Baba Naomba Kugombea Uongozi

 




Adeladius Makwega-MBAGALA

“Baba chuoni tunafanya uchaguzi wa Viongozi wa Wanachuo… natamani kugombea makamu wa Rais wa Wanachuo hapa DIDES fomu ni shilingi 10,000 natamani nigombee…Naomba ruhusa kugombea nafasi hiyo…”

Haya ni maelezo ya Mwanaisha Yusufu Binti Singano tarehe za mwishoni mwa mwezi Machi 2026 mwanafunzi wa Astashahada ya Maendeleo ya Jamii katika taasisi ya Mafunzo ya Maendeleo na Ujasiriamali Dodoma (DIDES) akiwasiliana na wazazi wake kuhusu mambo ya uchaguzi chuoni.

Wazazi walitoa kibali na binti yao kugombea nafasi hiyo na kisha kushinda kwa kishindo uchaguzini katika taasisi hii iliyosajiliwa na NACTVET ikiwa na hadhi ya ithibati.

 

Mwanaisha akiwa katika shamrashamra za ushindi aliwajulisha wazazi wake:

“Nimeshinda uchaguzi na sasa nimekula kiapo na nina majukumu ya kuwaongoza wezangu hapa DIDES Dodoma…”

Wazazi walimpongeza binti yao wakimtakia kila la heri katika nafasi hiyo.

Taasisi hii ipo katika Kata ya Nzuguni, umbali wa takriban kilomita 2 kutoka Kituo Kikuu cha Mabasi cha Dodoma.

Taasisi hii imesajiliwa kutoa mafunzo ya elimu ya ufundi katika ngazi ya Cheti na Stashahada ya Kawaida katika fani ya Maendeleo ya Jamii na Uzalishaji wa Kilimo. Pia, taasisi hutoa kozi fupi na semina kwa maafisa wa serikali pamoja na wafanyakazi wengine wa sekta binafsi na umma ili kuongeza ufanisi wao kazini. Aidha, taasisi ina dira ya kuanza kutoa shahada (Degree) katika siku zijazo.

Kwa kifupi Mwanaisha Yusufu Binti Singano anazaliwa katika Wilaya ya Lushoto iliyopo Kasikazini Mashariki mwa Tanzania.

Kwa desturi nchini Tanzania wanafunzi huwa wanachagua viongozi wao wakiwa katika vyuo vya kati na hata vyuo vikuu ili kuweza kujifunza uongozi tangu wakiwa wadogo.

Makala za Mwanakwetu zinampongeza Bi Mwanaisha Binti Singano kushinda nafasi hii katika ngazi ya vyuo vya kati.

Mwanakwetu upo? Kumbuka:

“Baba Naomba Kugombea Uongozi.”

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257







 

0/Post a Comment/Comments