Hatushauri Watoto Kufika Sehemu za Kutoa Huduma za Afya Wakiwa Wazima

 

Adeladius Makwega-MBAGALA.

“Mazingira ya kutolea huduma za afya iwe kambi za tiba, zahanati, kituo cha afya na hata hospitali siyo sehemu ya watu kutembelea kila mara na mara nyingi sisi watoa huduma za afya hatushauri watoto wadogo ambao wana afya njema kwenda nao mazingira haya…”

Haya maelezo yanatolewa katika jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, idara ya Afya na Ndugu Stanley Kajuna ambaye ni Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Mara.

“Maambukizi ya Magonjwa yanaweza kutoka kwa mgonjwa kwenda kwa mtu mwingine jirani awe mtu wa kawaida au mtoa huduma na hata maambukizii haya yanaweza kutoka katika mazingira ya kutoa huduma za afya kwenda kwa binadamu mwingine na ndiyo maana watoa huduma tunajikinga mno na maambikizi kadhaa ikiwamo kwa kujikinga na vifaa maalumu na wakati mwingine kupata chanjo maalumu. Ndiyo maana tunasisitiza chanjo kadhaa kwa watoa huduma kutolea kwa wakati ili kulinda usalama wa watoa huduma kazini. Katika ili Mkoa wa Mara tunafanya vizuri maana watoa huduma wetu wote iwe katika taasisi wa umma au binafsi wanapata chanjo hizo kwa wakati na jambo tunashauri lizingatiwe nchi nzima.”

Ndugu Kajuna alisema kuwa katika mila za kiafrika kuna changamoto kubwa ya jamii kuwa pamoja na mpendwa wao pale anapokuwa kwenye shida mathalani ugonjwa, familia nzima inaweza kufika hospitalini kumuona mgonjwa, hivyo basi pengine mgonjwa akawa anashindwa kula, ukoo mzima unakaa naye huku wakila naye mgonjwa ili kumtia moyo.

“Huu ni utaratibu mzuri, huu ni upendo mkubwa lakini kwa hali ya magonjwa iliyvo ya sasa tunashauri jamii yetu kuepuka haya wakati wanapokuwa maeneo ya kutoa huduma za afya.”

Wakati Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Mara ndugu Kajuna anazungumza haya kandoni alikuwa akirejea vitabu viwili kutoka Wizara ya Afya ambavyo ni Standard Operating Procedures For Infection Prevention And Control in Tanzania na National Infection Prevention And Contol Guidelines For Health Services in Tanzania. Wakati haya yakiendelea hapa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara huduma kadhaa zinaendelea kutolewa huku wananchi wakifika kuonana na viongozi kadhaa hasa Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Alfred Mtambi na majina yaliyonukuliwa katika kitabu cha wageni katika Ofisi hii ya umma ni mengi wakimuona Kanali Mtambi, miongoni mwao ni Bi Elizabeth Mwaka kutoka Musoma Mjini aliyeingia saa 3 kamili ya asubuhi naye Aruko Mcharo kutoka Tarime aliingia saa 5. 46 ya asubuhi. Wakati haya yakiendelea hali ya hewa ya Mji wa Musoma ni nyuzi joto 24, unyevunyevu ni wa asilimia sufuri, ujirani na mvua ni wa asilimia 65 na upepo ukivuma kwa KM 10 kwa saa.

Mwanakwetu upo?Kumbuka:

“Hatushauri Watoto Kufika Sehemu za Kutoa Huduma za Afya Wakiwa Wazima.”

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257

 

 

 

 

 

0/Post a Comment/Comments