Mbuyu Ukianguka Unaua na Miti Mingine Kando Yake

 




Adeladius Makwega-MBAGALA.

Machi 24, 2026 Wakazi wa Wilaya ya Lushoto wamemzika Mheshimiwa Lukas Shemndolwa aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Lushoto kwa vipindi vitatu mfululizo huku akifanya kazi na Wakurugenzi kadhaa.

Uongozi wa Mheshimwa Lukas Shemndolwa ambaye alikuwa mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mkulima maarufu wa mbogamgoga hapo Malindi na Lukuzi ulihitimshiwa rasmi mwishoni mwa  mwaka wa 2020 baada ya kushindwa kura za maoni CCM katika ngazi ya Kata ya Malindi na hivyo hakuwa mgombea wa udiwani wa CCM katika Uchaguzi wa Mkuu wa mwaka wa 2020.

Kwa kuwa Mwanakwetu alifanya kazi katika Halmashauri ya Lushoto kati ya mwaka wa 2016-2018 na baadaye kuhamishiwa Wilayani Mbozi Agosti 15, 2018, siku ya leo anaomba alitazame jambo moja muhimu katika uongozi  hasa ngazi ya Halmashauri ya Lushoto huku akimtazama mzee wake marehemu Lukas Shemndolwa hasa nyakati zake ngumu.

Kwa hakika kazi moja nzuri iliyofanywa na Lukas Shemndolwa katika Halmashauri ya Lushoto yenye majimbo mawili Mlalo na Lushoto ilikuwa ni kufanikishwa mashamba ya Mkonge kutoka kwa wamiliki wa zamani ambao walikuwa yanasuasua na mashamba hayo kupata mwekezaji mpya hasa lile Shamba la Mkonge la Mnazi.

Kazi hii ilifanywa vizuri sana na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya marehemu Rais John Pombe Magufuli na Waziri wake mahiri wa Ardhi mheshimiwa William Lukuvi, huku kwa mkoa wa Tanga zoezi hili lilisimamiwa kwa Karibu na Martine Shigella na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga wakati huo Injinia Zena Said.

Kwa hakika Mwanakwetu akiwa Mkurugenzi wa Lushoto hapa alibaini kuwa zoezi hili lilikuwa gumu sana huku Baraza la Madiwani likigawanyika pande mbili, wapo waliopinga shamba kuuzwa na wapo waliotaka pesa zote za shamba zibaki Halmashauri ya Lushoto.

 

 

Maamuzi ya kuuzwa mashamba ya Mkonge na kuwapokonywa wawekezaji waliokuwa goigoi yalipitisha katika Vikao vya Ushauri vya Mkoa wa Tanga vilivyotanguliwa na vikao vya ushauri vya wilaya kadhaa za mkoa wa Tanga vilivyotangulia  chini ya Serikali ya Awamu ya Nne Uongozi wa Jakaya Kikwete nadhani hili aliyekuwa Mkuu wa Wiaya ya Lushoto wakati huo Alhaji Majid Mwanga analifahamu hii vizuri, hivyo basi Rais John Magufuli alikuja kuridhia maombi hayo na kusimamia utekezaji wake.

“Shamba likatangaza kuuzwa katika tenda ya Kimataifa, nadhani walipatikana wateja watatu lakini chini ya kiwango, hata ilipotangazwa tena hakupatikana mnunuzi, maamuzi yalifanyika na yule alikuwa na kiwango juu katika wale watatu wa kiwango chini alichaguliwa maana Heri ya Nusu Shari Kuliko Shari Kamili na taratibu za malipo zikawa zinafanyika.”

Msomaji wangu naomba utambue kuwa Mkoa wa Tanga ulikuwa umezerota mno kutokana na mashamba mengi ya Mkonge kutofanya uzalishaji au uzalishaji wa kiwang cha chini na ndiyo maana wasanii wa Bongo Fleva Mgosi na Mkoloni wakaimba Kunani Kule Tanga ?

Hapa serikali ilikuwa inajibu huu wimbo kwa kufufua mkoa wa Tanga, sasa japokuwa bei ya Mkonge juu katika Soko la dunia maamuzi ya Serikali ya kutafuta wawekezaji wapya Mwanakwetu anakubaliana nayo mia kwa mia, yalikuwa sahihi na yanapaswa kupongeza maana shabaha ilikuwa ni kuupa uhai Mkoa wa Tanga na mikoa jirani na Tanzania kujipatia pesa za kigeni.

 

Katika hizi harakati Mwanakwetu Mkurugenzi Mtendaji huku watumishi wa Halmashauri ya Lushoto walifanya kazi katika mazingira magumu sana kukiwa na vikao vingi.

