
Adeladius Makwega MBAGALA.
Mwanakwetu anaingia katika viunga hivi ambavyo vilipambwa vizuri sana, huku akisema naam kweli leo tupo katika sherehe. Haya yalikuwa ni majira ya usiku wa Februari13 kuelekea Februari 14, mwaka wa 2026 Musoma Mjini ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Alfred Mtambi anazungumza na wafanyakazi wa Ofisi yake karika viunga vya ofisi hii hapa kando ya mlima Mukendo, huku watumishi kadhaa wa kutoka taasisi za umma na binafsi, viongozi kadhaa kama vile wakuu wa wilaya zote , Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zote tisa za mkoa wa Mara na watumishi wa ofisi hii wakiwa katika hafla fupi ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2026 na kuuwaga mwaka wa 2025 ambao ulikuwa mwaka wenye mengi ya kusimulia.
“Kuna mwanafalsafa mmoja wa masuala ya vita anaitwa Meja Jenerali Patton alisema kuwa unapokuwa katika uwanja wa vita lazima uhakikishe kila silaha iwe inasaidia kufanikisha ushindi wa vita kama isipokuwa hivyo huko itakuwa ni fujo na mwisho ni vigumu kushinda.Nawaomba watumishi wa Serikali katika Mkoa wa Mara tuendeleze ushirikiano wapo waliohama na wapo waliohamia, natambua mnafanyakazi kwa umoja hali hii iendelee ili tuwatumikie wananchi wa mkoa huu ambao wao ndiyo wenye mali.”
Kwa hakika mambo katika sherehe hayana hotuba ndefu haya ni maneno ya Kanali Mtambi akiongea na hadhara hii mara baada ya kukaribishwa na Katibu Tawala Mkoa wa Mara ndugu Gerald Musabila Kusaya. Shughuli iliendelea vizuri na huku Kanali Mtambi alishika usukani wa maelezo yake:
“Katika sherehe kama hizi kule jeshini huwa zinatolewa nafasi za watu kuzungumza juu ya hali ya dunia ilivyo, huku kila mmoja akiyasema yake mbele ya hadhara hiyo kulingana na maudhui aliyoyachagua iwe siasa, uchumi, vita na kadhalika. Naomba mimi leo niwapeleke kule jeshini na niseme hili-hivi karibuni Taifa la Marekani liliivamia Venezuela wakaingia katika kambi ya Kijeshi na kumnyakua Rais wa Maduro na kuondoka naye hadi Marekani. Makazi ya Rais huyu yalikuwa katika Kambi ya Jeshi iliyokuwa na watu karibu 5000 lakini hedikopta za Marekani kati ya tano hadi saba zikaenda kupenya na kupambana hadi kumchukua rais huyu na mkewe na kuondoka naye.
Siku hiyo umeme ulizimwa, vifaa vyote vya mawasiliano vilizima, watu walishindwa kuwasiliana, kila mmoja alikuwa anasikia kelele tu masikioni mwake, baada ya tukio hili la Januari 3, 2026 dunia ikawa njia panda nini kimetokea?
Je silaha gani zilitumika? Majuzi Rais Marekani Donald Trump aliondoa ukimya naye ye ana sifa moja kubwa na kutokuwa mficha siri akamwaga mtama katikati ya kuku wengi, alisema maneno haya silaha iliyotumika ni Discobomberbulete, silaha hii inafanya kazi kwa discobomberbulete na wale inaowashughulikia inafanya kazi wa kudiscobomberbuleted wakishakuwa discobomberbuleted ikishafanikisha zoezi ndipo wanaiondoa hiyo discobomberbuletion, jamani asanteni sana nawatakia hafla njema.”
Kumbuka msomaji wangu Mwanakwetu yu katika hafla hii na Mkuu wa Mkoa wa Mara ndiyo anamaliza kuongea na hitimisho lake lilikuwa juu ya Uvamizi wa Rais Donald Trump huku Venezuela tukio la Januari 3, 2026. Hapa hapa Mwanakwetu alitaka kujua kile kilichotokea Marekani baada ya Uvamizi ule Venezuela hali ilikuwaje?
