Mazingira ya Elimu Jirani na Migodi ya Dhahabu Yaboreshwe

 

Adeladius Makwega-MBAGALA.

“Changamoto mojawapo ya wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari katika maeneo yenye migodi ni utoro maana wanafunzi hao wanaona ni heri ya kwenda kufanya vibarua katika migodi hii midogo midogo ambapo malipo yake kwa siku ni kati ya shlingi 15,000-30,000. Jambo la kufanya ambalo shule yetu ya Msingi ya Pakinyigoti inafanya ni kuhakikisha kwanza mazingira ya shule ni mazuri, huku wanafunzi wakipata huduma zote muhimu kama vile chakula cha mchana ambapo asubuhi wanakunywa uji na mchana wanakula kande.”

Haya ni maelezo ya Mkuu wa Shule ya Pakinyigoto, Mwalimu Nyatito Nyatito, Kata ya Ikoma Wilayani Serengeti Mkoani Mara wakati akifanya mazungumzo maalumu na Maafisa Elimu Mkoa wa Mara kadhaa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara mapema Februari 2, 2026.

“Shule yetu inawanafunzi 518 huku kwa matokeo ya darasa la saba mwaka wa 2025 darasa lenye wanafunzi 42 ni wanafunzi 39 walifaulu na wamepangiwa shule za sekondari maeneo kadhaa ya Tanzania hivyo hii ikiwa sawa na ufaulu wa asilimia 92.8.”

Mwalimu Nyatiti aliongeza kuwa kikubwa wana ushirikiano mzuri baina ya walimu, wazazi na hata viongozi wa makapuni yenye miradi kadhaa iwe madini na hata mbuga jirani na eneo lao huku changamoto zingine kama wanyama wakali nazo zikitatuliwa kwa wakati.

 

 

Wakilitazama suala la elimu kwa Mkoa wa Mara Mwalimu Kinyemi Sepeku Mgaza ambaye ni Afisa Taaluma anayeshughulikia darasa la nne amesema kuwa upatikanaji wa chakula cha mchana ni muhimu kwa wanafunzi wetu siyo darasa la nne pekee bali hata ngazi zingine za elimu.

“Unajua hata Chuo Kikuu kama unasoma kisha haupati chakula vizuri kwa utaratibu mzuri hauwezi kufanya vizuri kitaalamu, hivyo chakula cha mchana ni muhimu.”

Kwa upande wake mwalimu Haidi Jerome Sinene ambaye ni Afisa Taalumu Mkoa wa Mara anayeshughulikia Kidato cha pili alisema:

“Ni kweli nimetembelea shule kadhaa ikiwamo Shule ya Msingi Palonyingoti mazingira yake ninayafahamu vizuri, wanajitahidi ninashauri shule zingine wajifunze kwao.”

Akihitimisha mjadala huu Afisa Elimu Sekondari Mkoa wa Mara anayeshungulikia kidato cha nne na cha sita Mwalimu Ayubu Hezron Mbilinyi aligusia juu ya wale wanafunzi ambao hawakufikia kiwango cha ufaulu kidato cha pili ambao Serikali imeagiza waendelee na masomo amesema kuwa :

“Shabaha ni kuwapa nafasi za kuendelea masomo na siyo kushusa ufaulu bali wakiwa kidato cha tatu watapewa muda zaidi wa kusoma kupitia remedial classes na kikubwa hata ule muhtasari kwa waliyoyasoma mwaka uliyopita yaani 2025 kama wangerudia ingekuwa mzigo maana muhtasari mpya ndiyo unatumika kwa sasa kuwarudisha nyuma kukariri ilikuwa na kuwapa mzigo zaidi na kuwapoteza zaidi wanafunzi wetu. Mathalani Mwanafunzi DFG alitakiwa kufaulu kwa upata alama D tatu, hiki ndicho kigezo kama amepata D mbili maana yake redial classes zitamsaidia kufikia kigezo hiki ”

Wakati haya yakiendelea hapa Mkoani Mara, hali ya hewa ya Mji wa Musoma ni nyuzi joto 23 unyevunyevu ni wa asilimia 20, ujirani na mvua ni wa asilimia 81 na upepo ukivuma kwa KM 10 kwa saa .

 

Mwanakwetu upo? Kumbuka:

”Mazingira ya Elimu Jirani na Migodi ya Madini Yaboreshwe.”

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257
















 

0/Post a Comment/Comments