Kushiriki na Kunyamazia Utekaji Ni Kuhatarisha Kipambavu Usalama wa Ndugu Zako Mwenyewe

 


 

Adeladius Makwega-MBAGALA.

Suala la watu kadhaa kutekwa na hata watu kutaka kumtekwa kaka wa Humphrey Polepole huku ughaibuni Mwanakwetu amelichukulia umakini mkubwa, kwa maana familia ya Polepole hadi sasa imeshaumizwa na watekaji na familia nyingi za Watanzania zinalia kilio hiki hiki, machozi yale yale,nani wa kuwafuta machozi? Huku familia ya Polepole haiwezi kukaa kimya, ikiwa ndugu yao hajulikani alipo, Watanzania wenye mapema mema hawewzi kukaa kimya, lazima waseme na iwevyo na iwe, ama zao ama zetu tupambane ili mustakabali wa Polepole upatikane na huu ushenzi wa watu wabaya wanaotaka kumfanyia Kaka wa Humphrey Polepole lazima kupambana nao, kwa udi na uvumba ili usitokee na hata Humphrey apatikane iwe hai na hata mfu.

Jambo la kusikitikisha ni moja tu japokuwa Tanzania kuna vyombo vya dola inaonekana dhahiri vimeonesha ugoigoi.

Mwanakwetu anaona kuwa huu ugoigoi ni hatari sana kwa wale ambao majina yao yameshika nafasi kama Waziri Ulinzi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Viongozi vya vyombo hivyo wakati matukio haya yanatokea tangu ngazi ya Taifa, mkoa, wilaya,tarafa na kata.

Katika hili msomaji wangu naomba niende mbali zaidi hadi katika zile Kamati za Ulinzi na Usalama za Vijiji/Mitaa, Je msomaji wangu unazijua kamati hizi?

“Inawezekana ukaishi kijijini/mtaani lakini usifahamu kuwa ipo Kamati ya Ulinzi na Usalama ya eneo hilo ambalo inawajua watu wema na wabaya iwe Kijijini au Mtaani na lazima kamati hii itajua kilichotokea eneo lao kama kuna jambo baya au zuri wanapotakiwa kulielezea.”

Kwa hiyo tangu kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania kule ngazi ya Kitaifa hadi ngazi ya kijiji/ mtaa wapo ndugu zetu wanaofahamu mengi kwa mamlaka tunayowapa kisheria.

 

Kwa hakika iwe leo, iwe kesho na hata kesho kutwa Watanzania wanao watu kadhaa wa kuwauliza maswali na kisha maswali hayo kujibiwa tangu ngazi ya Kijiji/ Mtaa hadi Taifa labda Mwenyeenzi Mungu kwa maamuzi yake ndugu hawa awachukue awapeleke huku mbali nasi wakati tunaulizana majibu lakini hata huku kwake Mwenyeezi Mungu kuna maswali ni heri maswali na majibu ya hapa duniani.

Watanzania tuna udhaifu mmoja mbaya sana huwa ni hodari sana wa kupokea vyeo na matunda yake mazuri ya vyeo hivyo, kwa mikono miwili lakini kuwajibika katika haya yote pale balaa likija mioyo yote inakuwa na matende mithili ya mtu anayeugua ugonjwa na mabusha.

Kwa hakika kwa sasa Watanzania wameshuhudia utekaji wa Watanzania ndani ya nchi na hata wale Watanzania waliotekwa ughaibuni yaani nje ya mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Jambo la kusikitisha ni moja tu mazoezi haya haramu mara zote yamegonga mwamba nje ya mipaka ya Tanzania:

“Rejea kutekwa kwa Maria Sarungi Tsehal na baadaye kuokolewa na Vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Kenya-Januari 12, 2025, rejea kutekwa kwa Hamza Mshabaha huku Machakosi Februari 22, 2026 ambapo jaribio hili liligonga mwamba kwa Vyombo vya Usalama vya Kenya vikawakamata watuhumiwa wa utekaji huo wakijumuisha Wakenya na Watanzania na tamati ndugu hawa kufikishwa mahakamani.

Jambo la kushangaza ni moja utekaji wa Maria saerungi Tsehal ulifanyika miezi ya mwanzoni yam waka 2025 na hata utekaji wa Hamza Msabaha ni miezi ya mwanzoni ya mwaka wa 2026. Je mimi na wewe tunajua nani yupo katika orodha ya kutekwa hapo mbeleni? ”

Kwa wale ndugu zangu waliosoma sheria naomba niwakumbushe kitu kinachoitwa Igizo la Mahakama-MUTE COURT.