“Hili ni jambo kubwa, kwanza ninashukuru kwa sisi sote kuwepo hapa, jana usiku na mapema ya leo kwa maelekezo yangu , Majeshi ya Marekani yalitekeleza Oparesheni ya kipekee ya kivita katika Mji Mkuu wa Venezuela yakitumia nguvu kubwa ya Kijeshi ya Marekani ya Angani , nchi kavu na baharini. Nguvu hii ilitumika kuanzisha shambulizi la hatari na ajabu na lilikuwa shambulizi ambalo dunia haijawahi kuliona tangu vita va vya pili vya dunia na ilikuwa ni shambulizi dhidi ya ngome ya kijeshi iliyokuwa imara sana katikati ya Caracas na kumleta Dikteta Nicolaus Maduro kwenye mikono ya haki na sheria, kwa hakika shambulio hili ni mojawapo ya mafanikio makubwa ya kijeshi ya taifa letu la Marekani.”
Haya ni maelezo ya Rais Donald Trump wa Marekani Januari 4, 2026 mara baada ya kufanikisha kumnyakua Rais Maduhu wa Venezuela. Kwa hakika Marekani imetoa maelezo kadhaa juu ya oparesheni hii ambayo imeibua maswali tele huku dunia imekuwa na shauku ya kilichofanyika Venezuela hata kufanyika maeneo mengine haya unaweza kuyaona katika maoni ndani ya mitandao ya kijamii kwa wasomaji wengi.
Marekani ikisema kuwa oparesheni zake kama hii zina tija sana na huu ni wajibu wao kwa Marekani na dunia kwa ujumla wake. Maswali ni mengi kama hizi oparesheni ni muhimu Je baada ya Venezuela Marekani itakwenda wapi? Kumnyakua nani?Je oparesheni hizi zitasitishwa na mwendo kuwa ni wa mazungumzo na diplomasia?
“Kama mlivyosikia Rais Trump akizungumza mara nyingi tunazungumzia amani kupitia nguvu. Katika Idara yetu ya Vita, tunajiona kama idara ya nguvu. Lakini pia tunahitaji kukumbuka kwamba tunapata nguvu zetu kupitia imani na kupitia ukweli na kupitia neno la Mungu. Kwa hiyo, hapa kuna somo kutoka Injili Takatifu kama ilivyoandikwa na Marko sura ya 8: Mstari wa 28 hadi 38.Neno la Bwana linasema: Yesu akaenda pamoja na wanafunzi wake hadi vijiji vya Kaisaria Filipi. na akiwa njiani akawauliza wanafunzi wake.‘Ati watu wanasema mimi ni nani?’Nao wakamwambia, ‘Yohana Mbatizaji; wengine wanasema Eliya; na wengine, mmoja wa manabii.’ Akawauliza, ‘Lakini ninyi mnasema mimini nani? Petro akamjibu ‘Wewe ndiwe Kristo.’ Akawaonya kwa ukali wasimwambie mtu yeyote habari zake. Akaanza kuwafundisha kwamba Mwana wa Adamu lazima ateseke mambo mengi, na kukataliwa na wazee nawakuu wa makuhani na waandishi, na kuuawa, na baada ya siku tatu kufufuka tena. Alisema hayo waziwazi. Petro akamvuta kando na kuanza kumkemea.Lakini Yesu akageuka na kuwaona wanafunzi wake, akamkemea Petro akisema.‘Ondoka mbele yangu, Shetani, kwa maana huwazi mambo ya Mungu bali ya wanadamu.’ Akawaita umati wa watu pamoja na wanafunzi wake akawaambia.‘Mtu yeyote akitaka kunifuata, ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake na anifuate. Kwa maana yeyote atakayetaka kuokoa maisha yake atayapoteza; lakini yeyote atakayepoteza maisha yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili atayaokoa.Kwa maana itamsaidia nini mtu kuupata ulimwengu wote na kuipoteza nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? Kwa maana yeyote atakayenionea aibu mimi na maneno yangu katika kizazi hiki cha uasherati na dhambi, Mwana wa Adamu naye atamwonea aibu atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.’
