baba Mtakatifu Leo wa XIV.”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257.
.gif)
.gif)
Post a Comment