 

Mathalani tupo mahakamani Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Mstaafu ambaye matukio haya yametokea kipindi akiwa anaongoza taasisi hii, mathalani kapelekwa mahakamani anaulizwa swali mbele ya Jaji .

“Haya matukio ya utekaji yaliyofanyika ndani ya Ardhi ya Tanzania na hata nje ya mipaka na mifano yapo tele, takwimu zinaonesha hilo swali kwako ni je kwanini matukio ya utekaji mengi yaliyofanyika ndani ya ardhi ya Tanzania yanaonekana yanafanikiwa bila kuonekana kizingiti chochote wakati wewe ulikuwa na jukumu hilo la kuweka vingiti, kupambana na watekaji na pia kufanya uchunguzi na wahusika kukamatwa na kufikisha Mahakamani?”

Msomaji wangu tambua kuwa Mwanakwetu hajasoma sheria lakini ameshuhudia ndugu zake kadhaa wakisoma sheria, kwa wale walimu wa sheria naomba fanyeni Mute Court kisha naombeni mnitumie mwenendo wa shauri hilo utakavyokuwa hadi uamuzi katika igizo hilo na Mwanakwetu atachapisha igizo hilo. Hapa ukizingatia Sheria ya Makosa ya Jinai ya Tanzania.

 

Kwa hakika hoja za tuhuma za kutajwa jina la Sega Igenge kuwa ndiye kiongozi wa Genge la Watekaji huko Ughaibuni imempa tafakari kubwa Mwanakwetu na akawa anajiuliza mambo mengi:

“Sega Igenge aliniambia kuwa anafanya kazi Hoteli ya Kitalii huku Zanzibar. Je hili jibu ilikuwa danganya toto kula kunde mbichi? Sega Igenge wakati anasoma Tumaini Iringa alikuwa anapatikana katika mitando ya kijamii ilikuwaje apotee gafla baada ya kuhitimu mafunzo yake ya Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Biashar? Vijana wengi wa Kitanzania wanapomaliza shahada ya kwanza huwa baada ya miaka miwili kazini wanasoma shahada ya uzamili hasa wakiwa na ajira za Serikalini maana elimu hii hutumika kupanda ngazi ya mshahara. Ni mara chache sana watumishi wa taasisi binafsi kama vile mikahawa, hoteli, kumbi za starehe, makasino kuitaka elimu ya Shahada ya Uzamili na hata Shahada ya Uzamivu labda kwa wale wanafanya kazi katika taasisi za Elimu mathalani vyuo vikuu. Swali ni Je Bi Sega Igenge alikuwa mtumishi wa umma au binafsi? Kama umma je ni kweli alitaka kuitumia elimu hii kupanda ngazi ya mshahara? Au nyuma ya pazia kulikuwa na nini? Haya ni maswali ambayo Mwanakwetu anajiuliza.”

Ukisoma utafiti wa Sega Igenge ule wa Shahada ya Uzamivu wenye jina Uongozi wa Mabadiliko na  Ubunifu: Umuhimu Husika wa Jinsia kurasa za awali hususani ukurasa wa nne ya kirumi anasema meneno haya:

“Napenda kuishukuru sana familia ya A. Maseko kwa kuwa wema na wakarimu kwangu na kunitia moyo wakati nakusanya takwimu za utafiti huu, namshukuru sana Bi Stella Maseko kwa kuwa nami kila asubuhi nilipokuwa nakwenda kukusaya takwimu.”

Katika ukurasa huo huo aya iliyotangulia Bi.Sega Igenge aliyasema haya:

“Namshukuru sana rafiki yangu wa Uholanzi Erwin Lami na Angelique Van Egmond kwa moyo wenu endelevu wa kunisaidia…mlikuwa tayari muda wote kunisaidia… Pia nawashukuru sana wahadhili kadhaa wa kozi ya Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Biashara ya Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa ambao ni  Ndugu Samweli Lupyana, Dkt Norman Sigalla(Profesa sasa), Ndugu E Ugulumu, Dkt C. Chaturved, Dkt. Emmanuel Luvanda na Dkt S Mwakyambiki.”

