Ni Sega Igenge Ninayemfahamu?

 



Adeladius Makwega-MBAGALA

“Katika kujaribu kujenga kampuni inayodumu kwa muda mrefu, ni muhimu kuelewa sio tu jukumu muhimu ambalo uongozi unafanya katika kuathiri ubunifu wa shirika, bali pia athari ya jinsia katika ubunifu huu kwa hiyo utafiti huu umeonyesha wazi kwamba jinsia ina jukumu kubwa katika kuelezea ubunifu wa hatua kwa hatua (incremental innovation), ambao ni mojawapo tu ya vipimo vitatu vya ubunifu.”

Haya ni maelezo ya hitimisho ya nakala ya utafiti ya kuhitimu Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Biashara ya Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa kipengele ya 6.2 ukurasa 98 mwaka wa 2008 uliyopewa jina- Uongozi wa Mabadiliko na Ubunifu: Umuhimu Husika wa Jinsia uliyofanya na Sega Igenge ambaye Mwanakwetu alikuwa anamfahamu.

Utafiti huu unaeleza kuwa ulisimamiwa na Bi Kettie L. Chipeta ambaye alikuwa mhadhiri wa chuo hiki wakati huo.

Katika utafiti huu Sega Igenge anayataja majina yake mawili ambapo ni tofauti na wasomi wengi ambapo mara nyingi huyataja majina matatu.

Isitoshe ukurasa wake wa Shukrani Bi. Sega Igenge ametoa shukurani kwa watu kadhaa akiwamo mama yake mzazi Martha Peter Igenge na kaka zake ambao ni Deogratias, Raymond na Peter pia akaenda mbali kwa kuwataja dada zake ambao ni Maria, Salome na Leah kwa kumtia moyo wakati anasoma kuelekea kuhitimu masomo yake haya mwaka wa 2009.

 

Msomaji wangu nakuomba utambue kuwa kipindi hiki wakati Sega Igenge anasoma chuo hiki nayeye Mwanakwetu alikuwa anasoma na kwanza Shahada ya Sanaa ya Habari na baadaye Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Biashara hiyo hiyo aliyosoma Bi Sega Igenge.

Msomaji wangu naomba kwenda mbali zaidi Mwanakwetu alikuwa Mjumbe wa Kikao cha Taaluma ya Chuo Kikuu hiki na akitokea Serikali ya Wanachuo ambapo Mwanakwetu alikuwa Makamu wa Rais wa Serikali hii ya wanachuo mwaka wa 2007 hadi mapema 2008, hapa anakumbuka hata huyu Kettie L. Chipeta ambaye mara nyingi alikuwa anakaimu Mkuu Kitivo alikuwa akiingia katika vikao hivyo ambapo Makamu Mkuu wa Chuo alikuwa ni Profesa Niclous Bangu na Mkuu wa Chuo Msaidizi Taaluma alipokuwa Profesa Andolongwise Katule, hawa maprofea wote walikuwa na Maprofesa wa Sayansi.

Msomaji wangu unaweza kujiuliza huyu Mwanakwetu leo hii ana nini?

Hivi karibuni mitandao ya kijamii imesambaa Taarifa kuwa Kaka wa Humphrey Polepole Geogratias ametakwa kutekwa huko Sweden na kundi la watu 15 huku ikidaiwa kuwa kundi hili linaongozwa na mwanamke mmoja aliyetambuliwa kuwa majina mawili ambayo ni Sega Igenge.

Maelezo haya yametolewa na Bi Recho Dangwa huku akisema kuwa hawa jamaa walikutana na Deogratias Polepole mara mbili kisha kukimbia.

Tangu ilipotoka taarifa hii kumekuwa kimya Mwanakwetu hajasikia Sega Igenge mwenyewe kusema lolote na hata kukanusha kuwa yeye hayumo katika mambo haya mabaya.

Mwanakwetu anamkumbuka Sega Igenge wakati anasoma pale Tumaini Iringa ambaye alikuwa akisalimiana nayem kipindi hiki Mwanakwetu alikuwa kijana.

Sega Igenge alikuwa jirani mno na mama mmoja mke wa mhadhiri wa kozi ya Habari ambapo mara zote Sega Igenge na huyu mama walikuwa mithili ya mapacha huku Mwanakwetu akiwatania nawaona mapacha wawili:

 

Mwanakwetu anakumbuka haya:

“Sega Igenge alikuwa dada mmoja mrefu, mwili uliojengeka , mweusi anajiamini, mrembo, ambapo Mwanakwetu naungama wazi kuwa niliwahi kumchokoza dada huyu na alikuwa mkali mno na baadaye akisema kuwa ‘Makwega sasa umefunga ndoa, acha vurugu ukiendelea na fujo kwangu sitaona gharama kupamb abasi na kumfuata mkeo Tanga kumueleza vituko vyako kwangu.

Hili lilikiwa bakora kwa Mwanakwetu na tangu hapo Sega Igenge hakusumbuliwa tena na Mwanakwetu.”

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Sega Igenge nakuomba popote ulipo tafadahali ueleze ukweli wa haya yote yanayosambaa au yupo Sega Igenge mwingine?

Kwa hakika Sega Igenge kama niliyosema una ndugu zako, una rafiki zako lakini tupo akina Mwanakwetu ambao tunakupenda tangu siku nyingi, hizi tuhuma za watu kutaka kuteka mtu mmoja kutajwa ni mbaya tambua kuwa zinaweza kuleta balaa kwa wetu wengine ni vizuri kujibu hoja. 

 

Kwa hakika Sega Egenge popote ulipo nakuomba kipenzi jibu hii hoja ili nafsi yangu ipone.

Baada ya kutoka taarifa hii ya Recho Dangwa nilikumbuka maneno haya ambapo siku ya kwanza nakuona pale Chuoni m nilikusalimu na nilikuomba namba yako ya simu ukanipa na nilipokuuliza unafanya kazi wapi ? Ulinijibu kuwa unafanya kazi Hoteli ya Kitalii huko Zanzibar. Au kule Zanzibar hotelini ulihama?

Hapa nakumbuka maneno yako ya hitimsiho katika utafiti wako:

“…ni muhimu kuelewa sio tu jukumu muhimu ambalo uongozi unafanya katika kuathiri ubunifu wa shirika, bali pia athari ya jinsia katika ubunifu…”

Hapa Sega Igenge kama kweli hata wanawake wanashiriki mambo haya ya kutekana hili lina athari kwa jinsia ya kiume hili litafanya akina Mwanakwetu waogope hata kuwasalimu akina mama.

Mwanakwetu Upo?Kumbuka:

“Ni Sega Igenge ninayemjua?”

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

071769257











 

 

0/Post a Comment/Comments