Vua Sweta Lako

 







Adeladius Makwega-MBAGALA.

“Wewe Mwanakwetu vua sweta hilo jua kali sasa hivi. Unafuata nini huku ofisini kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara?”

Haya ni maneno kutoka kwa Karani wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara Bi Adventina Chacha akimsonda vidole Mwanakwetu mapema ya Februari 5, 2026 ambapo alikuwa kigulu na njia kuelekea Idara ya Afya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara inayoongozwa na Dkt. Zabron Masatu.

Mwanakwetu alipopigwa vijembe hivyo alicheka sana huku akijibu mapigo haya kwa tambo kadhaa zenye majivuno mengi:

“Sisi wenzenu tunakaa ghorofani viyoyozi kila kona, siyo nyinyi mnaokaa huku bondeni jua la kutoka juu linawapiga kama mlivyo hadi mnakuwa weupe kumbe weusi zaidi yangu.”

Mwanakwetu alipopigwa vijembe hivyo na Adventina vikamkera hivyo akaghairi kuingia ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara maana akumulikaye mchana usiku atakuunguza, hapa hapa mjivuni Mwanakwetu akachagua kuingia ofisini moja iliyo jirani naye .

“Haya jamani hodi hodi! Humu mnafanya kazi gani? Mbona vitabu vingi hivi vimepangwa mezani mithili ya vilele va Kibo na Mawezi va mlima Kilimanjaro?”

Mama mmoja akajibu kuwa hapa wamepokea vitabu tele katika dazani tatu kutoka Wizara ya Afya ya Tanzania :

“Menstrual Health And Hygiene Training of Trainers-Toolkit First Edition 2025 ambapo kurasa ya juu ina picha ya binti wa kike akiwa shuleni huku akibembea, naye mwalimu wake akisaidia ili abembee vizuri. Hapa picha hii ina maana kubwa kuwa mtoto wa kike kama akiwa katika hedhi yake na akapatiwa sodo kwa wakati akaivaa vizuri , mambo yatakuwa maridadi anaweza kushiriki michezo yoyote ile na hata kusoma atasoma kwa amani.”

Wakati mama huyu akimpa maelezo haya Mwanakwetu, gafla akaingia Mratibu wa Lishe Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara Bi .Grace Mgongorwa.

Kisha Bi Mgongorwa akasema:

“Dkt. Magreth Shaku hivi haya majarida yanakwenda lini huko halmashauri?”

Jibu likatolewa kuwa vitabu hivyo vinapakiwa hivi punde kwenda katika Halmashauri tisa za mkoa wa Mara ambazo ni Musoma Vijijini , Musoma Manispaa, Bunda Mji, Bunda Vijijini, Tarime Mji, Tarime Vijijini, Serengenti, Rorya na Butiama.

 

 

Dkt. Shaku akamuomba Bi Mngongora asubiri kwanza ili amueleze Mwanakwetu juu ya vitabu viwili vilivyosali katika ile dazeti tatu ya vitabu kutoka Wizara ya Afya:

“Kitabu cha pili kimepepewa jina Intergrating Menstrual Healh into Sexual and Reproductive Health Education and Service Delivery Tookit First Edition 2025- kava la juu la kitabu hiki inaonesha familia nzima imeketi huku ikijadaliana juu ya suala la afya ya uzazi ya mtoto wakike- shabaha hapa ni kwamba suala hili katika jamii zetu za kiafrika linaonekana kana kwamba jambo la siri , kufichaficha ni kubaya, hadi mabinti wakiogopa hata hedhi zao hadi sodo zao wakishazitumia wanazificha uvunguni chini ya vitanda, kisha baadaye wazifue na wazitumie mara ya pili ili linasababisha hadi magonjwa katika via va uzazi, ni hatari kubwa kiafya lazima tuvunje ukimya, haya mambo yanazungumzika.”

Dkt. Magreth Shaku aliendelea kueleza kitabu cha tatu na cha mwisho ambapo kilipewa jina National Menstrual Health And Haygene Guidelines ,First Edition 2025 ambapo kitabu hiki kinaonesha jamii mbalimbali lazima kuhusishwa na suala la afya ya uzazi, hata wenzetu wenye ulemavu, hatupaswi kuwatenga.

Dkt. Magreth Shaku alimalizia huku akisema kuwa yeye ni Kaimu Mratibu wa Elimu ya Afya kwa umma hapo Mkoani Mara.

Mwanakwetu akamuuliza sasa Dkt .Shaku mbona vitabu vyenu vyote vimeandikwa kwa kimombo? Dkt Shaku alijibu kuwa hivyo ni vitabu kwa wawezeshaji vinakuwa kama Kiongozi cha Mwalimu, ni kweli vipo kwa kimombo na wao wanajua Kiingereza lakini pia wanafahamu Kiswahili mambo yatakuwa mazuri sana tusiwe na shaka.

Gafla ulisikia mlio wa Toyota Land Cruza ikipiga honi pipii,pipiii pipiiii… alishuka dereva mmoja nduguye wa Chifu Kingalu Mwana Banzi wa Matombo Marogoro, ndugu Emmanuel Msimbe akisema jamani nimekuja kuchukua vitabu je vipo tayari? Alijibiwa vipo tayari, vilibebwa kimoja baada ya kingine na kupelekwa Wilayani.

 

Mwanakwetu aliagana na Dkt. Magreth Shaku na yeye kurudi alipotoka huku akiyakumbuka maneno ya yule karani wa RMO Bi Adventina Chacha

“Mwanakwetu Vua Sweta Lako.”

Mwanakwetu upo?

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257

 

 

0/Post a Comment/Comments