Kwa hakika Sega Igenge ni mtu anayeishi, ni mtu aliyekuwa anakaa na watu katika hatua kadhaa na ndiyo Mwanakwetu anamshinikiza Sega Igenge ajibu hoja na atoke huko alipo na kukaa kimya ni hatari mno na kunaharibu jina zuri la familia yake ambayo ni familia ya Kikristo.

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

 

“Watekaji huwa wanaangalia ujirani baina ya taifa wanalotoka/kumchukua mtu muhusika alipo, hapa kunaweza kuwa na makubaliano kabisa ya kisheria kama vile ya kubadilishana wale wanaoaminika kuwa waharifu lakini pia zinaweza kutumia njia haramu kama vile kumteka na kumpitisha njia za panya, kumtia katika magari, ndege au meli huku aliyetekwa akipigwa hata sindano za dawa za usingizi kisha kumkifisha hadi anapotakiwa kufika. Kama hilo linakuwa gumu mtu huyu aliyetekwa anaweza hata kuuwawa huko huko katika zoezi hilo la utekaji.”

Kwa faida ya msomaji wangu unaweza kurejea mifano kadhaa katika mataifa haya ya Kenya na Tanzania:

“James Aggrey Bob Orengo mwanasiasa wa Kenya mwaka 1982 alikamatwa nchini Tanzania baada ya kukimbilia hapa akituhumiwa yeye na wenzake katika tuhuma za kuipindua serikali ya Daniel Moi, alikamatwa na kutiwa katika Land Rover hadi nchini Kenya na kukabidhiwa mikononi mwa Vyombo vya Usalama va Kenya.”

Hiki ni kisa cha kwanza na cha mfano lakini je kisa hiki chatosha la hasha vipo visa tele:

“Ni kweli tuliambiwa kuwa alilazimishwa kuingia ndani ya ndege na vyombo vya usalama vya Kenya ndani ya ndege ya KLM ya saa nne usiku na tumebaini kuwa alipandishwa humo kibabe na sasa anaelekea Canada na huu ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.”

Haya yanasema na Cliff Ombeta na Nelson Havi Februari 7, 2018 ambapo walikuwa mawakili wa Miguna wa Miguna mwanasiasa na wakili machachari wa Kenya ambapo Serikali ya Kenya ilimkata ndugu huyu na kumuingiza na kumbeba mzega mzega hadi ndani ya ndege na kurudisha Canada alipokuwa anaishi.

 

Kwa hakika yapo maandishi kadhaa yaliyopewa majina kama Sheria za Kimataifa na Sheria za Mataifa yaliyopewa Baraka na mabunge na vikao kadhaa na kuwa sheria halali za kupambana na utekaji na hata huu usafirishaji haramu wa binadamu.

“Cha kusikitisha matukio haya bado yanafanyika, hoja ya msingi ni wale wanaosimamia hizi Kanuni na hizo sheria wawe makini, kama mwenzako anatekwa wewe umekaa kimya, wewe umefumbata mikono au wewe unashiriki, wewe unaweza usitekwe kwa kuwa umewekewa ulinzi lakini mama yako, baba yako , mjomba wako, shangazi yako na hata mwanao amewekewa ulinzi kila pahala anapopita? Hata wewe unayetumwa kama wanaokutuma wakikugeuka utakuwa salama? Kwa hakika Kutoshughulikia utekaji ni kujiingiza kipambavu katika hatari ya kutekewa jamaa zako.”

Kwako Sega Igenge popote ulipo kumbuka maneno yako yale ndani ya ukurasa ule wa nne ya kirumi ya utafiti wako wa mwaka wa 2009 unayasema maneno haya:

“Napenda kuishukuru sana familia ya A. Maseko kwa kuwa wema na wakarimu kwangu na kunitia moyo wakati nakusanya takwimu za utafiti huu, namshukuru sana Bi Stella Maseko kwa kuwa nami kila asubuhi nilipokuwa nakwenda kukusaya takwimu.”

Kama wewe unayetumiwa na haya ni Sega Igenge ninayekujua na hizi tuhuma ni za kweli na ndiyo maana unakaa kimya, Je kama familia ya Maseko ingekufanyia ubaya mwaka wa 2008 na 2009 wakati wa utafiti je ungekuwa salama hadi sasa? Jitokeze ujibu hoja.

 

Mwanakwetu upo? Kumbuka:

“Kunyamazia Utekaji Ni Kuhatarisha Kipambavu Usalama wa Ndugu Zako Mwenyewe.”

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius @gmail.com

0717649257

 

 

 






















 

 

 

0/Post a Comment/Comments