Utafauti Wako Unaweza Kusababisha Watu Wakukumbuke.

 


 

Adeladius Makwega-MBAGALA

Wiki hiyo Mwanakwetu alikuwa Mwalimu wa Zamu pale Isimani Sekondari. Mwanakwetu alitimza wajibu wake vizuri huku wanafunzi wakifanya shughuli zao zote na wakishiriki jukumu lao la kusoma vizuri.

Mwanakwetu akiwa zamu siku hii alishangaa wazazi kadhaa wakifika shuleni hapo, huku wakiuliza ofisi ya Walimu ipo wapi? Waliekezwa na kwenda ili kukutana na Mwalimu wa nidhamu.

Kama mwalimu wa zamu Mwanakwetu alitakua kujua hapo shuleni kunanini? Majibu aliyapata kwa Mwalimu wa Nidhamu kuwa kuna kundi la mabinti wasichana wanaoishi katika Bweni ya Parokia ya Isimani wamerushiana maneno na mtawa wa Kike wa Kanisa hili ambaye ndiye kama mlezi wao huko bwenini.

Mwalimu wa Nidhamu akasema majina ya wasichana wenyewe ni haya hapa akitaja moja baada ya lingine kama akija mzazi msisite kumleta hapa kwangu ili tuyazungumze.

Kwa faida ya msomaji wa Mwanakwetu hii ilikuwa ni mwaka wa 2005 miezi ya mwanzoni. Huku mbunge wa Isimani ni mheshimiwa Wiliam Lukuvi.

Wakati shule hii ilikuwa ya kutwa kidato cha kwanza hadi cha nne, wanafunzi wavulana wachache walitengewa madarasa mawili yakiwa mabweni huku Kanisa Katoliki Parokia ya Isimani likatoa mabweni mawili huko Kanisani huku likawa linawahifadhi wanafunzi wa kike kwa gharama nafuu baada ya mbunge wa Isimani kuomba hisani hiyo.


 

Mwanakwetu akatimiza wajibu wake vizuri wa kuwaelekeza wazazi hao pahala alipo mwalimu wa nidhamu na jambo hili likawa linazungumzwa.

Siku hii hata sista huyu wa Kanisa Katoliki Isimani alikuja amekarisika mno nap engine hata kabla ya kikao hiki hata Baba Askofu wa Jimbo hili wakati huo Taricisius Ngalale Kumtwa pengine alipigiwa simu ya upepo kuambiwa kilichotokea, mtawa huyu alikuwa mweupe hadi macho yyake yalikuwa mekundu namna alivyorushiana maneno na wanafunzi wa kike mabapo wote walikuwa wa kidato cha nne.

Kwako msomaji wangu nadhani itakuwa busara kama nitaelezea kiasi juu ya Parokia ya Isimani ilivyokuwa:

“Parokia hii ilikuwa inaongozwa na Padri Muitaliano aliyekuwa anafahamika kama Padri Angela, huku ikiwa ni Parokia yenye miradi kadha ya kilimo kama vile mashamba makubwa ya mahindi na trekta kadhaa zilikodishwa kwa wakulima.”

Ugomvi baina ya mabinti wakubwa kidato cha nne na mtawa wetu chanzo hakukifahamu lakini mazingira ya utatuzi wa mgogoro ndiye aliyoyaona tu Mwanakwetu.

“Mazingira ya Isimani Tarafani kwa mwaka wa 2005 yalikuwa Kijijini mno na wanafunzi waliokuwa wanasoma walikuwa kutoka familia masikini huku hekaheka za kuwasaka mabinti wa kazi kutoka Iringa zilikuwa zimepamba moto.Kama kazi ya mabinti wa kazi wangekuwa wanyama kama swala basi mkoa wa Iringa ungekuwa Mikumi .”

Muda wa wanafunzi kurudi nyumbani ulifika, ikagongwa kengele wanafunzi wa kike na wale waliopanga mitaani wakarudi mitaani huku wavulana waliokuwa wanakaa shuleni katika madarasa mawili wakawarudi bwenini huku wale wasichana wanaokaa Parokiani wakarudi kwa paroko.

Msomaju wangu nakuomba kumbuka kikao cha nidhamu kinafanyika mabinti wale, wazazi wao wanajadili hilo.

Mwanakwetu yeye anaendelea na zamu akawongoza wanafunzi wa bweni kula ugali wao na maharage huku, wanafunzi wanasikiliza nyimbo za bongo flava kwenye redio zao, hapa shuleni hata umeme hakuna.

Majira haya sasa ni jioni aliyeopo ni shuleni Mwalimu Nidhamu kikaoni nayeye Mwanakwetu ambaye mwalimu za zamu.

Msomaji wangu nakuomba ufahamu na hili, Mwanakwetu alikuwa na simu yake moja ya Nokia na hapa shuleni mtandao ulikuwa unapatikana nyuma ya choo cha walimu, simu ikipigwa ukiwa ofisini unakimbilia nyuma ya choo cha walimu unaongea huko bila kujali aliye chooni kama anatumbo la kuhara au la, huko yeye atajua mwenyewe.

Mwanakwetu yu ofisini akaandika ripoti ya siku hii kisha kujiandaa ili aweze kuondoka kurudi Isiman Mjini ambapo alikuwa anakaa katika nyumba ya kijiji kando ya Barabara ya Iringa Dodoma jirani na ule msikiti kando ya godauni la Kijiji.


 

 

Kabla Mwanakwetu hajaondoka kikao cha nidhamu kikamalizika wazazi wakatoka na mabinti zao kila mzazi akachukua njia yake kurudi kwake iwe kwa baiskeli au miguu  hawa ni wazazi wa Kitanzania kama wa Chamundindi, iwe Pawaga, Iwe Migori iwe Nduli, iwe Ndolela, iwe Iringa Mjini hapa kila mmoja na njia yake.

