Hodari wa Kupiga Pasi Ndefu

 

Adeladius Makwega MBAGALA.

Siku hii Mwanakwetu alikuwa Sirari wilayani Tarime, Mkoani Mara ambapo kulikuwa na shughuli za Maendeleo ya Jamii na kwa bahati mbaya katika kikao hiki timu ya Mwanakwetu hakiweza kupata chakula ambayo ilijumuisha Afisa Habari mmoja ambaye ni Mwanakwetu, dereva mmoja anayefahamika kama Chilongani na wanahabari watatu.

Kwa hiyo kuanza safari ya kurudi Musoma ilikuwa ngumu, hivyo basi ikaamulika waende kula chakula katika mkahawa mmoja, hiyo sasa ni saa 12. 30 ya jioni.

Awali siku hii kazi hizi za Habari walianzia Chuo Kikuu Sayansi na Tekinolojia ya Kilimo Butiama ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi alikuwa anakagua ujenzi wa taasisi hii ili kama ingeweza kuwapokea wanachuo wa mwaka wa kwanza 2025/2026

Kwa hiyo siku nzima timu ya Mwanakwetu hawakuweka kitu chochote tumboni na walipomaliza ndipo safari ya kwenda Sirari ilianza na kufika salama.

Msomaji wangu kumbuka shughuli ya Sirari imekamilika sasa wanakula chakula mkahawani, hapa kila mmoja kachagua meza yake, amekaa kando sehemu ambayo muziki hausikiki vizuri ili aongee na simu. Hapa hapa mara Mwanakwetu akasalimiwa na kijana mmoja mwembamba mrefu aliyevalia nguo za michezo.

“Kaka shikamoo? Unakuja hadi kwetu Sirari! Karibu sana Sirari. Shida yako Mwanakwetu haunyi pombe, ngoja nikulipie chakula na juisi ya boksi moja ili ilingane na bei ya bia tatu ninazokunywa mimi.”

Kijana huyu mwenye nguo za michezo akaagiza pombe yeye na mwenzake wakawa wanakunywa, huku anamtupia maneno kwa Mwanakwetu:

“Shida ya pili ya Mwanakwetu ipo katika taaluma yake, yeye ni mchezaji mzuri lakini anayependa kupiga pasi ndefu, hodari wa pasi za Kijerumani, Mwanakwetu pasi fupi hawezi.”

Jamaa kando wakawa wanacheka wakidhani kuwa Mwanakwetu huwa hali chakula cha mchana. Huyu jamaa akaendelea kusema:

“Tulimfuata tukamwambia mbona umeandika vizuri habari za Chuo cha Dodoma mbona za hawa jamaa haundiki? Mambo yale ya Dodoma na hapa ni yale yale, yaani chanda na pete. Wakati wa mitihani ukifika tunachangishwa fedha tunampelekea mhadhiri, kisha tunapewa mtihani yaani kama hauna, hilo limekula kwako. Labda uwe mnasaidia mhadhiri kusaisha mitihani au kwenda kwenye kazi zake.

Hivi unakumbuka nilikuja kukuomba shilingi 25,000 /- ile ilikuwa siyo kwamba sikuwa na fedha ya kula bali ilikuwa ya kukamilisha mikakati ya mitihani.”

Jamaa huyu anaongea huku watu wanakula chakula.

“Nasikia yule ni mwanafunzi wako wa Ndolela, Pawaga na huko Lilinga yeye alikuwa haoneshi mitihani, siku mitihani wake unafika hali ilikuwa tete, mwenyekiti wa kamati ya ufundi akakaa akasema jamani tunafanyaje?”

Wakati haya yanaendelea, mara akaja jamaa wa mkahawa kuchukua pesa kisha Mwanakwetu kusema ameshalipiwa. Jamaa yule mlevi akawa anaendelea kuongea akisema yaani tukashauriana tukusanye pesa kisha tukampa mtunzaji wa mitihani kupitia kwa hawala yake tuliyokuwa tunasomanaye, mitihani ule ukavuja.

Tukaufanya ila mwanafunzi wako alijua kuwa mtihani ule ulivuja, nasikia baadaye jamaa jamaa wale walivyo mafedhuli walikaa wakawa wanamgeuzia kibao kuwa mwanafunzi wako kavujisha mitihani, kumbe wamevujisha wao wenyewe. Jamaa huyu anaongea huku akiwa na ujasiri mkubwa kama anafahamu Mwanakwetu.

 

Jamaa huyu alimaliza kunywa bia zake kadhaa na kusimama kisha kuondoka zake huku Mwanakwetu na kundi lake la wanahabari na wao kuingia garini kurudi Musoma Mjini.

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Mwanakwetu baada ya kutoka hapa alikuwa na maswali mengi maana huyu jamaa alikuwa hamkumbuki huku Mwanakwetu ana wafunzi wengi ambao ni wahadhiri, wakufunzi , walimua mahakimu , majaji , waendesha mashtaka, madaktari, madereva, makarani, wakulima na wafugaji.

Mpaka sasa Mwanakwetu hajui je ni mwanafunzi wake huyo.

Mwanakwetu anampa pongezi Mwanafunzi wake huyu ambaye haoneshi mitihani yake kwa wanafunzi wake lakini moyoni bado anakereketwa kutaka kumjua Mwanafunzi wake huyu ni nani?

Mwanakwetu upo? Kumbuka:

“Hodari wa Kupiga Pasi Ndefu.”

Nakutakia Siku Njema

makwadeladius@gmail.com

0717649257

 

 

 

0/Post a Comment/Comments