Elimu Wachimbaji Madini Inapunguza Madhara Migodini

 



Adeladius Makwega-MBAGALA

“Wewe ni mwana wa nani?Mimi ni Mwana wa Masanja, natokea Mwanza ila nipo huku nafanya kazi zangu. Kumbe! Sawa sasa unapatikana wapi? Napatikana jirani tu na jirani na uwanja wa Ndege wa Musoma nafanya kazi zangu.

Karibuni sana maana nyie ni kaka zangu?”

Vijana hawa wa Kisukuma mmoja wao akasema tukija kwako wanapatikana wanawake weupe? Vijana hawa Wakisukuma wakaendelea kuongea na mama huyu huku mama huyu akiongeza spidi huko aendapo.

“Eheee mzee …Maana sisi Wasukuma tunawapenda sana wanawake weupe…”

Haya ni majira ya mchana, Februari 13, 2026 Mwanakwetu yu nje kidogo ya Mji wa Musoma katika machimbo ya Kokoto na Mchanga ambapo kulikuwa kunafanyika mafunzo ya vitendo ya ulipuaji wa miamba kwa kutumia baruti kama yalivyokuwa yakitolewa na Chuo cha Madini Dodoma na Ofisi ya Kanda ya madini ya Mkoa wa Mara kwa juma nzima tangu Februari 9 hadi 13, 2026. Mazungumzo haya ya wanamke weupe ni ya vijana wa Kisukuma ambao walikuwa wanashiriki mafunzo mara baada ya Mwanamke mrembo kupitia kati yao ambaye alikuwa ni Mnyakyusa huku akifahama Kisukuma vizuri sana hivyo basi wakampenda huku wakimuuliza anapatikana wapi? Ndipo mama huyu anayejua akaanza kuongea nao nae Mwanakwetu alikuwa kando akisikiliza soga hizo huku kijana mmoja kando akimtafsiria



Katika kundi la hawa vijana watano alikuwepo kijana mmoja maarufu kama Abdul , yeye peke yeke alikuwa Mluguru anayetokea Dar es Salaam Yombo Dovya Jirani na makaburi ya Wakristo huku alikuwa hafahamu Kisukuma lakini sasa yupo Mkoani Mara akijishughulisha ulipuaji wa baruti katika migodi kadhaa.

“…migodi yote ya madini yapo madai kuwa wamejaa vijana wa Kisukuma na Kinyamwezi ambao ndiyo wanaofanya kazi hizo kwa wingi na kweli hata kundi letu la vinaja watano Mluguru peke yangu na Wasukuma wanapendana sana si unaona wanavyomtania dada huyu anayepita jirani yao.”

Msomaji wangu kumbuka sasa mafunzo haya yanatolewa kwa vitendo hapa mgodini, kwanza ilioneshwa namna bora ya kulipua baruti katika mlipuko mdogo ambapo zoezi lilifanyika vizuri na kisha vijana hawa kuuliza maswali na kujibiwa.

Awali mafunzo haya yalianzia darasani kwa kujifunza kwa nadhalia kisha kwa vitendo ambapo washiriki wawili tu ndiyo walikuwa wanawake ambapo alikuwepo Bi Veronika Hamisi na Lilian Maiko.

Wote kwa pamoja walisema wamevutiwa na mafunzo haya huku Bi Hamisi akisema kuwa kazi hii anaifanya sasa kwa miezi minne awali alikuwa muuza mbogamboga huku kwa siku moja anaingiza kati ya shilingi 100,000 na 150,000 huku analipua shimo moja kwa shilingi 5000 huku wakati mwingine anaweza kulipua hadi mashimo 50.

Mwanakwetu akiwa hapa alijiuliza na kustajabishwa sana inakuwaje wanaume mafunzoni ni wengi lakini wanawake ni wachache?

Kulijibu swali hili Injini Salumu Kajo kutoka Chuo cha Madini Dodoma aliyasema haya:

“Hoja hii inachangamoto hata chuoni Dodoma, katika mafunzo haya unaweza kuona wanawake wapo watatu tu huku wanaume wanafika 100 hapa nashauri wanawake kujitokeza zaidi huku makampuni ya migodi kuwafadhili wanaweka kushiriki mafunzo haya. “

Kwa hakika wa kila mshiriki wa mafunzo haya alionesha kuvutiwa na mafunzo haya maana walisema kuwa kushiriki mafunzo ya elimu bora ya uchimbaji wa madini inasaidia kwa mlipuaji na mchimbaji wa madini hasa wale wadogo wadogo ili wabaki salama maana kinyume chake unaweza kupoteza maisha na kutofikia shabaha yako uliyokusudia, elimu ni muhimu kwa usalama wa mchimbaji madini.

Mwanakwetu alishuhudia mafunzo haya kisha baadaye kurudi nyumbani kwake na jua lilikuwa limezama na baadaye kuamua kuyaandika makala haya kama unavyoyasoma msomaji wangu.

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Kwa hakika elimu ya uchimbaji wa madini ni muhimu hasa kulinda uhai na usalama wa wachimbaji wadogo wadogo na hata jamii jirani na mdogo. Hii elimu kama itatolewa kwa kina, inaweza kupunguza sana madhara huku itasaidia vijana wengi kujishungulisha na uchimbaji madini na kujiongeza kipato , hapa msomaji wangu rejea kisa cha kijana Abdul kutoka Yombo Dovya Dar es Salaam akisafiri KM zaidi ya 1000 kutafuta pesa migodini, huku vijana wa Kisukuma kadhaa wapo bado nab ado tena vijana mabintiwawili Lilian Maiko na Veronika Hamisi ambapo yeye(Veronika) anajipatia kipato kikubwa kwa kulipua baruti tu.

Msomaji wangu kumbuka vijana watano na wasichana wawili maana yake vijana saba ni baadhi tu walinukuliwa na Mwanakwetu katika makala haya huku kundi ya vijana zaidi ya 100 wakijipatia mafunzo haya ambayo ni mkombozi kwa vijana na wachimbaji wadogo wadogo wa madini nchini Tanzania.

Mwanakwetu upo? Kumbuka:

“Elimu ya Uchimbaji Madini Inapunguza Madhara Kwa Wachimbaji Wadogo Wadogo.”

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257

 

 





0/Post a Comment/Comments