Mwalimu wa nidhamu akatoka wa mwisho ofisini akasema Makwega nimeshamalizana na mgogoro huu, sasa narudi nyumba funga ofisi za shule yako. Mwanakwetu akafunga ofisi zote na kuipeleka funguo nyumba kwa Makamu Mkuu wa Shule na kuanza safari ya kama dakika 15 kuelekea alipokuwa anakaa.

Akiwa njiani Mwanakwetu akamuona mama mmoja mrembo, kapendeza sana mbele yake na kama vile alimuona shuleni! Mwanakwetu akaongeza spidi akimsogelea huyu mama huku akisema huyu mama wa wapi?

Msomaji wangu tambua kuwa Mwanakwetu ni wa mjini katokea Mbagala Dar es Salaam, hapa yupo Isimani Iringa Vijijini anakutana na mama ambaye hakuamini macho yake.

Mwanakwetu hapa anapita njia ya mkato kurudi Isimani Mjini, baadaye akili yake ikaungama kuwa huyu mama ni miongoni mwa wazazi ambao watoto wao walikuwa wamerushiana maneno na yule mtawa wa kike kule Parokiani. Swali la Mwanakwetu mbona huyu mama yu tafauti na wazazi wengine waliokuja katika mashauri ya watoto wao?

Mwanakwetu urahibu ya kumsogelea huyu mama jiunamjia mithili ya mlevi ambaye hajakunywa pombe kwa mwezi mmoja.Hapa akamuta huyu mama akamsalimu na kumpa shikamoo mama akaiitikia.

Mwanakwetu hodari sana wa maneno akaongea na huyu mama hadi akasema kuwa anatokea shule katika shauri ya binti yake na kosa walilofanya bwenini na huku mama huyu akitaja adhabu waliyopewa binti.

Mwanakwetu akamuuliza mama huyu je Binti yako anaitwa nani ? Mama huyu akajibu kuwa binti yake anaitwa Akwilina Aqunata Koliwaka wa kidato cha nne. Mwanakwetu akamkumbuka huku akisema binti yako ni mpole sana, mtulivu mwenye aibu na adabu.

Mwanakwetu hodari wa maswali kwa mtu anayempenda huku akiwa mvivu wa maswali kwa mtu aliyemchukiza, mama huyu aliyajibu maswali yote:

“Sisi ni Wangoni wa Songea, Mume wangu ni Askari Mstaafu wa JWTZ, amefanya kazi maeneo mbalimbali ya Tanzania, kwa sasa anafanya kazi na Jimbo Katoliki la Iringa huku Parokiani na ndiyo maana tupo huku. Unajua mwalimu familia za wanajeshi zinazunguka sana, usipokuwa makini unaweza ukapotelea mikoa ya watu. Nimekaa maeneo mengi hata hawa wanangu hawajazaliwa huku, Mwalimu karibu sana nyumbani kwetu.”

Mwanakwetu akaongozana na mama huyu hadi stendi na kufika hapo, mama huyu hadi akapata usafiri awali akisema kuwa anaelekea Migori ndipo anapoishi na familia yake.

Mwanakwetu alikaa hadi gari lilipofika kisha mama huyu alipopanda ndipo na yeye akarudi zake kwake,

Kuanzia siku zilizofuata Mwanakwetu akawa anatumia majina haya: Akwilina , Aqunata, Koliwaka na Wangoni wa Songea katika kutunga sentensi katika masomo yake mawili aliyokuwa anafundisha iwe Kiingereza au Kiswahili katika sarufi ya lugha hizo.

Jambo hili liliwashitua sana wanafunzi wa Isimani huku Mwanakwetu alikata shauri na kuwaambia kuwa alimpenda sana mama yake Akwilina maana kati ya wazazi waliokuja katika shauri la wanafunzi siku ile mama yake Akwilina alipendeza sana.

Huku wanafunzi wengi walitaka kujua Mwanakwetu njiani wakati anakutana na Mama wa Akwilina baada ya kufunga ofisini mbona kana kwamba mwalimu wao alikuwa anaficha jambo? Mwanakwetu hakulijibu swali hili kwa kina kwa wanafunzi wa kidato cha nne lakini alilijibu swali hili kwa kwa kina kwa wanafunzi wa kidato cha tatu ambapo kwanza walikuwa wachache:

“Jamani hakuna ninachoficha hayo niliyoyasimulia ndiyo mazungumzo yetu yalivyokuwa njiani.”

Mwanakwetu hadi leo kila anapomuona Akwilina Koliwaka katika mitandao ya kijamii kisa hiki huwa anakikumbuka sana.

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Msomaji wangu unaweza kusema Mwanakwetu alikuwa mbaguzi katika kundi la wazazi wale, hili siyo kweli bali ni namna huyu mama alivyopendeza tu alikuwa tofauti na wazazi wenzake na hilo lilifanya Mwanakwetu amkumbuke tu. Kumbuka katika kundi la watu yapo mambo kadhaa ambayo yanaweza kusababisha watu wakukumbuke ni ule utafauti tu lakini kwa ushauri wangu kumbuka huo utafauti wako uwe mzuri/uwe mwema

Katika makala haya Mwanakwetu hakuwasilimulia kwa kina wanafunzi wa Kidato cha nne mwaka wa 2005 kwa hoja moja tu kwa kuwa Akwilina alikuwa akisoma mle darasani.

Mwanakwetu upo?Kumbuka:

“Utafauti Wako Unaweza Kusababisha Watu Wakukumbuke.”

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257


 

 

0/Post a Comment/Comments