“Naomba ifahamike kuwa kuuzwa shamba la Bilioni 2.8 ni pesa nyingi lakini mtu aliyekuwa mmiliki awali ni tajiri anapokonywa, hilo siyo jambo jepesi, linaleta maneno, watumishi wanaweza hata kuuwawa na hata madiwani wanaweza hata kutembelewa na tajiri wa awali kuomba asaidiwe abaki kuwa mmiliki wa shamba hilo. Hapa msipokuwa makini tajiri hawezi kukubali afe mwenyewe lazima afe na watu wengine-Mbuyu Ukianguka Unaua na Miti Mingine Kando Yake?

Tajiri mmiliki wa awali wa shamba a Mkonge ambaye alikuwa raia wa Kenya aliapa mbele yangu akasema atahakikisha Mwanakwetu anaondolewa Ukurugenzi- Mwanakwetu alicheka na kuachana naye.

Madhaifu ya CCM ni haya mtu anakuwa diwani, ukifika wakati wa uchaguzi anashindwa kura za maoni, pengine amekuja tajiri mwenye uwezo wa kuhonga zaidi yake, huyu anashindwa uchaguzi hapati muda wa kuketi na mwenzake kuongea na kuelezana mambo yalivyo, hapa CCM inapata mgombea mpya, mawazo mapya huku mawazo haya yanaweza kusimamiwa sana na mtu aliyemsaidia diwani huyo kushinda uchaguzi hawa matajiri, huyu diwani mpya akifika Halmashauri hatuwezi tambua pengine kaingizwa na matajiri wenye maslahi yao, hapa sasa michakao kadhaa ya Serikali inaweza kushikwa shati na kurudishwa nyuma, wananchi wanateska na kuyumbishwa na watu wema wanayumbishwa.Mwenye pesa anagharamia analolitaka  na mkono mtupu haulambwi.

 

Mungu bahati Viongozi wa Serikali ya awamu ta Tano walikuwa wakali walilisimamia hili hadi mwisho.

Katika hili nakumbuka maneno haya aliyasema Martine Shigella ofisini kwake na meza yake ikizungukwa na baadhi ya wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Lushoto (ambao wapo hai hadi leo hii), Mkurugenzi Mtendaji na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Lushoto Mheshmiwa Lukas Shemndolwa:

“Mwenyekiti wa Halmashauri ya Lushoto, hili jambo naomba lifahamike hivi Serikali inapofuta umiliki wa awali wa shamba na kuliuza , yule mmliki wa awali zipo stahiki zake ikiwamo uwekezaji wake alioufanya katika shamba hilo, pia kiasi cha fedha kinalipa madeni anayodaiwa na watumishi/vibarua hadi wazabuni.

Hii pesa inayosalia ndiyo inakwenda Serikalini hii ndiyo haki ya Watanzania wote siyo Wilaya yenu tu , kama ilivyo kwa ardhi zenye madini na rasilimali zingine

lakini kama Halmashauri inahitaji pesa hizo rudini katika vikao vyenu muombe kiasi cha fedha kwa matumizi yanayohusiana na ardhi tu mtapewa na siyo kulipana posho ya vikao.”

Lukas Shemndolwa akaungama mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga hili jambo lipo chini ya uwezo wangu nitalieleza vizuri Baraza la Madiwani. Hili lilifanyika na Baraza la Madiwani waliambiwa vizuri tu.

 

 

Hili lilifanyika na pesa hiyo kuombwa na halmashauri kuruhusiwa kutumia baadaye na baada tu ya barua hii kufika Agost 15, 2018 Mwanakwetu alihamishiwa Halmashauri ya Mbozi nakuagana na Mwenyekiti wake mheshimiwa Lukas Shemndolwa, huku kazi ilikuwa imekamilika mwekezaji mpya alianza kuwekeza huku Kijiji cha Mnazi kilianza kufufuka, mkong kulimwa kwa wingi

Baadaye Mwaanakwetu alikuja kubaini kuwa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto liliwafukuza kazi watumshi watatu : Rehema Sadiki-Afisa Ardhi na Kaimu Afisa Sheria wa Halmashauri hii, Renatus Mutasiwa Mweka Hazina wa Halmashauri hii na Deogratias Lyampawe ambaye alikuwa Mkuu wa Kitengo Manunuzi.

Mwanakwetu baadaye aliwasiliana na Lukas Shemndolwa na kuuliza mwenyekiti haya maamuzi yenu yalikuwa sahihi? Unajua kuwa zoezi hili lilikuwa gumu? Shida ilikuwa ni kweni nyinyi madiwani tena mmefanya nini mzee wangu?

