
Adeladius Makwega-MBAGALA
Wanamichezo kadhaa kutoka Wilaya ya Magu mkoani Mwanza wamefanya ziara ya kimichezo Mkoani Kagera na kushiriki katika michezo kadhaa ikiwa ni ziara ya kujenga udugu baina yao kati ya Machi 26 na 28, 2026 huku Wilaya ya Magu ikishinda michezo yote.
Haya yamebainika katika viunga vya Manispaa ya Bukoba ambapo basi lililokuwa na maandishi makubwa Chama cha Walimu Magu lilionekana mitaani ambapo kundi la wanamichezo hao pia walionekana wakitoka kiwanja kimoja hadi kingine huku wakishirki michezo kadhaa.
Haya ni ya ndani ya siku tatu mfululizo Machi 26, 27 na 28, 2026 hapa Bukoba.
Katika viwanja kadhaa ambapo Manispaa ya Bukoba iliambulia patupu huku ikicheza viwanja vya nyumbani.
“Katika kuvuta Kamba Magu ilishinda mara mbili huku Bukoba Manispaa haikuambulia kitu, Katika mchezo wa mpira wa miguu Manispaa ya Bukoba ilipata sufuli huku Magu ikipachikia kimiani mabao matatu, hata katika mpira wa mikono Manispaa ya Bukoba ilipata magoli 14 nao Magu walipata magoli 24.”
Katika hali ya kusikikitisha mno hata ushangiliaji timu kutoka Wilaya ya Magu ilikuwa na washangiliaji wazuri, waliochangamka huku Manispaa ya Bukoba walikuwa wanyonge japokuwa walikuwa katika viwanja vya nyumbani.
Wakizungumza mara baada ya ushindi huo viongozi wa Timu ya Wilaya ya Magu mmojawapo wa viongozi wake wa hamasa Bahati John alisema kuwa kwa pamoja wana furaha kwa kujipatia ushindi huo lakini kikubwa ni kujenga udugu na siyo kujenga utenganishi baina yao:
“Ni kweli tumeshinda michezo yote lakini kikubwa sasa hivi mimi nikija Bukoba tena sintokuwa mgeni ,nimepata wenyeji wengi ukitegemea Mwanza, Kagera na hata Mara ni mikoa jirani ni mikoa ndugu.”
Kwa upande wake mwalimu Maimuna Hamisi ambaye alikuwa miongoni mwa washangiliaji kutoka Manispaa ya Bukoba alisema kuwa ni kweli wamepoteza michezo yote lakini hivyo ndivyo michezo ilivyo :
“Tutajipanga vizuri na sisi tutakwenda Magu na hakika tutashinda nadhani wenzetu walituzidi ujanja tu labda walikuwa na fisi wa Kisukuma waliwaongezea nguvu.”
Mwanakwetu upo?Kumbuka:
“Magu yaidhoofisha Bukoba.”
Nakutakia siku njema.
0717649257




.gif)
.gif)
Post a Comment