Maafisa Tehama na Maafisa Habari Mkoa wa Mara Wapata Viongozi Wao

 



Adeladius Makwega MBAGALA

Maafisa Tehama na Maafisa Habari walio chini ya TAMISEMI kutoka Mkoa wa Mara Februari 23, 2026 Wilayani Musoma wamefanya uchaguzi wa viongozi wao kadhaa ambao watakuwa wanawaongoza katika vikao kadhaa vinavyofanyika kila mara watakapokuwa wakifanya vikao vya maboresho ya kazi zao ndani ya taaluma zao.

Uchaguzi huo uliyosimamiwa na Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA mkoa wa Mara ndugu Ngobayi Mwisaalya ulimchagua Liwina John Mnamba kuwa mwenyekiti kwa kura zote thelatini huku Bi Amina Jason Chaula kuwa Katibu na muweka mikakati sawa ambapo Bi Chaula nayeye alijinyakulia kura zote thelathini.

“Ninawapongeza kwa kuchaguliwa katika uchaguzi huu, maana yake kazi ndiyo imeanza na sasa hivi nawaomba mje mkae viti vya mbele ya kikao chetu mtuongoze.”

Akikiongoza kikao hiki ndugu Mnamba ambaye ni Afisa Habari kutoka Halmashauri ya Mji wa Bunda alisema kuwa anawapongeza maafisa hawa kwa kumuamini na kuwa kiongozi wao katika mambo haya .

“Ninatoa ahadi nitawaongoza vizuri, kikubwa mwenye jambo tuwasiliane.”

Ndugu Mnamba ni mhitimu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kwa Shahada ya Uandishi wa Habari aliyohitimu mwaka wa 2022 kisha kuajiriwa na Halmashauri ya Mji wa Bunda.

 

Kwa upande wake Bi Chaula ni Afisa Tehama wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, huku akiwa ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe aliyehitimu mwaka wa 2024 Shahada ya Tehama katika Biashara na kisha kuajiriwa na Halmashauri ya Mji wa Tarime Mkoani Mara.

Mwanakwetu Upo?

“Maafisa Tehama na Maafisa Habari Wapata Viongozi Wao.”

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257







 

0/Post a Comment/Comments