Lukas Shemndolwa alimjibu Mwanakwetu kwa maneno haya:

“Makwega alikuja Waziri Mdogo wa TAMISEMI mheshimiwa Mwita Waitara aliongea maneno kadhaa, hapa nipo mwenyewe , nakosa nguvu, huku baadhi ya wapinzani wangu wa kisiasa wametumia karata ya kuuzwa kwa shamba hili kama karata ya kunidondosha kisiasa na hili .”

Mwanakwetu akamwambia maneno haya:

“Huyo mheshimiwa Mwita Waitara ni sawa ni Waziri Mdogo wa TAMISEMI lakini alikuwepo wakati RCC inakaa? Alikuwepo wakati changamoto hizo zinatokea? Lazima viongozi tuwe na uelewa wa pamoja katika mambo ya umma.

Hitilafu katika mambo ya umma zipo nyingi tu, iwe za kisheria na hatua zingine lakini itilafu zinapotokea zituongeze siyo kuumizana bali kuzuia hitilafu hizo zisijirudie.

Binafsi nasema wazi kuwafukuza Rehema Sadiki, Deogratias Lyampawe na Renatus Mutasiwa haukuwa uamuzi sahihi na isitoshe hawa wote walikuwa watumishi ambao ni peshenable. Sisi kama Serikali tunapata nini katika maamuzi kama haya?

Mzee wangu Lukas binafsi nakumbuka nilipokuwa nasoma sekondari wakuu wa shule walikuwa hodari sana wa kuwafukuza sana watoto wa watu shuleni.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati huo  marehemu Ditopile Ramadhan Mzuzuri alimwambia maneno haya Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Tambaza Ndugu Wajimila—Hivi Tulijenga haya majengo kuja kuwafukuza watoto wa watu? Tulidai Uhuru wa Tanganyika ili tukae sisi kisha tufukuzane? Haya maneno yalisema nayasikia kwa masikio yangu. Mzee wangu Lukas nakumbuka Mwalimu Wajimila alikaa kimya kisha Ibrahimu Raha(Mzee Jongo) akamwambia mwalimu Wajimila omba msamaha, Wajimila aliomba msamaha…

Ditopile akasema makosa mengine ni hitilafu za kibindamu-Ibrahimu Raha akasema –Mtoto Akiunyea Mkono Usiukate, nyinyi mngekatwa mikono mgekuwa walimu?

Mheshimiwa Shemndolwa hili alipo sahihi. Serikalini makosa yapo mengi lakini hitilafu hizo zisiwe chanzo cha kuumizana , nasema wazi wale ndugu yaani Binti Sadiki, Mutasiwa na Lyampawe walipaswa kupongezwa kufanikisha zoezi hili la kuuzwa shamba aua jamaa wa Kenya aliwapa kitu kidogo?.”

Tangu siku hii Mwanakwetu hakuwasiliana na Mheshiwa Lukas Shemndolwa hadi aliposikia amefariki Machi 2026.

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Kwa hakika Lukas Shemndolwa amefariki nakuzikwa kwao Malindi Lushoto Mkoani Tanga.

Kwa hakika katika utendaji wa kazi wowote ule hitilafu zipo kwa watumishi wa umma na hata kwa wanasiasa iwe Madiwani, Wabunge na hata Rais

Hata hayo mashauri yanayopelekwa mahakamani ni utaratibu tuliyorithi kutoka kwa mzungu tu . Siyo kweli mahakama ina hakia mia kwa mia. Swali ni je huku mahakamani hakuna malalamiko? Hakuna makosa? Makosa yapo mengi au Jaji huwa hakosii? Zile rufaa zinafanya kazi gani?

Lukas Shemndolwa yake ameyamaliza lakini sisi tuliyobaki tunajifunza nini? Ndiyo Lukas alishindwa kura za maoni mwaka 2020 Mwanakwetu anaamini Mkeya aliweka mkono wake. Je CCM Taifa inalifahamu hili? Serikali inalijua hili? Lukas alishindwa na hakuwa diwani na hakuwa tena Mwenyekiti wa Halmashauri, sisi tunajifunza nini?Kikubwa tuachane na maslahi binafsi tujali, maslahi ya wengu ambao ndiyo umma wa Watanzania. Madhaifu yapo lakini tukae tuvumiliane hakuna aliyekamilika.

Mwanakwetu Upo? Kumbuka:

Mbuyu Ukianguka Unaua na Miti Mingine Kando Yake.”

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

071769257














 

 

 


 

 

0/Post a Comment/Comments