Nyanjage Kuwa Mkombozi wa Wilaya ya Rorya

Adeladius Makwega-RORYA.

“Taswira ya pikipiki kadhaa, huku watu wakipanda na kushuka katika vyombo kadhaa vya moto ikiwamo pikipiki, magari madogo na mabasi. Mazingira haya ni kichakani huku hekeheka zikionekana kuna jambo jirani linaendelea.”

Mwanakwetu anasogea kando na eneo hili huku akiomba dereva wa gari hii asimame ili ajue kuna ajali au la?

Mwanakwetu anashuka kisha anakutana na watu wawili, binti akiwa ameshika kifurushi na dumu la maji ambalo ni tupu na kijana juu akimgoja apande bodaboda.

Binti huyu kwa kumkadilia aliweza kuwa na miaka 19-20 akiwa ameshika bando la barabara linaloonesha daraja la Nyanjage lililopo Wilayani Rorya Mkoani Mara.

Mwanakwetu akaamuuliza huyu binti, hapa kuna nini?

“Hapa ni eneo la Nyanjage Wilayani Rorya, kumegundulika madini ya dhahabu hivyo tumekuja kuchangamkia fursa.”

Hekaheka zinaendelea, huku wanaoshuka katika vyombo vya usafiri wakiwa wanazungumza lugha mbalimbali, wengi wakiongea Kisukuma na wengine lugha ambazo Mwanakwetu hakuweza kuzifahamu, kelele za miungurumo ya magari na pikipiki zikilipamba eneo hili.

Mwanakwetu alipoelezwa ili aliingia ndani ya gari hadi kule alipokuwa anakwenda na aliporudi alitaka kufahamu kwa kina juu ya eneo la Nyajange je ni kweli kumegundulika madini?

 

Gambales Samson Panga ni Afisa wa Mkoa wa Mara anayesimamia Viwanda, Biashara na Uwekezaji aliungama kuwa ni kweli eneo ili kumegunduka madini ya dhahabu, huku eneo ili limeanza kuchangamka na huduma kadhaa zimeenza kutolewa.

“Nimefika eneo Nyanjage Februari 22, 2026 na baadhi ya watu wameshaanza kupata dhahabu ambapo futi kati ya 15 hadi 20 mkanda wa dhahabu unapatikana.”

Ndugu Gambalesi alisema kuwa eneo ili japokuwa neema hii imepatikana lakini kuna utapeli unafanyika wapo wajanja na wanauza mifuko inayodaiwa kuwa ina mchanga wenye dhahabu na mfuko huu mmoja unauzwa shilingi 10,000 hadi 15,000 ipo mifuko yenye mchanga wenye madini hata lakini ipo mifuko ambayo haina mchanga wenye madini haya, kikubwa umakini unatakiwa kila aliyepo katika shughuli hii awe na akili timamu.

Akizungumzia hali hii Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Rorya Wakili Msomi Abdul Omari Mtaka alisema:

“Eneo la Nyanjage ni mojawapo ya maeneo muhimu katika uwekezaji kwa sasa kwa madini kwa Halmashauri yetu ya wllaya ya Rorya ambapo kwa muda mrefu Wilaya ya Rorya imekuwa tu na wachimbaji madini wadogo wadogo. Kama hali ikiendelea hivi hivi tutaweza kuwa na mgodi mkubwa na sisi Halmashauri ya Wilaya tutakuwa na chanzo kipya, kikubwa cha mapato.Kikubwa Halmashauri yetu itatoa ushirikiano mkubwa kwa wananchi wa eneo hili.”

Kwa ujumla Mkoa wa Mara ni eneo lenye utajiri Mkubwa wa madini ya dhahabu huku maeneo kadhaa yakizidi kuonekana kuwa yana utajiri wa madini ya dhahabu.

Mwanakwetu Upo? Kumbuka:

 

“Nyanjage Kuwa Mkombozi wa Wilaya ya Rorya.”

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257

 















0/Post a Comment/Comments