Wafanyakazi wote walio katika Sekretarieti Ofisi ya Mkoa wa Mara wameambiwa kuwa kila mmoja atekeleze jukumu lake alilopangiwa kulingana na taaluma yake maana kila mmoja ni sura ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara na lazima watumishi wote kuwa mfano kwa jamii na kwa taifa zima la Tanzania.
Haya yameelezwa Februari 26, 2026 Mkoani Mara wakati wa ufunguzi wa kikao hiki kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Mara na Afisa Tawala na Rasilimali watu wa Mkoa huu ndugu Dominicus Lusasi katika mchakato wa maandalizi ya Bajeti ya 2026/ 2027 ambapo kikao hiki kilijadili mapendekezo ya Bajeti ya Sekretarieti kwa Mkoa wa Mara ambapo fungu 77 ndilo lilikuwa mezani, mwongozi ni kwamba lazima wafanyakazi washirikishwe:
“Katika majadiliano yetu tutoe ushauri na tujadiliane kwa maslahi ya watu wa Mkoa wa Mara maana haya majadiliano na mapendekezo yanakwenda katika Kikao cha Ushauri cha Mkoa wa Mara. “
Akizungumza katika ufunguzi wa Kikao hiki ndugu Lusasi aliwaomba wajumbe kuwa huru na kutoa maoni yao vizuri.
Awali Emmanuel Mazengo Mkuu wa Sehemu ya Uratibu na Tathimini aliwasilisha mapendekezo haya ya bajeti :
“Kulingana na mapendekezo ya Bajeti ya Sekretarieti ya Mkoa wa Mara kwa mwaka fedha wa 2026/ 2027 ni matumizi ya shilingi bilioni 5.1 kama mishahara na shilingi bilioni 4.7 fedha za matumizi mengineyo. Huku shilingi bilioni 6.1 fedha za ndani zinakwenda kwenye matumizi ya maendeleo nazo bilioni 2.5 fedha za ndani pia kwa ajili ya maendeleo. Jumla kuu ya fedha zote kwa matumizi ya kwa Sekretareti ya Mkoa wa Mara ni shilingi bilioni 18.3.”
Akichangia hoja katika kikao hiki Katibu wa TUGHE Mkoa wa Mara wakili Msomi Hamis Edward Mwisa aliuliza je bajeti hii waliyosomewa je pesa ya zawadi kwa wafanyakazi hodari ipo? Swali ili lilijibiwa na ndugu Mazengo kuwa ndiyo fedha za zawadi kwa watumishi hao hodari kutoka kila kitengo, idara na sehemu zimetengwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa TUGHE mkoa wa Mara John Isomani aliuliza fedha za bajeti ya sherehe za wanawake dunia zimepangiwa ?
Ndugu Lusasi alijibu kuwa bajeti ya shughuli hii kwa mwaka wa fedha 2025/ 2026 zilishapangwa ila kwa mwaka wa fedha ujao wa 2026/2027 zimepangwa na kilichosomwa ni muhtasari tu.
Kikao hiki cha Baraza la Wafanyakazi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Mara Kilikuwa na ajenda saba ambazo zilijadiliwa vizuri na kwa uwazi mkubwa kutoka kwa kila mjumbe na bajeti hii kupitishwa kwa kauli moja..
Kabla ya kikao hiki kuhairishwa Mwanakwetu alijaribu kutazama namna watumishi ambao ni wajumbe wa Baraza hili la Wafanyakazi walivyovaa, wote walikuwa wamependeza na mavazi yao yalilingana kabisa na kanuni za mavazi za utumishi wa umma wa Jamhuri ya Muungano Tanzania zinavyoagiza, katika mavazi haya macho ya Mwanakwetu yalivutiwa mno na gauni alilovaa , kumkaa na kumpendesha sana Afisa Tawala Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara Bi Mariam Majogo.
“Kwa hakika Bi Majogo alipendeza mno, tangu alivyosuka nywele zake, gauni lake, viatu vyake rangi ya zambarau huku akitembea kwa kujiamini kikaoni na kwa hakika Bi Majogo angeweza kutuwakilisha na mavazi yake haya pahala popote ambapo angeagizwa na mwajili lakini tatizo la Bi Majogo lilikuwa moja tu alikuwa anaigopa mno kamera ya Mwanakwetu.”
Kikao hiki kilifanyika katika mazingira tulivu, huku hali ya hewa ya mji wa Musoma ni nyuzi joto 23, unyevunyevu ni wa asilimia 70, ujirani na mvua ni wa asilimia 69 na upepo ukivuma kwa KM 8 kwa saa.
Mwanakwetu Upo?Kumbuka:
“Mtumishi wa Umma Sura ya Mwajiri.”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257






Post a Comment