Hii ndiyo Injili ya Bwana Yesu Kristo, Neno la Bwana. Amina.Katika somo hili la Injili, tunamsikiaKristo akisema, ‘Chukua msalaba wakona unifuate.’ Ni wazi Kristo hakutumikatu kama mwanadiplomasia. Alikuwa pia mleta mabadiliko. Ujumbe wake ulikuwakutenganisha ukweli na uongo, mambo ya ulimwengu na mambo ya Mungu, nuru na giza, mema na mabaya na kama Kristo, kwa namna za kidunia, mashujaa wetu jasiri hawakuitwa kuuridhisha ulimwengu. Wanapaswa kuukabili. Tunajua tunapigana vita ya kimwili, lakini hatimaye imejikita, kama hali ilivyo sasa kama Rais Trump alivyosema, katika uwanja wa vita wa kiroho. Sisi si wapiganaji tu wenye silaha zauhuru, bali hatimaye tumevikwa silaha zaimani, na tumekuwa hivyo tangu mwanzo. Kama vile George Washington alipiga magoti kwenye theluji huko Valley Forge, akiomba mbinguni mwongozo na ulinzi, ndivyo mashujaa wetu wanavyofanya leo hii. Tunazungumzia 1776 na miaka 250, nani amewahi kufanya hivyo? Lakini katika, Idara ya Vita, sisi ni kama idara ya 1775 kidogo. Tunajua huwezi kuwa na uhuru wa 1776 bila kuwa tayari kupigana na kuutetea. Kwa hiyo, katika kusudi hilo, tunaishi kauli mbiu ya taifa letu kuu:
‘Kwa Mungu tunamwamini.’ Utayari wa kujitoa muhanga kwa ajili ya nchi yako huzaliwa katika jambo moja, imani ya kina na thabiti katika upendo wa Mungu kwetu na ahadi yake ya uzima wa milele. Maandiko yanasema.‘Kwa maana yeyote atakayetaka kuokoa maisha yake atayapoteza, na yeyote atakayepoteza maisha yake kwa ajili yangukwa Injili atayaokoa.’
Mwanajeshi yuko tayari kuyatoa maisha yake kwa ajili ya kikosi chake, nchiyake, na Muumba wake. Mwanajeshi huyo anapata uzima wa milele. Urithi wake hautakuwa wa hasara, bali wa utukufu kwa kusudi lililo kubwa kuliko yeye mwenyewe na ili kuhifadhi roho za Wamerikani, lazima tuendelee kushika si upanga wa kimwili tu, bali pia upanga wa ukweli—bila hofu wala aibu. Katika mapambano haya, lazima tukumbuke kila siku, hasa hasa katika mji huu, kwamba mamlaka yote, heshima yote, na utukufu wote ni wa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Kristo ni Mfalme na Mungu awabariki mashujaa wetu. Mungu alibariki taifa letu la Marekani.”
Haya ni maelezo ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth.
Msomaji wangu kumbuka Mwanakwetu alikuwa katika sherehe na haya alikuwa anayaona katika mtandao huku akipekua baada ya kumsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mara Februari 13, 2026 pale alivyomtaja Rais wa Marekani na uvamizi ule wa Venezuela. Mara baada ya sherehe hii kumalizika ndipo Mwanakwetu akarudi nyumbani kwake na kuyatayarisha makala haya unayoyasoma msomaji wangu.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Kwa hakika tangu uvamizi ule wa Venezuela na kunyakuliwa Rais Maduro ni karibu mwezi umepita na kauli ya Kanali Evans Alfred Mtambi ndiyo kauli ya juu kutamkwa hadharani ni Mtanzania mwenye wadhifa Serikalini na Jeshini juu ya uvamizi ule wa Marekani Venezuela.Kutoka na maelezo haya ya Kanali Mtambi ambaye ni mpiganaji wa JWTZ ndiyo maana Mwanakwetu aliamua kuyatayarisha makala haya huku Mwanakwetu akiamini kuwa oparesheni kama ile ya Venezuela inaweza kufanya na Marekani katika taifa lolote lile hivi sasa kwa sababu nyingi ikiwamo ni kufanikiwa kwa oparesheni ile ya Januari 3, 2026 lakini pia yale mashaka ya dunia katika oparesheni hii inafanya mataifa mengi kuwa na ganzi na hii kuzidi kuipa nguvu zaidi Marekani kufanya itakavyo na pia hata maelezo ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani yanaonesha kuwa sasa Marekani imechoka na vita vya maneno suluhu ni nguvu za kijeshi ambazo inazo:
“…Kristo hakutumika tu kama mwanadiplomasia. Alikuwa pia mleta mabadiliko. Ujumbe wake ulikuwakutenganisha ukweli na uongo, mambo ya ulimwengu na mambo ya Mungu, nuru na giza, mema na mabaya na kama Kristo, kwa namna za kidunia, mashujaa wetu jasiri hawakuitwa kuuridhisha ulimwengu. Wanapaswa kuukabili. Tunajua tunapigana vita ya kimwili, lakini hatimaye imejikita, kama hali ilivyo sasa…”
Msomaji wangu kwa leo inatosha, nilitamani kulitafakari hili na hili libaki katika kumbukumbu za dunia hii kipindi linatokea Mwanakwetu alikuwa anaishi duniani.
Mwanakwetu upo? Kumbuka:
“Mvivu wa Kutunza Siri.”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257






Post a Comment