Tumeanza Maandalizi ya Randama ya Bajeti

 






Adeladius Makwega

“Kwa sasa tunafanya maandalizi ya awali ya Vikao vya Bajeti ya mwaka wa fedha 2026-2027 lakini sasa kunafanyika maandalizi ya RANDAMA hii ya Bajeti, kwanza ili kufika huko tunaangalia namna tulivyotekeleza Bajeti inayokwenda kumalizika yaani ile ya 2025/ 2026 …Kisha hapo mbeleni ndipo tutaifikia ile Bajeti ya 2026/2027.”

Ni majira ya asubuhi ya Februari 9, 2026 Mwanakwetu anatembelea Ofisi ya Mkuu wa Sehemu ya Mipango na Uratibu, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara ndugu Emmanuel P. Mazengo akitoa maelezo yake kwa kazi wanazofanya kwa sasa:

“Katika kufanikisha kupatikana kwa taarifa nzuri ya utekelezaji tumekusanyika hapa pamoja na maafisa wote wa Divisheni ya Mipango, Waratibu wa Mikopo na Waweka Hazina kutoka Halmashauri zote tisa:Bunda Vijijini, Bunda Mji, Tarime Vijijini , Tarime Mji, Musoma Manispaa , Musoma Vijijini, Tarime Mji, Tarime Vijijini Butiama na Rorya ili kuiweka vizuri na kazi  hii itakamilika kwa juma zima.

Tukiwa wataalamu dazeni tatu kwa hakika tutakuja na taarifa nzuri na kuyapigiwa mfano.”

Alisisitiza Ndugu Mazengo.

Mwanakwetu alipotoka katika Ofisi hii ya Mpango na Uratibu ofisi hii katika korido la taasisi hii ya umma ameshuhudia shughuli kadhaa za Kiserikali zikiendelea kama kawaida hasa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara huku Katibu Tawala Mkoa wa Mara Mwalimu Gerald Musabila Kusaya akionekana akishiriki vikao vya siku hii hapa na pale na kuzungumza na watumishi na wegeni kadhaa wanaofika ofisini kwake.

 

Mgeni mmojawapo aliyenukuliwa katika kitabu cha wageni kwa siku hii ni Donald Bwire Masatu kutoka Shirika Lisilo la Kiserikali Gender and Public Health Organization (GPO).


 

Wakati haya yakiendelea hapa Musoma Mjini ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara hali ya hewa ya Mji wa Musoma ni nyuzi joto 24, unyevunyevu ni wa asilimia 50, ujirani na mvua ni wa asilimia 76 na upepo ukivuma kwa KM 8 Kwa saa.

Mwanakwetu Upo?

Kumbuka:

“Tumeanza Maandalizi ya Randama ya Bajeti.”

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257

 

0/Post a Comment/Comments