Adeladius Makwega-Musoma MARA
Haya yalikuwa majira asubuhi kukimbilia mchana wa Februari 26, 2026 hapa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara ambapo Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara , ambaye ni Afisa Tawala na Rasilimaliwatu ndugu Domicus Lusasi anapokea ugeni kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) unaongozwa na kiongozi kutoka tawi la Chuo hiki hapa Musoma Dkt. Anna Kyamba:
“Kiongozi kwa Niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) tumekuja kwako kuwatambulisha wageni kutoka Chuo Kikuu cha Ludwig Maximilian cha nchini Ujerumani maana Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kinaprogramu zake za kubadilishana ujuzi na wataalamu kwa hiyo hawa ndugu zetu wawili ni miongoni mwa wataalamu kutoka huko wamekuja nchini Tanzania hivi karibu kwa program hizi.”
Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara ndugu Lusasi aliwakaribisha wataalamu hawa ambapo Anna Sophewornznofr na Analina Etemi:
“Haya majina yenu ya kwanza ni mepesi lakini ili jina la ukoo la Sophewornznofr kwangu ni gumu, itabidi mnifundishe Kijerumani ili niweze kulitamka…Nami nitawafundisha Kiswahili…”
Alisema kwa utani ndugu Lusasi ofisini kwake. Ndugu Lusasi aliongeza kuwa anawakaribisha sana Tanzania na hususani Mkoani Mara. Huku anakaribisha kujifunza utamaduni, vyakula na mambo mengine mengi.
“Serikali ya Mkoa wa mara inatambua mchango mkubwa wa Chuo Kikuu Huria kwa Tanzania na Mkoa wa Mara na kwa kuwa Chuo Kikuu cha Ludowig ni rafiki wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania hata kwa Bi Anna na Bi Analina ni marafiki pia wa Mkoa wetu wa Mara. Karibuni sana Mkoa wa Mara.”
Awali wageni hawa kutoka Chuo Kikuu Huria walipokelewa na Dkt. Elpidius Baganda ambaye ni Afisa Elimu Mkoa Mara.
Baada ya mazungumzo haya mafupi ofisini ndipo ugeni huu ulipata wasaa wa kupiga picha kadhaa za pamoja na Katibu tawala Mkoa wa Mara.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
“Chuo Kikuu cha Ludwig Maximilian (LMU) ni chuo kikuu mashuhuri cha utafiti duniani kilichopo Munich, Ujerumani, kilichoanzishwa mwaka 1472.Kikiaminika kuwa mojawapo ya taasisi bora za elimu ya juu barani Ulaya na duniani kote, kikiwa na historia tajiri ya ubora wa kitaaluma na huku washindi kati ya tuzo 30-50 wa Tuzo ya Nobel miongoni mwao ni Ferenc Krausz aliyeshinda Tuzo ya Fizikia ya mwaka wa 2023 huku majina kadhaa ya wahitimu wa Chuo Kikuu hiki yakitajwa katika tuzo mbalimbali ulimwenguni.”
Mwanakwetu kwa makala haya anawakaribisha wasomi hawa wawili kutoka Ujerumani hapa Mkoani Mara na husasani nchini Tanzania.
“Nyinyi Pia ni Marafiki wa Mkoa wa Mara.”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257








Post a Comment