Adeladius Makwega MBAGALA.
Unapoutazama Utumishi wa Umma wa Tanzania ya leo unachekesha sana, japokuwa Tanzania imeongeza idadi kubwa ya wasomi wa kila nyanja swali la kujiuliza ni moja tu je hali ya Utumishi wa Umma imekuwa na tija yoyote?
Majibu ya swali hili la Mwanakwetu ndiyo yanajenga makala haya siku ya leo.
Kwa hali ya sasa ya Tanzania na kwa jicho la Mwanakwetu anaona Utumishi wa Umma umezungukwa na misitu miwili ambayo ni makaratasi na mifumo kadhaa ya tekinojia ambapo utendaji kazi ule wa kikarani ndiyo umepamba moto.
Tangu mkoloni Watanganyika walihangaika na makaratasi wewe hadi Tanganyika/Tanzania huru makaratasi yalishika hatamu. Mara baada ya miaka kadhaa Tanzania imepokea mifumo ya tekinolojia kadhaa sasa msitu mwingine umeingia bila Watanzania kukumbuka kuwa utaratibu wa kufanya kazi wa Mwafrika ulikuwa wa vitendo zaidi.
Mathalani leo unaweza kumuuliza mtumishi swali hili:
“Shekhe/ ustadhart siku ya leo umefanya kipi cha taaluma yako?”
Majibu mengi yanaweza kutolewa
“Mwingine anaweza kukujibu nimeandika dokezo A, nimeandika barua B, nimejaza katika mfumo C lakini ukikitafuta kitu kilichofanywa katika ulimwengu wa ushahidi katika ardhi hakuna kilichofanyika ni patupu kabisa.
Huu ukarani hauwezi kulikomboa taifa hili.
Kama mtumishi ni mwalimu wa Sekondari anafundiha Basic Mathematics tumkute darasa C anafundisha Martrix. Kama Mtumishi Z ni Bwana Shamba Tumkute shamba Z analikagua namna mkulima wake alivyoyapanda mahindi yake kwa kutumia mistari na kuweka mbolea, Kama Mtumshi Y ni Bwana Mfugo tumkute anamkagua Ng’ombe wa Bwana P katika zizi lake kijiji F . Kama Mwanakwetu ni Afisa Habari tuone katika kuwa wiki W ametuzalishia habari ngapi? Kwa ushahidi. Kama Musa ni Mtendaji wa Kijiji T tuone amefanya mikutano mingapi ya kuhimiza maendeleo kijijini na mikutano hiyo tuione inafanyika.
Kama Dkt.Grace Makwega ni dakitari wa Binadamu katika Hospitali ya Wilaya J kama yupo Kazini wodini Februari 11, 2026 ukifika Hospitalini unakuta anamtibu mgonjwa Z wodini.”
Kwa hali ilivyo sasa ya mifumo na makaratasi kila mmoja ni uhodari wa ukarani na hili linatupoteza.
Mathalani mtumishi A anakwenda likizo kuna haja gani ya kuyajaza mafumo mengi, katika mifumo, kuna haja gani ya kuandika barua tele, kama kweli likizo ni haki ya mtumishi ukarani wa karatasi na mifumo una maana gani?
“Bibi wewe unaenda likizo tarehe 1-29 nenda likizo haki yako ni hii mambo yanakuwa mepesi…”
Hoja ya barua nyingi ukiuliza unaweza kupewa majibu ili linafanyika ili kuondoa hoja za mkaguzi wa ndani na wa nje.Mkaguzi wa Ndani ni nani? Mkaguzi wa Nje ni nani? Huu ndiyo ule ule ukarani ambapo mzungu anatupoteza muda kwa miaka kadhaa katika karatasi na sasa anatupoteza muda katika mifumo.
“Swali ni je huyu mkaguzi wa ndani na nje kwani yeye hajui kuwa mtumishi ana haki ya kwenda likizo?Kwani isijaze karatasi moja tu mtumishi aweze kwenda likizo? Kwanini kunakuwa ni mirorongo mirefu ya makarani wengi badala ya watu kufanya kazi zao walizosome,a watu wamekuwa mabingwa kusaini makaratasi na nyaraka tu.Hili halikubaliki.”
Kwa hakika Mwanakwetu anashauri Watanzania tuache Ukarani iwe katika karatasi na iwe katika mifumo hauna maana hauwezi kuikomboa nchi hii.
“Mzungu katuletea karatasi tumehangaika nazo wewe miaka karibu karne nzima sasa bado tupo pale na sasa katuletea mifumo sasa tunahaingaika nayo wee Tanzania itahangika karne nzima tena, tunapoteza muda. Kila mmoja afanye kazi ya utaalamu wake ili maisha yawe mepesi.
Tusipokuwa makini tutapoteza tunaipoteza karne nyingine hivi hivi wakati wenzetu wazungu wao wanatazama kile mtu anachokizalisha baada ya kazi kwa kukiona kwa macho na siyo katika karatasi na mfumo.
Mwanakwetu upo ?Kumbuka
“Ukarani Hauwezi Kuiondoa Tanzania Katika Umasikini.”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257


.gif)
Post a Comment