
Wakristo wameambiwa kuwa kama walivyoingia Jumapili ya Matawi kwa shangwe kwa kumpokea Kristo wasiwe kama mayahudi walivyompokea kwa shangwe zote lakini wakakengeuka na matawi hayo ya miti hiyo ilitumika kumsubilisha . Haya yamesemwa na Frateli Justine Selestene Mapesa wa Jimbo Katoliki la Musoma katika ibada ya Jumapili ya Matawi Machi 29, 2026 Parokiani Mwisenga misa ya ibada ya pili.
“Tunapaswa kuwa na Kristo muda wote maishani mwetu, tusiwe vigeu geu”
Akihubiri katika ibada ya dominika hii Frateli Mapesa alisema:
“Mateso ya Yesu Kristo yana thamani kuwa ambayo yametupatia wanadamu ukombozi na hata Wakristo kuitwa Wakristo , mateso haya lazima kuyaenzi na kuyaheshimu huku kila mmoja ajitahidi kuacha dhambi, unapofanya dhambi unamtundika Yesu Msalabani na unamvisha taji la miba.”
Frateli Mapesa aliupigilia msumari wake wa mahuburi kwa kuvuka mipaka ya madhehebu ya Kikristo kwa kusema maneno haya:
“Wasabato wana wimbo unaoitwa NYUNDO ambao una teolojia nzuri sana ya Ukristo. Wimbo huu unazumngumzia jamaa mmoja ambaye anajengwa na dhana kama alikuwa kando siku Yesu anasurubiwa alipokuwa amesimama kando akatazama harakati za umati wakati wakimsulubu Bwana Yesu , Jamaa huyu akatazama mno kisha ndugu huyu akajiuliza ni nani aliyemtundika hapa Mfalme wa Amani? Baadaye ndugu huyu aligundua kuwa kazi yote hii imefanya na nyundo, baadaye huyu ndugu akasema kuwa aliyekuwa anafanya uharamia ule si mwingine bali yeye mwenyewe kutokana na maisha yake dhalimu, kutoka na na matendo yake ya dhambi. Jamani tuache dhambi.”
Awali akitoa maneno ya Utangulizi ya Ibada hii ya Misa Padri Julius Ogolla alisema kuwa katika maisha ya Kiafrika zipo sherehe nyingi ambapo watu wakiwa katika sherehe wanabeba matawi na kushangilia ushindi mathalani mkiibiwa ng’ombe kisha mkazitafuta na kuzipata wakati mnazirudishi zizini ni shangwe na hata kwa makabila yanayofanya tohara za wanaume kama kijana amekwenda kutahiriwa kisha hajalia wala kumshika mkono ngariba akitoka hapo kijana huyu, familia yake, ukoo na jamii nzima inashangilia na hata katika Ukristo tunaposali dominika ya Matawi tunamshangilia Yesu kama mshindi japokuwa mwanadamu ni kigeugeu.
Wakati haya yalikuwa ndani ya kuta za Kanisa la Tanzania hali ya hewa ya Mji wa Musoma ni nyuzi joto 26, unyevunyevu ni asilimia 0 na ujirani na mvua ni asilimia 53 na upepo ukivuma kwa KM 8 kwa saa.
Mwanakwetu upo ?Kumbuka:
“Dhambi Zetu Zinamtundika Tena Yesu Msalabani.”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257




.gif)

Post a Comment